Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Mwanamke (yule Babeli) wa Ufunuo 17 anaelezwa kuwa

“alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, Siri [2 The. 2:7], Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba” [Ufu. 17:5, KJV].

Asema hivi yule Nabii:

“Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.” Babeli anatangazwa tena kuwa ni “mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.” Ufunuo 17:4-6,18.
ae7a1c4de023bbda2da0a25e30e725f6.jpg

Tyndale aliuliwa na utawala wa kipapa kwa kutafsiri biblia...



Mamlaka ile iliyodumisha utawala wake wa kidikteta juu ya wafalme wa Ulimwengu ule wa Kikristo kwa karne nyingi ni Roma. Rangi ile ya zambarau na nyekundu, dhahabu na kito cha thamani, na lulu, huonyesha waziwazi picha ya utukufu wake na fahari yake iliyozidi ile ya kifalme [angalia pia rangi za sare za viongozi na mapambo yao],
da95cf61b762f5a8bb3ffa13c0e24c5f.jpg

b601c77df03518a6574d5fdbdf97b1ea.jpg


mambo ambayo jimbo lile la Roma ( Vatikani), lenye majivuno makuu, lilijigamba kuwa nayo. Wala hakuna mamlaka [serikali] nyingine ambayo kweli ingetangazwa kuwa ilikuwa imelewa kwa damu ya watakatifu,” kama ya kanisa lile ambalo kwa ukatili mbaya sana limewatesa wafuasi wake Kristo.

Babeli pia anashtakiwa kwa dhambi ya kuungana isivyo halali [kuzini] na “wafalme wa nchi.” Ilikuwa ni kwa njia ya kujitenga mbali na Bwana, na kuungana na washenzi [wapagani], ndipo kanisa lile la Kiyahudi likageuka na kuwa kahaba [Soma Ezekieli 23]; naye Roma [kama kanisa], akifanya uasherati [ukahaba] unaolandana kabisa na ule na kutafuta msaada [kuungwa mkono] toka kwa mamlaka [serikali] zile za kidunia, anapata lawama iyo hiyo.

014c67cfdb1f454cb6ffad5c5931e2e5.jpg

2d74043e7497ad8b2d6a027cbaa597c5.jpg
 
Here we go again. Seventh Day Adventists (Wasabato) at work. Yaani bila Papa na ukatoliki hamna dini. Hata hiyo misingi ya Usabato huwa mnaihubiri saa ngapi kama kazi yenu kuu ni kupambana na Papa na ukatoliki 24/7? Nyinyi mnaamini nini? Wokovu unapatikanaje? Kwa kusoma na kufuata mafundisho ya Bibi Ellen G. White? Kwa kutokula samaki wenye magamba, wanyama wasio na kwato zilizogawanyika na wale wasiocheua? Ni kwa kuabudu Jumamosi? Ni kwa kutokunywa chai, kahawa na soft drinks? Ni kwa kukurupuka na kuwa na kiherehere cha kuhusisha kila tukio na unabii wa vitabu vya Daniel na Ufunuo? Usabato ni nini? Mtu atakwenda mbinguni kwa sababu ni Msabato?

Inawezekana kweli Papa ni ajenti wa shetani na kahaba mkuu wa Ufunuo lakini je, hili linawasaidiaje nyinyi kama Wasabato? Mbona mko so obsessed na Papa na Wakatoliki? Dini na madhehebu mengine yote yako sawa isipokuwa Wakatoliki? Mbona siwaoni mkiwachimba mf. Mormons au Jehova's Witness? Why Catholics only? Au mna bifu la kihistoria na Papa na ukatoliki?

Samahani kwa maswali mengi na natumaini kwamba hutatoa povu na badala yake utajaribu kutuelimisha kuhusu kikundi hiki cha kifarisayo (washika sheria za Musa) kiitwacho Seventh Adventists, kiundi chenye mauzauza mengi yasiyofungamana na mafundisho ya Biblia.

Anyway, Happy New Year mkuu (kama mnasherehekea mwaka mpya)! Naona mwaka mpya Wasabato mmeuanza vizuri na Wakatoliki aisee mpaka waombe poo . Post zaidi ya 7 hivi za kuanika ushetani wa Papa na ukatoliki tangu 2017 uanze. Ingekuwa mnashambulia let's say Uislamu naamini threads zenu zingekuwa zinafutwa. Komaeni na "mashetani" na "makahaba" wa kikatoliki mpaka kieleweke ila tu hakikisheni kuwa na nyie mko sawa kiimani!
 
Vikombe vinagongana kabatini leo. Kumbe kuna mambo mengi yamejificha nyuma ya kanisa ambayo watu wengi hawayajui. Aiseee.

Kweli ukiwa bendera unaweza ukapelekwa pelekwa tu na upepo pasina kujua. Mungu awafunue macho mpate kuiona ile kweli iliyo na ukweli.

MUNGU AWATOE UPOFU WA MILELE.
 
huenda ukawa "sahihi" na mapokeo uliyopokea toka kwa wanazuoni wa kikundi chako cha kisabato nawe kuendelea kuwahadaa walimwengu wasio na elimu ya dini na ya imani ya kikatoliki, ila swali langu, je Mungu huwaacha wenye haki wapotee..?? kama siyo, "haki" ipo katika "usabato" (kwa mujibu wa mafundisho yenu), na usabato una karibia miaka 200, je kwanini kikundi hiki cha wenye "haki" mbali na kutumia maarifa yao kueneza "haki" kwa "wasio na haki"?... kwanini utawala wa "kishetani" (kanisa katoliki/waprotestitanti) halijawahi kuadhibiwa na Mungu kwa Mungu kuwaonesha "wenye haki" njia sahihi???
 
Safi Sana Kwa uzi nzuri Sana. Kama huko nyuma kofia ya alama ya Mnyama 666 ilivaliwa na Papa. Wakatoliki wanashindwa kuoji Nani aliyekabuni kofia Ile na alikuwa na cheo gani huko Vatican na lengo Lake ni nini, je alikuwa ni mtu mmoja au kikundi . Kwa nini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa Kwa mbunifu wa Ile kofia. Badala yake tunaambiwa kofia ilipigwa marufuku, Kwa nini Ile alama ya Mnyama 666 ilionekana watu wakashtuka. Fikira huru inakuja baada kuwa unbiased
 
huenda ukawa "sahihi" na mapokeo uliyopokea toka kwa wanazuoni wa kikundi chako cha kisabato nawe kuendelea kuwahadaa walimwengu wasio na elimu ya dini na ya imani ya kikatoliki, ila swali langu, je Mungu huwaacha wenye haki wapotee..?? kama siyo, "haki" ipo katika "usabato" (kwa mujibu wa mafundisho yenu), na usabato una karibia miaka 200, je kwanini kikundi hiki cha wenye "haki" mbali na kutumia maarifa yao kueneza "haki" kwa "wasio na haki"?... kwanini utawala wa "kishetani" (kanisa katoliki/waprotestitanti) halijawahi kuadhibiwa na Mungu kwa Mungu kuwaonesha "wenye haki" njia sahihi???
Kama usabato una miaka200 napata mashaka na kitabu cha biblia...sababu sabato imetajwa toka kitabu cha Mwanzo na hata kutoka...na maana yake walikuwepo wasabato waabudu sabato waliofuata usabato huo. Swali langu ni Je, ni nani aliuleta usabato huo wa kuanzia kipindi cha Musa nk!? Na je ni nani aliuleta Uroman Cathoric!? Na Je uromani ulianza lini na nani aliuanzisha!?
 

Similar Discussions

17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom