Mfahamu Jaili: Chinja chinja aliyevuma Mbeya na Mama yake aliyekufa na kufufuka mara tatu

Mkuu hapo pa ikuti umekosea hawa jamaa wanapatika mkondo wa chuo cha magereza ukipita pale chuo kuelekea juu ndio kijiji cha hao malamanyafu ikuti iko nyuma ya magereza na huo mto songwe upo mpkani mwa tanzania na malawi kutoka kwa hao malamanyafu ni zaidi ya km 200
Wewe jamaa acha kutuchafua watu wa kijiji chetu sio cha hao wanyamanyafu.
 
Kuna mzee mmoja naye alikuwa anaitwa Mwanjisi alifanya biashara ya Hiace, sifa ya gari ya ni ilikuwa imechoka sana naye alikuwa na stori za mauza uza. Hivi bado yu hai?

Sent using Jamii Forums mobile app
Baba Bato alikuwa anavutavuta Sana bangi, ndiye mwanzilishi wa route ya Majengo Iyela kupitia Uwanja wa Ndege wa zamani.
 
Unamkumbuka Mzee Miraji wa Joka Road? Alikuwa na nyumba yake mtaa huo, nyumba ilikiwa na mahindi yamelimwa na yametoa mbelewele, Sasa kukawa na jamaa wanachunga ng'ombe, wakaingiza mifugo kwenye hicho kibustani cha mbele ya nyumba, wale wanyama wakapigwa upofu, na wale vijana wachungaji wakahangaika siku nne kwenye hicho kibustani wanatafuta njia ya kutokea wasiione.
Hili neno mbelewele sijalisikia siku nyingi sana
 
Ukifika Mbeya Mjini kuna eneo linaitwa Forest Mpya.

Siku za nyuma eneo hilo lilijulikana tu kama Forest kwa kuwa kulikuwa na msitu mkubwa sana wa miti ya milingoti ambayo Kama huijui ni miti inayozalisha nguzo za umeme na za TTCL...
We Bujibuji kweli ni wa Mbeya. Nami ingawaje kwetu Nyegezi Mz, lakini nimekaa mitaa hiyo.

Unafahamu hadi posolo?
 
Umenikumbusha mbali sana! Kuna jirani yetu alichanjwa, kupitia ukuta uliokuwa nyumbani kwetu.
Dawa, ilikuwa kupaka maji ya malimao. Hivyo, tulimnunulia pale REJIKO sokoni.
Nakumbuka pia, kuna jamaa watatu walikurupushwa ule mtaa aliokuwa anaishi Mzee Mwangoka (tulikuwa tunamuita MKUBWA WA TANU),kwa mayowe kuwa WACHANJAJI! Walipigwa hao watu, huku tukiwapeleka polisi. Tulipofika kwenye daraja pale mbele ya duka la Dauseni, kuelekea kwa yule mganga mfuga nyuki mzee Kibwana, mmoja akafariki, kwa kipigo. Bahati nzuri polisi walikuja, wakawaokoa wale wawili, na kuubeba ule mwili.
Nilikuwa mdogo, lakini mpaka leo ninajiona nina hatia ya yule TULIYEMUUA!

Sent using Jamii Forums mobile app
Simon Sirro liked your post.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
61 Reactions
Reply
Back
Top Bottom