Mfahamu kinyonga

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,425
Kinyonga ni kiumbe mwenye sifa ya kuwa na rangi nyingi, kiumbe huyu pamoja kuwa na sumu kali lakini ni mpole na hana matumizi mabaya ya sumu hiyo, ni kiumbe anayeogopwa sana japokuwa si mtata, pengine yawezekana ni mkwala wake anaotoa kwa kupanua mdomo wake anapohisi hatari au muonekano wake tuu, mbali na kuwa na macho yanavutia lakini pia ana sifa ya kutembea taratibu sana, si kwamba hawezi kabisa kuongeza spidi la hasha hata akiiongeza bado haitaweza fanana na viumbe wengine kama mjusi, hata hivyo usije fikiri hana wanyonge wake katika mwendo wapo wengi tuu hawamfikii mwendo kinyonga, kama jongoo, washawasha na hata konokono.

Duniani kuna aina zaidi ya 100 ya vinyonga chakula chake kikuu ni wadudu, kama kumbi kumbi, nzi, na wengineo wa aina hiyo, Madume wa vinyonga ndio huishi miaka mingi zaidi ya 2 na isiyozidi mitano, wakati majike huishi muda mfupi sana kwakuwa punde tuu wanapozaa hufa.

SIFA ZA KIPEKEE ZA KINYONGA.

1. Hubadiri rangi kutokana na mazingira
Sababu kuu ya kufanya hivyo ni kujikinga na maadui asionekane kwa urahisi, maana uwezo wake katika mapambano ni Mdogo.

2. Huweza kuelekeza macho yake sehemu tofauti.
Kinyonga ana uwezo jicho lake moja kutizama vitu vya mbele na jicho lake la pili akatizama nyuma na yote yakifika katika ubongo yakachambuliwa.

3. Ulimi wake ni mrefu kuliko mwili wake wote.
Hivyo silaha yake kubwa wakati wa mawindo ni ulimi wake ambao huweza kuurusha mbali pindi atafutapo chakula chake.

4. Kinyonga huwa hazai
Maumbile ya jinsi yake huwa hayawezi kutanuka hivyo namna pekee ya kuwatoa watoto wake tumboni ni tumbo lake likimzidia uzito tuu, hujiachia toka juu na kupasuka ndipo watoto hutoka na mama kufa.

5. Kinyonga huanza kujitegemea kuanzia sekunde aliyozaliwa.
Na hii ni kutokana na mama yake anapokufa ili azae.

6.Kinyonga ni kiumbe anayethamini sana usalama.
Na ndio maana hata atembea hujiuliza Mara Mbili kabla ya kushusha mguu wake.

7. Hapendi kuonekana onekana sana

8. Huzaliana sana wakati wa mvua

9. Hupendelea kukaa kwenye miti yenye matunda matunda

10. Sumu yake kubwa ni ugoro, ukimpa hiyo kitu atahangaika sana kabla ya kifo kumpata.

11. Anapopata maumivu hubadilika badilika rangi na hiyo humsaidia kupunguza maumivu.

12. Macho yake huzunguka

13. Pamoja na kubadirika badirika rangi lakini kila kinyonga ana rangi yake kuu.

14. Wapo vinyonga wenye rangi nzuri sana hasa ile kuu.

15. Vinyonga pia hutofautiana kutokana na aina zao, wapo ambao huwa na nundu kichwani, wapo wenye pembe, wapo wanaovimba mashavu, wapo wenye mapezi kama samaki no.

16.Mikono yake ina chembe chembe za nta akikukamata mpaka aamue yeye kukuacha au wakupeleke kwa shangazi yako akutoe (sasa kama shangazi naye muoga unalo) hahahahaha

#Mwisho
Nchi nyingine huwafanya vinyonga kama mapambo ya ndani, je ukipewa watano na maliasiri waweza weka chumbani kwako na umeme huu wa mashaka ?

Hahahaha !
 
3.ulimi wake ni mrefu kuliko mwili wake wote.

Ngoja nikuongezee picha maana uzi bila picha haunogi
IMG_20190102_065630.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ati akikukamata hadi shangazi yako aje. Shangazi wa nini wakati ugoro tu unamuondoa duniani chini ya dk 2! Nilimfanyia majaribio mmoja huko Moro tena mimi ndio nilimkamata yeye.
 
Similar Discussions

25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom