Mfahamu Jaili: Chinja chinja aliyevuma Mbeya na Mama yake aliyekufa na kufufuka mara tatu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
Ukifika Mbeya Mjini kuna eneo linaitwa Forest Mpya.

Siku za nyuma eneo hilo lilijulikana tu kama Forest kwa kuwa kulikuwa na msitu mkubwa sana wa miti ya milingoti ambayo Kama huijui ni miti inayozalisha nguzo za umeme na za TTCL.

Huu msitu ndio Jaili aliutumia kuchinja watu ambao alikuwa akiwapiga kwanza na nyundo, Kisha huwapakia kwenye gari na kwenda kuwachinja Forest.

Mama yake Jaili alikuwa ni mchawi sana na alikufa na kufufuka Mara tatu kwenye uhai wake. Na alipokuja Mara ya nne haraka haraka wakaenda kumzika kwenye makaburi ya Nonde.

Mara ya kwanza alifia katika Hospital ya Rufaa Mbeya, enzi hizo ikiitwa Gredi Wani. Alipokufa wakampeleka mortuary, sasa Kuna watu walikuwa na maiti ya ndugu yao kafa kwa ajali, wakati mhudumu anavutavuta mafriji, mama yake Jaili akanyanyuka, na kutembea kwa miguu hadi kwa mwanae mitaa ya Ghana.

Mara ya pili alifia nyumbani kwa mwanae, na akapelekwa mortuary ambako alikaa, na siku walipoenda kumuandaa kwa ajili ya maziko, aliamka na kurudi kuwa hai, watu wakatoka nduki vibaya Sana.

Baada ya siku chache huyu Bibi mwenye mauzauza ambayo Mshana Jr hajawahi kuyaona maishani mwake, alifariki Tena, ila Safari hii nimesahau alifufukaje.

Sasa alipokuja kufa Mara ya nne, hawakumchelewesha, Wananzengo fasta wakakimbilia kwenye makaburi ya Nonde, wakachimba kaburi refu sana, ngazi ya zimamoto inazama, wakaandaa na trip ya mawe, jiwe la chuma sio mamoma.

Maiti fasta ikawekwa kwenye jeneza lililotengenezwa kwa mti wa Mkambokambo, ile miti ambayo zamani wakati wa Christmas ilikuwa inauzwa Namanga na Kariakoo Cyprus tree.

Fasta wakaitwa Mchungaji Mwamlima na Mwinjilisti Mwaibofu wa wa kanisa la Moravian. Mwili wa marehemu hakuingizwa kanisani kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya mwisho. Moja kwa moja ikapelekwa Nonde, Mwamimwa akaendesha ibada huko. Ibada ilikuwa fupi Sana kuokoa muda ili asifufuke Tena.

Jeneza likashushwa huko kaburini, kwa namna ya kuvurumushwa.
Lile tipper ambalo lilikuwa na trip ya mawe, likabenua mawe yote Ndani ya kaburi.
Baada ya hapo vijana wakapiga posolo /chepe za kutosha kumfukia marehemu.

Huu msiba ulisisimua sana, watu wa Ghana, Mbata, Majengo, Nonde, Mabatini na hata Mwanjelwa walifika kuona mazishi hayo ya kigagula. Huyu Mama ndiye aliyekuwa anafanya mwanawe Jaili asikamatwe, na hata akikamatwa alikuwa anatoroka jela. Jaili alikufa miaka ya 1998/99 na kuzikwa Nonde.

Jaili ameishi maisha ya uzee kwa mateso makubwa, alikuwa anashinda Uhindini kwa Wahindi akiwaomba hela, wakimnyima anatishia kutoa Siri zao.

Mtoto wake aitwaye Manyenye alikuwa tishio Sana, naye alikufa siku chache baada ya kifo Cha baba Yake.
 
Kwa hiyo mama Jaili alimezeshwa hirizi ya simba akiwa mdogo au alisindikwa na wazee ?
Alikuwa ni Mmanyafu, kabila dogo sana linalopatikana kwenye mpaka wa wilaya ya Rungwe na Ileje Kijiji Cha Ikuti.

Kijijini hapo unapita mto Songwe/Kiwira. Kijiji chote ni wachawi sana na mto huu mkubwa ukifika kijijini hapo, huwa mdogo kabisa, kiasi cha kuweza kuruka kwa miguu.

Ukiruka mto hupanuka na wewe kudumbukia Ndani na kupoteza maisha. Kitendo hicho huitwa na wenyeji ATINYELITE BUKOMU kwamba hajaruka vizuri.
 
Mbeya kwa matukio hatari sana

Mara Jombi, Jaili , wachuna ngozi ,wapiga nondo hatari sana

Nakumbuka marehemu shemu wangu Kuna siku nilikuwa kwake mitaa ya block T karibu kabisa na Uwanja wa ndege

Jamaa alikuwa dereva wa mabasi ya St Mary pale Forest

Sasa anatoka saa 11.30 kuchukua Basi awafate watoto mbalizi

Akafika mitaa ya karibu na SIDO wapiga nondo wakaanza kumkimbiza

Tuko ndani tunasikia sauti mtu anapiga kelele"fungua mlango " hapo yuko mbio

Daaah Mbeya nuksi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa ni Mmanyafu, kabila dogo Sana linalopatikana kwenye mpaka wa wilaya ya Rungwe na Ileje Kijiji Cha Ikuti.
Kijijini hapo unapita mto Songwe/Kiwira...
Mkuu hapo pa Ikuti umekosea hawa jamaa wanapatika mkondo wa chuo cha magereza ukipita pale chuo kuelekea juu ndio kijiji cha hao malamanyafu Ikuti iko nyuma ya magereza na huo mto Songwe upo mpkani mwa Tanzania na Malawi kutoka kwa hao malamanyafu ni zaidi ya km 200
 
Mbeya kwa matukio hatari sana

Mara jombi,jaili ,wachuna ngozi ,wapiga nondo hatari sana

Nakumbuka marehemu shemu wangu Kuna siku nilikuwa kwake mitaa ya block T karibu kabisa na uwanja. Wa ndege

Jamaa alikuwa dereva wa mabasi ya st Mary pale forest

Sasa anatoka saa 11.30 kuchukua Basi awafate watoto mbalizi

Akafika mitaa ya karibu na sido wapiga nondo wakaanza kumkimbiza

Tuko ndani tunasikia sauti mtu anapiga kelele"fungua mlango " hapo yuko mbio

Daaah mbeya nuksi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Walimpiga au mlimuokoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbeya kwa matukio hatari sana

Mara jombi,jaili ,wachuna ngozi ,wapiga nondo hatari sana

Nakumbuka marehemu shemu wangu Kuna siku nilikuwa kwake mitaa ya block T karibu kabisa na uwanja...
Pia miaka ya mwanzoni mwa 80 kulikuwa na wachanjaji, wakikupiga chale zao unakufa. Vitanda vyumbani vikasogezwa katikati ya chumba, kitanda kikikaa ukutani wanakupiga chale zao za kichawi.

Chale ilichanjwa kwenye mgomba na aliye Ndani anaathirika, na kufa. Mfu huenda kuwekwa ndondocha
 
Mkuu hapo pa ikuti umekosea hawa jamaa wanapatika mkondo wa chuo cha magereza ukipita pale chuo kuelekea juu ndio kijiji cha hao malamanyafu ikuti iko nyuma ya magereza na huo mto songwe upo mpkani mwa tanzania na malawi kutoka kwa hao malamanyafu ni zaidi ya km 200
Asante kwa maboresho, nakuaminia Sana Mndali wangu
 
Pia miaka ya mwanzoni mwa 80 kulikuwa na wachanjaji, wakikupiga chale zao unakufa. Vitanda vyumbani vikasogezwa katikati ya chumba, kitanda kikikaa ukutani wanakupiha chale zao za kichawi.
Chale ilichanjwa kwenye mgomba na aliye Ndani anaathirika, na kufa. Mfu huenda kuwekwa ndondocha
Duuh mbeya noma sana

Siku hizi wamestaarabika sana .

Ila nimemisi sana mitaa yangu ya Nzovwe, Itigi, Lumbila, Iyunga na Kalobe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa ni Mmanyafu, kabila dogo Sana linalopatikana kwenye mpaka wa wilaya ya Rungwe na Ileje Kijiji Cha Ikuti.
Kijijini hapo unapita mto Songwe/Kiwira.
Kijiji chote ni wachawi Sana na mto huu mkubwa ukitika kijijini hapo, huwa mdogo kabisa, kiasi Cha kuweza kuruka kwa miguu. Ukiruka mto hupanuka na wewe kudumbukia Ndani na kupoteza maisha. Kitendo hicho huitwa na wenyeji ATINYELITE BUKOMU kwamba hajaruka vizuri.
Pia nishawahi sikia maajabu ya mto Kiwira

Nasikia Kuna ushirikana mwingi sana

Mimi huwa siielewi why watu wa Kyela wanatumia maji ya visima yenye chumvi ilihali mto Kiwira una maji mengi umepita wilayani kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia miaka ya mwanzoni mwa 80 kulikuwa na wachanjaji, wakikupiga chale zao unakufa. Vitanda vyumbani vikasogezwa katikati ya chumba, kitanda kikikaa ukutani wanakupiha chale zao za kichawi.
Chale ilichanjwa kwenye mgomba na aliye Ndani anaathirika, na kufa. Mfu huenda kuwekwa ndondocha
Aaah Niko Mbeya na utoto wangu miaka hiyo. Ole wako mtu akupigie kelele za mchanjaji! Watu watu watatoka kila kona na kila silaha, ya haraka mawe, ni kifo mara moja!
 
Pia miaka ya mwanzoni mwa 80 kulikuwa na wachanjaji, wakikupiga chale zao unakufa. Vitanda vyumbani vikasogezwa katikati ya chumba, kitanda kikikaa ukutani wanakupiha chale zao za kichawi.

Chale ilichanjwa kwenye mgomba na aliye Ndani anaathirika, na kufa. Mfu huenda kuwekwa ndondocha
Umenikumbusha mbali sana! Kuna jirani yetu alichanjwa, kupitia ukuta uliokuwa nyumbani kwetu.

Dawa, ilikuwa kupaka maji ya malimao. Hivyo, tulimnunulia pale REJIKO sokoni.

Nakumbuka pia, kuna jamaa watatu walikurupushwa ule mtaa aliokuwa anaishi Mzee Mwangoka (tulikuwa tunamuita MKUBWA WA TANU),kwa mayowe kuwa WACHANJAJI! Walipigwa hao watu, huku tukiwapeleka polisi.

Tulipofika kwenye daraja pale mbele ya duka la Dauseni, kuelekea kwa yule mganga mfuga nyuki mzee Kibwana, mmoja akafariki, kwa kipigo. Bahati nzuri polisi walikuja, wakawaokoa wale wawili, na kuubeba ule mwili.

Nilikuwa mdogo, lakini mpaka leo ninajiona nina hatia ya yule TULIYEMUUA!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom