Mfahamu Kelvin Bokai Doe, aliyeishangaza dunia

wapo mkuu yupo jamaa yangu flani hivi pande za Njombe aisee jamaa ni Ginius wa ajabu yaani hua nashangaa anaweza kusuka inverter,transiformer,amplifaya
radio,transimiter
Na mavitu kibao ya umeme na hajasoma popote secondary kwenye maabara ya physics aliacha makolo kolo ya kutosha aliyoyatengeneza na kuacha kama alama
Cha ajabu sasa jamaa ni inteligent balaa kupitia yeye ndio niliwajua kina Tesla & Co kiundani

Hilo getto lake sasa lina makololo kibao hakuna kitu cha kieletronic hatengenezi yani kwenye ukuta kajaza formula za kila namna yaani kama unataka fuma sabuufa anakuonesha mfumo wake wote


Ila cha ajabu tupo naye kitaa sababu nchi yetu tunaijua wenyewe ila jamaa yupo njema sana ikitokea mdhamini aende mambele tutamsahau ndani ya wiki genius haswa!
Ungetengeneza Thread apate watu wamtoe ,jamiiforums kuna watu mkuu
 
yupo.mwingine anaizwa frank wire,yuko mabibo,walimchukua watu wa tume ya sayansi na teknolojia, baadaye akaona wanamzingua tu,siasa nyingi
 
Kuna ukweli fulani kwamba watu wanazidiana uwezo, hatuwezi kuwa sawa wote.

Ila, naona kama hizi habari za u genius zinakuwa overrated, watu wanapenda stories dramatic.

Naona kama mazingira yakichanganywa na utashi wa mtu, yakiendelezwa na ung'ang'anizi wa kutaka kupata matokeo, mambo haya yana nafasi kubwa ya kufanya kile kinachoweza kuonekana kama maajabu ya ma genius.

Jamii zetu zina matatizo mengi ya kimazingira, wengi wanashindwa kwa sababu mazingira hayako rafiki.

Na mazingira haya yasiyo rafiki pia yanadumiza utashi. Na ninaposema mazingira sina maana tu ya laboratories na vifaa, hata utamaduni ni sehemu ya mazingira. Jamii zetu zina utamaduni wa ku penalize failure sana. Hatuna room for experimentation and allowance for failure while perfecting a craft, ndiyo maana tunapenda sana hizi imani za "hawa ma genius, hawa wajinga kabisaa".

Sasa unapochanganya mazingira haya na utamaduni wa ku penalize failure sana, hapo automatically unaua utashi wa watoto, watoto wanaogopa kucheza kwenye matope wakirudi nyumbani watachapwa, wakati inawezekana kucheza kwenye matope ndiyo kunajenga akili ya ubunifu, kutengeneza vigari vya udongo nk. Mtoto kakua amekatazwa kugusa redio ya baba, hata utashi wa kuisogelea kujiuliza redio inawezaje kunasa sauti inakuwa tabu.

Mimi nakumbuka mwaka 1993 baba alikuwa na laptop anatuonesha anavyocheza mchezo wa chess na laptop, lakini laptop ile ilikuwa huwezi kuigusa mtoto! Of course wakati huo laptop ilikuwa kifaa cha bei mbaya sana so I understand. Baadaye alikuja kuona umuhimu wa kuwaandaa watoto kwenye teknolojia.

So, katika jamii kama hii ambayo watoto wanaonekana "ni dunia ya kesho", hawaaminiwi kushirikishwa kwenye teknolojia, wao wenyewe wanakosa utashi, na wakikosa utashi, ni vigumu sana kuingia katika ung'ang'anizi.

Kuna watu wachache wanaweza kufanikiwa kuwa katika mazingira mabaya, wakabaki na utashi, wakawa na ung'ang'anizi, wakalazimisha hata kuvumbua vitu vyao.

Na sisi tukiona watu hao, wenye utashi na ung'ang'anizi, pengine wanaorudia sana kujifunza, tukija kuona matokeo, ndiyo tunawaita ma genius.

Mimi naona ni kweli watu wanazidiana uwezo, hata kibaiolojia tu haiwezekani wote tuwe sawa.

Lakini, kuzidiana huku uwezo kunakuwa exaggerated, watu wengi ambao wanapata mazingira mazuri, wana utashi na wana ung'ang'anizi, wanaweza kupata mafanikio makubwa kama hao tunaowaita ma genius.

Kuna mtu aliniita genius siku moja, nikamwambia tafadhali sana naomba usniite hilo jina. Kwa sababu, nafanya kazi sana kusoma ili kujua mambo mengi ninayojua, na wewe ukiniita genius, ni kama unadogosha ile kazi kubwa niliyofanya, unanifanya kama mtu anayejua mambo mengi tu bila kufanya kazi, kwa sababu yeye genius.

Mimi naona kuwaita watu hawa ma genius ni kama tunadogosha kazi wanazozifanya kujua mambo mengi.

Na wengi tuna uwezo wa kuwa kama wao.

Tatizo linakuja, hata ukiwa na mazingira mazuri, unaweza kufanya sacrifices za kuacha kujumuika na wenzako kwenye gumzo, michezo, bar, wachumba etc, uweke king'ang'anizi katika utafiti wako mpaka kieleweke?

Hapo ndipo wengi tunaposhindwa.
 
Vijana kama hawa wapo wengi tu huwa wanaibuka lakini baadae hawaendelezwi wanaishia mitaani au kufanya vitu tofauti na hizo fani..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom