Mfahamu Jaili: Chinja chinja aliyevuma Mbeya na Mama yake aliyekufa na kufufuka mara tatu

Zambotti

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,558
2,000
Alikuwa ni Mmanyafu, kabila dogo Sana linalopatikana kwenye mpaka wa wilaya ya Rungwe na Ileje Kijiji Cha Ikuti.

Kijijini hapo unapita mto Songwe/Kiwira...
Nimewahi kufika hiki kijiji, kuna stori za mauza uza sana hapo.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
48,950
2,000
Umenikumbusha mbali sana! Kuna jirani yetu alichanjwa, kupitia ukuta uliokuwa nyumbani kwetu.
Dawa, ilikuwa kupaka maji ya malimao. Hivyo, tulimnunulia pale REJIKO sokoni.
Nakumbuka pia, kuna jamaa watatu walikurupushwa ule mtaa aliokuwa anaishi Mzee Mwangoka (tulikuwa tunamuita MKUBWA WA TANU),kwa mayowe kuwa WACHANJAJI!..
Unamkumbuka Mzee Miraji wa Joka Road? Alikuwa na nyumba yake mtaa huo, nyumba ilikiwa na mahindi yamelimwa na yametoa mbelewele, Sasa kukawa na jamaa wanachunga ng'ombe,

wakaingiza mifugo kwenye hicho kibustani cha mbele ya nyumba, wale wanyama wakapigwa upofu, na wale vijana wachungaji wakahangaika siku nne kwenye hicho kibustani wanatafuta njia ya kutokea wasiione.
 

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
7,785
2,000
Bujibuji mwaka 2001 kuna ajali ilitokea Mbeya wakafa watu wote halafu baada ya ajali mtu mmoja akawa anaokota ubongo wa hao Marehemu anatia kwenye mfuko.. inasemekana wakati anafanya hayo alikuwa haonekani na macho ya nyama ..

sasa basi kumbe wakati anafanya hivyo Kuna " mjanja" mmoja alimuona akamzindua na kisha kuwasanua raia.

Then after that Jamaa alishambuliwa na kufa papo hapo. Tukio hili Lili ripotiwa na gazeti la uwazi..

Unafahamu kuhusu tukio Hilo chief? What really happened?

Na Kingine interval ya huyo Bibi kufa na kufufuka ilikuwa muda gani?

Atakuwa alikula.madawa yanaitwa Lufakale au alikuwa ana pass her death to other people au Wachawi wenzake walikuwa wanamlisha dawa moja ya porini inafufua.

Hiyo dawa nyoka akiwa anapigana na nyoka mwenzie halafu akafa, nyoka Huyo huenda kuchuma dawa hiyo kwa mdomo kisha anamtemea mdomoni nyoka aliekufa anafufuka..

NI hatari Sana hiyo dawa inafufua mtu without a doubt .

Sharti lake lazima ichumwe kwa mdomo pia.

And nyoka akiwa anachuma dawa hiyo halafu akakuona he kills you labda uwe na ulinzi wa Mungu au uwe na madawa ya kuzuia nyoka.
 
Top Bottom