Mfahamu kijana mdogo mpambanaji Solomoni Mahlangu


Vladimir Lenin

Vladimir Lenin

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Messages
1,750
Points
2,000
Vladimir Lenin

Vladimir Lenin

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2018
1,750 2,000
Asante sana, Pale Sua-Kampasi ya Mazimbu kuna shule ya msingi Solomon Mahlangu nimepita sana mitaa hiyo sikuwa najua historia ya huyu mtu.
Yaa mkuu shule ya longi sana nakumbuka nilikuwaga nampeleka mdg wangu na baiskeli
 
infinix

infinix

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2018
Messages
523
Points
500
infinix

infinix

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2018
523 500
mbona hakuna mahali ambapo alifanya tukio korofi?
zaidi ya kukimbia kwao Na kwenda kujifunza ugaidi hatimaye kukamtwa kizembe pasipo kufanya tukio
Wewe mwenyewe huna ujasiri,ndiyo maana umekubali kuwa kibaraka wa bwana yuleeeee
 
Inferior Complex

Inferior Complex

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Messages
3,603
Points
2,000
Inferior Complex

Inferior Complex

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2014
3,603 2,000
Wewe mwenyewe huna ujasiri,ndiyo maana umekubali kuwa kibaraka wa bwana yuleeeee
sawa Mimi Sina ujasiri je,wewe umechukua hatua Gani za kupambana na "Bwana Yule"?
 
A

Apeche Alolo

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2017
Messages
1,154
Points
2,000
A

Apeche Alolo

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2017
1,154 2,000
Anaitwa Solomon Kalushi Mahlangu,alizaliwa mwaka 1956 tar 6 ,April na akafa 1979.alikuwa moja ya kijana mpambanaji Afrika kusini ,kipindi cha utawala wa makaburu (Dutch/Boaers colonialists).

Mama yake alikuwa anaitwa Martha Mahlangu ,baba yake alikufa 1962 hivyo alilelewa na Mama ,alikuwa na kaka na ndugu zake wengine.

Alikuwa anasoma Mamelodi high school ,darasa la 8,ila akiwa shule alikuwa akiumia juu ya ubaguzi uliokuwa ukiendelea ,sheria mbalimbali za kibaguzi kama sheria ya kibali cha kukaa na kupita maeneo ya mjini ,ambayo ndio sheria zilizopelekea maandamano makubwa ,yakiratibiwa na viongozi wa ANC ,Mandela ,oliver Tambo,Walter sisulu maandamano kuelekea kituo cha police huko mji wa Sharpervil kupitia Transvaal mwaka 1960 ,tar 21 march ! Yaliyopelekea watu wengi kufa na kuitwa Jina SHARPEVIL MASSACRE mauwaji ya Shapervil ,watu wengi walikufa.

Mahlangu akiwa bado kijana mdogo ana miaka minne,mauwaji haya yalipelekea chama cha ANC kufutwa kabisa, hii ikapelekea Nelson Mandela na wapiga naji wengine kuazimia kuunda kikundi cha mapigano sababu njia ya amani imeshindikana kabisa,kipindi hiko SOLOMON MAHLANGU ana miaka 5 ,akiwa chini ya malezi ya mama yake.

1961 ,December 16 .Mandela alitoa hotuba iliyoitwa "Am prepare to Die " Najiandaa kufa ,kutoa hamasa kwa wapiganaji kuanzisha mapambano dhidi ya ubaguzi wa Rangi ,kikundi kikaundwa kiitwacho Umkhonto We Sizwe (MK) (spear of the Nation)mkuki wa Taifa,kikundi cha wapiganaji .Manifesto ya UMKHONTO we SIZWE ilitolewa kuonesha malengo na dhumuni. Mandela aliandika Barua kwenda kwa Makaburu ikachapishwa kwenye Gazeti kuwa kama hawatakubali kubadili katiba na sheria juu ya ubaguzi mashambulizi dhidi yao yataanza kwa kasi.

1976 ,Mahlangu alikuwa shule akisoma ,kutokana na magomo iliyokuwa yakiendelea shule tofauti tofauti yakiongozwa na wanafunzi weusi ,ilipelekea shule nyingi kufungwa ,hivyo 1976 shule zilifungwa .

Mahlangu alirejea nyumbani akiwa na uchungu na maumivu saana ,akiwa na miaka 20 kipindi hiko hiko 1976,aliamua kuondoka nyumbani kwenda kujiunga na kikundi cha mapambano kiitwa UMKHONTO WE SIZWE hakuaga ila aliacha barua chini ya mto wa kulalia wa kaka yake ikisema ,"Boet Lucas,Boet Lucas ,Boet Lucas Don't look for me ,l have left and you will never find me (Boet Lucas ,Boet Lucas ,Boet Lucas usinitafute nimeondoka na hautanipata )

.kikundi hiki cha wapiganaji kilikuwa na vituo mbalimbali vya mafunzo ya kikamanda,Mozambique, pia Angola .

1976 ,aliingia Angola na 1977 aliingia Mozambique kupokea mafunzo ya kikamanda kupambana na Makaburu. Katika kikosi kiitwacho ENGENEERING huko Angola alipata mafunzo ya combat,Scout ,pia siasa .

Walikuwa wakipewa kutekeleza operations na missions mbalimbali za uvamizi ,Operation na mission kwao ilikuwa ni ya kurudi south Afrika kupitia Swiziland kutokea John'sburg kusaidia mapigano ya wanafunzi wa SOWETO.wakiwa watu watatu ,Solomon, George Lucky na Motloung .

Walifanikiwa kuingia Swisziland wakaonana na General, Siphiwe Nyanda ,aliyewapa mkoba wa Suitcase kila mmoja ,iliyowekwa makaratasi juu chini Bunduki za AK-47,mabomu ya mkono ya kurusha(Grenades).

Tar 11,June 1977 walivuka mpaka kuingia John'sburg ,wakiwa katika mtaa wa eneo la TAXI ndani ya Diagonal street ndani ya John'sburg ulinzi wa police ulikuwa mkubwa sana ,kila pande na wao walitaka kupata taxi liwapeleke SOWETO huko ktk mapigano ya wanafunzi.

Police wawili waliwatilia shaka na kuwapiga chini ya ulinzi kukagua zile SUITCASE ,police alisema "_laat ek sien wat het julle dar" "naomba niangalie kilicho katika mikoba yenu" wakanyanganywa mara bunduki ikandondoka ,loooh

Ikabidi wakimbie kuelekea ,mtaa wa Goch ,Goch street wawili Motloung na Solomon wakaingia katika Duka la John Orr's ,Duka mauzo na store ila wakati wanakimbia Solomon alipigwa Risasi ya mguu ,walipoingia Dukani ,Motloung alimimina Risasi kwa wafanya kazi kadhaa mule ndani ,baada ya Muda police walizunguka jengo na kuwakamata.

Wakawekwa Gereza la John varster square Prison,mama yake solomon,Martha alienda kumuona huko akawa analia kwa uchungu mbele ya mtoto wake na polisi wa kizungu.Solomon alimwambia mama yake .

"why are you crying in front of these dogs ,I don't care what they do for me ,and if they spill my blood ,may be it will give the birth of other Solomon" "kwani unalia mbele ya hawa mbwa ,sijali wanavyonifanyia na hata kama wakimwaga damu yangu ,kuna uwezekana damu yangu ikazaa Solomon wengine .

Solomon alifikishwa Mahakamani, kwa kosa la kuuwa yeye na Motloung na kosa la Ugaidi ,ikiwa wamepigwa hadi hawawezi simama kwa siku 90 walozokuwa huko Gerezani ,na Solomon ubongo wake ulikuwa tayar umeathirika kwa kipigo,

Solomon akitetewa na mawakili 2 ,waliowekwa na wazazi wake ,wakili msomi Ismail Mohammed,na Clifford Mailer ,mwaka 1977 Nov.7 ,alihukumiwa kunyongwa yeye na mwenzake kwa sheria ya ugaidi,kuuwa wakitumia sheria pia Common purpose law ,na hakuruhusiwa kukata Rufaa.

Tar 6,April 1979 ndio siku aliyonyongwa ila kabla ya kunyongwa alitamka maneno haya,akiwa na umri wa miaka 22 tuu

" Tell my people that l love them ,and they must continue the fight ,my blood will nourish the tree that will bear the fruits of freedom, Aluta continue!! " "waambie watu wangu kuwa nawapenda nawaendelee mapambano, damu yangu itarutubisha mti ambao utazaa matunda ya uhuru ! Mapambano yaendelee!! " akanyongwa.

Solomon anachukuliwa kama mpambabaji atayeishi katika kumbukumbu milele ,niwazi walio mnyongo wamekufa au watakufa na hawatakumbukwa milele ila Solomon aliacha alama hadi Leo anakumbukwa.

1.kijijini kwao limejengwa sanamu lakr,Solomo Mahlangu freedom square

2.Durban kuna mtaa unaitwa Mahlangu ,

3.Jengo la uongozi (Administration building)chuo cha Witwatersrand, 2016 ilibadilishwa na kuitwa Solomon Mahlangu House ,kufuta jina la awali Senate House.

4.pia kuna SOLOMON MAHLANGU FREEDOM COLLEGE .

5. 2017 Ilitengenezwa film ya maisha ya Solomon inaitwa KALUSHI .

6.Tanzania, chuo kikuu cha Sua Campus zake 2 ,Morogoro zinaitwa Solomon Mahlangu Campus.

Ujasiri kukemea uovu huzaa heshima,na utu katika jamii yako hata ukifa leo utakumbukwa ,unafiki na ubinafsi huzaa dhambi ya mauti ,na hata kama ukifa leo hutakumbukwa.

Abdul Nondo.
abdulnondo10@gmail.com.
Solomon Mahlangu's tombstone.
 

Forum statistics

Threads 1,285,016
Members 494,369
Posts 30,847,424
Top