Mfahamu Jaili: Chinja chinja aliyevuma Mbeya na Mama yake aliyekufa na kufufuka mara tatu

Comrade 01

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
535
500
H
Alikuwa ni Mmanyafu, kabila dogo sana linalopatikana kwenye mpaka wa wilaya ya Rungwe na Ileje Kijiji Cha Ikuti.

Kijijini hapo unapita mto Songwe/Kiwira. Kijiji chote ni wachawi sana na mto huu mkubwa ukifika kijijini hapo, huwa mdogo kabisa, kiasi cha kuweza kuruka kwa miguu.

Ukiruka mto hupanuka na wewe kudumbukia Ndani na kupoteza maisha. Kitendo hicho huitwa na wenyeji ATINYELITE BUKOMU kwamba hajaruka vizuri.
Zilikuwa Imani tu,huu mto kuna sehemu nime uruka Sana.Karibu na chuo cha magereza kule.Tulikuwa tunaenda kufanya mazoezi.Ni kama wanavyosema kwenye bwawa la "kisiba" kule Tukuyu njia ya kwenda Lwanga.
 
Comrade 01

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
535
500
Kuna mzee mmoja naye alikuwa anaitwa Mwanjisi alifanya biashara ya Hiace, sifa ya gari ya ni ilikuwa imechoka sana naye alikuwa na stori za mauza uza. Hivi bado yu hai?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha Mwanjisi hakuwa mchawi bali mbabe alikuwa anafunga "kilemba".Kuna route moja aliianzisha, Airport - Sokomatola,basi akikuona unapeleka hiace njia hiyo,ujue ni vita.Na gari yake ikikamatwa tu,alikuwa anabeba familia yake anaipeleka central police waihudumie wao polisi.
 
Capital G

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
831
1,000
Mkuu iko wapi hii dawa me nkachume aisee, nina ndoto nyingi sana kabla sijafa
Bujibuji mwaka 2001 kuna ajali ilitokea Mbeya wakafa watu wote halafu baada ya ajali mtu mmoja akawa anaokota ubongo wa hao Marehemu anatia kwenye mfuko.. inasemekana wakati anafanya hayo alikuwa haonekani na macho ya nyama ..

sasa basi kumbe wakati anafanya hivyo Kuna " mjanja" mmoja alimuona akamzindua na kisha kuwasanua raia.

Then after that Jamaa alishambuliwa na kufa papo hapo. Tukio hili Lili ripotiwa na gazeti la uwazi..

Unafahamu kuhusu tukio Hilo chief? What really happened?

Na Kingine interval ya huyo Bibi kufa na kufufuka ilikuwa muda gani?

Atakuwa alikula.madawa yanaitwa Lufakale au alikuwa ana pass her death to other people au Wachawi wenzake walikuwa wanamlisha dawa moja ya porini inafufua.

Hiyo dawa nyoka akiwa anapigana na nyoka mwenzie halafu akafa, nyoka Huyo huenda kuchuma dawa hiyo kwa mdomo kisha anamtemea mdomoni nyoka aliekufa anafufuka..

NI hatari Sana hiyo dawa inafufua mtu without a doubt .

Sharti lake lazima ichumwe kwa mdomo pia.

And nyoka akiwa anachuma dawa hiyo halafu akakuona he kills you labda uwe na ulinzi wa Mungu au uwe na madawa ya kuzuia nyoka.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
1,434
2,000
Mwishoni mwa miaka ya sabini niliwahi kusikia kisa cha jamaa huyu...ukisikia mtu analia " nakufaaaa" kwenye msitu ule usikimbilie. Ndivyo tuliambiwa chinjachinja alikuwa anafanya vitu vyake...
Hakika mzee Mwanakijiji umekula sana chumvi. Nimeona nyuzi zako back in 2006. Hebu tupe uhondo zaidi.
 
okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
1,262
2,000
HAH HAH HAH HAH

NZOVWE HOME.

Ila mkuu usiwatishe sana watu ikuti ni sehemu salama kwa sasa.

Japo kuna vitukuu vinakuna kuna watu..

ila ni salama ebu nikaribishie na wengine.Alikuwa ni Mmanyafu, kabila dogo sana linalopatikana kwenye mpaka wa wilaya ya Rungwe na Ileje Kijiji Cha Ikuti.

Kijijini hapo unapita mto Songwe/Kiwira. Kijiji chote ni wachawi sana na mto huu mkubwa ukifika kijijini hapo, huwa mdogo kabisa, kiasi cha kuweza kuruka kwa miguu.

Ukiruka mto hupanuka na wewe kudumbukia Ndani na kupoteza maisha. Kitendo hicho huitwa na wenyeji ATINYELITE BUKOMU kwamba hajaruka vizuri.
 
okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
1,262
2,000
Mkuu JOMBI shikamoo braza uliacha uwizi wako wa magari.?!

Daaah Lumbila.

Mkuu umenikumbusha hiyo mitaa back then wakati nasoma Iyunga ndo tulikuwa tunaenda kufata mademu hiyo mitaa .Pamoja nakule juu Ikuti.
 
BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,015
2,000
Bujibuji mwaka 2001 kuna ajali ilitokea Mbeya wakafa watu wote halafu baada ya ajali mtu mmoja akawa anaokota ubongo wa hao Marehemu anatia kwenye mfuko.. inasemekana wakati anafanya hayo alikuwa haonekani na macho ya nyama ..

sasa basi kumbe wakati anafanya hivyo Kuna " mjanja" mmoja alimuona akamzindua na kisha kuwasanua raia.

Then after that Jamaa alishambuliwa na kufa papo hapo. Tukio hili Lili ripotiwa na gazeti la uwazi..

Unafahamu kuhusu tukio Hilo chief? What really happened?

Na Kingine interval ya huyo Bibi kufa na kufufuka ilikuwa muda gani?

Atakuwa alikula.madawa yanaitwa Lufakale au alikuwa ana pass her death to other people au Wachawi wenzake walikuwa wanamlisha dawa moja ya porini inafufua.

Hiyo dawa nyoka akiwa anapigana na nyoka mwenzie halafu akafa, nyoka Huyo huenda kuchuma dawa hiyo kwa mdomo kisha anamtemea mdomoni nyoka aliekufa anafufuka..

NI hatari Sana hiyo dawa inafufua mtu without a doubt .

Sharti lake lazima ichumwe kwa mdomo pia.

And nyoka akiwa anachuma dawa hiyo halafu akakuona he kills you labda uwe na ulinzi wa Mungu au uwe na madawa ya kuzuia nyoka.
naitafuta hio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brilucy

Member
May 23, 2020
7
45
Ukifika Mbeya Mjini kuna eneo linaitwa Forest Mpya.

Siku za nyuma eneo hilo lilijulikana tu kama Forest kwa kuwa kulikuwa na msitu mkubwa sana wa miti ya milingoti ambayo Kama huijui ni miti inayozalisha nguzo za umeme na za TTCL.

Huu msitu ndio Jaili aliutumia kuchinja watu ambao alikuwa akiwapiga kwanza na nyundo, Kisha huwapakia kwenye gari na kwenda kuwachinja Forest.

Mama yake Jaili alikuwa ni mchawi sana na alikufa na kufufuka Mara tatu kwenye uhai wake. Na alipokuja Mara ya nne haraka haraka wakaenda kumzika kwenye makaburi ya Nonde.

Mara ya kwanza alifia katika Hospital ya Rufaa Mbeya, enzi hizo ikiitwa Gredi Wani. Alipokufa wakampeleka mortuary, sasa Kuna watu walikuwa na maiti ya ndugu yao kafa kwa ajali, wakati mhudumu anavutavuta mafriji, mama yake Jaili akanyanyuka, na kutembea kwa miguu hadi kwa mwanae mitaa ya Ghana.

Mara ya pili alifia nyumbani kwa mwanae, na akapelekwa mortuary ambako alikaa, na siku walipoenda kumuandaa kwa ajili ya maziko, aliamka na kurudi kuwa hai, watu wakatoka nduki vibaya Sana.

Baada ya siku chache huyu Bibi mwenye mauzauza ambayo USER=98741]Mshana Jr[/USER] hajawahi kuyaona maishani mwake, alifariki Tena, ila Safari hii nimesahau alifufukaje.

Sasa alipokuja kufa Mara ya nne, hawakumchelewesha, Wananzengo fasta wakakimbilia kwenye makaburi ya Nonde, wakachimba kaburi refu sana, ngazi ya zimamoto inazama, wakaandaa na trip ya mawe, jiwe la chuma sio mamoma.

Maiti fasta ikawekwa kwenye jeneza lililotengenezwa kwa mti wa Mkambokambo, ile miti ambayo zamani wakati wa Christmas ilikuwa inauzwa Namanga na Kariakoo Cyprus tree.

Fasta wakaitwa Mchungaji Mwamlima na Mwinjilisti Mwaibofu wa wa kanisa la Moravian. Mwili wa marehemu hakuingizwa kanisani kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya mwisho. Moja kwa moja ikapelekwa Nonde, Mwamimwa akaendesha ibada huko. Ibada ilikuwa fupi Sana kuokoa muda ili asifufuke Tena.

Jeneza likashushwa huko kaburini, kwa namna ya kuvurumushwa.
Lile tipper ambalo lilikuwa na trip ya mawe, likabenua mawe yote Ndani ya kaburi.
Baada ya hapo vijana wakapiga posolo /chepe za kutosha kumfukia marehemu.

Huu msiba ulisisimua sana, watu wa Ghana, Mbata, Majengo, Nonde, Mabatini na hata Mwanjelwa walifika kuona mazishi hayo ya kigagula. Huyu Mama ndiye aliyekuwa anafanya mwanawe Jaili asikamatwe, na hata akikamatwa alikuwa anatoroka jela. Jaili alikufa miaka ya 1998/99 na kuzikwa Nonde.

Jaili ameishi maisha ya uzee kwa mateso makubwa, alikuwa anashinda Uhindini kwa Wahindi akiwaomba hela, wakimnyima anatishia kutoa Siri zao.

Mtoto wake aitwaye Manyenye alikuwa tishio Sana, naye alikufa siku chache baada ya kifo Cha baba Yake.
Walimkosa kosa aisee ilibaki kidogo wamtoboe na nondo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom