Mfahamu Hussein Shekilango, aliyepewa jina la barabara jijini Dar (kuanzia Bamaga - Urafiki)

UNAIJUA BARABARA YA SHEKILANGO?

HUYU NDIYE SHEKILANGO MWENYEWE...

Na: Comred Mbwana Allyamtu

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA

Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe. Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

Katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa, Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi, huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa. Majonzi zaidi yakiwa kwa Wanakorogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

RIP SHEKILANGO...

Ndimi.
Comred Mbwana Allyamtu.
 
image.jpeg

JE WAJUA?

HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA

Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe. Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa, Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi, huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa. Majonzi zaidi yakiwa kwa Wanakorogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Mola amlaze Pema Shujaa Hussein Ramadhani Shekilango

Pichani ni Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, Picha ni kwa Hisani ya Familia ya Shekilango, Ukurasa wa Watanzania Mashuhuri unatoa shukrani za dhati kwa Bi Ikupa Shekilango kwa Msaa wake kwa Ukurasa.
 
Mbona Shekilango sijamsoma katika hekaya za Mohamed Said ?
Yamakagashi,
Kuwa mimi naandika hekaya labda ni hasad na chuki ndiyo zinazokusukuma
kusema hivyo.

Ushahidi wangu ni huo hapo chini:
  1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006 The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press 2006, Nairobi. (Children’s book).
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  6. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  7. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  8. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  9. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  10. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  11. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  12. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  13. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  14. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  15. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  16. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  17. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press 2006, Nairobi. (Children’s book).
  18. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  19. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  20. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  21. Awards: Several Awards.
  22. Visiting Scholar: (2011)
  23. University of Iowa, Iowa City, USA
  24. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  25. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  26. OTHER COUNTRIES VISITED
  27. Zambia, Ethiopia, Swaziland, Saudi Arabia, Msumbiji, Zimbabwe, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, Turkey and Abu Dhabi.
 
Mimi sina chuki na Mohamed Said ,nimeziita hekaya kwa namna ambavyo mimi nime digest makala zako hivyo kosa langu sijui ni lipi

Kila mtu ana mtazamo wake wa namna ya kuchukulia jambo ,mimi nimeona ni hekaya ,pengine wengine watakuabudu kwa hilo

Nakukuona ni mungu au Mkombozi

Ndio binadamu tulivyo

Shekilango mbona hujapata kutueleza machache kuhusu yeye?
 
Mimi sina chuki na Mohamed Said ,nimeziita hekaya kwa namna ambavyo mimi nime digest makala zako hivyo kosa langu sijui ni lipi
Kila mtu ana mtazamo wake wa namna ya kuchukulia jambo ,mimi nimeona ni hekaya ,pengine wengine watakuabudu kwa hilo
Nakukuona ni mungu au Mkombozi
Ndio binadamu tulivyo
Shekilango mbona hujapata kutueleza machache kuhusu yeye ?

Yamakagashi,
Ingekuwa wewe unahitaji kujua kwa nini sijaandika lolote kuhusu Hussein
Shekilango
ungeniuliza lakini wewe umeaanza kwa kejeli na dharau juu
yangu.

Hapo ukawa tayari ushanivunjia heshima.

Mimi nikakuwekea baadhi ya kazi zangu katika uandishi na vyuo ambavyo
nimealiikwa kwa minajili ya historia ya Afrika.

Nimekuwekea hayo yote ili niirejeshe akili yako katika hali ya kawaida ikae
mbali na mambo ya kipuuzi kwani haiyumkiniki nikawa nimehadhiri kote huko
pamoja na Northewestern University ambao ndiyo wanaongoza dunia kwa
historia ya Afrika ikawa pale mie nimealikwa kwa ajili ya ''hekaya.''

Najua ulipigwa na mshtuko na ndiyo ukawa kimya unawaza nini ufanye.
Angalau ungerudi na heshima zako.

Umerudi na upuuzi haba jana kushinda ule wa mwanzo.
Kaa ukijua kuwa huwezi kujitoa kimasomaso kwa kuongeza upuuzi juu ya upuuzi.

Sasa nakurudisha katika darsa.

Katika uandishi kuna kitu kinaitwa, ''demarcation,'' ikiwa unasoma Kiingereza ingia
hata ''Google,'' utapata maana yake.

Mimi nimetafiti na kuandika historia ya TANU na harakati za uhuru wa Tanganyika.
Hii ndiyo ilikuwa mipaka yangu.

Sasa hebu rejea katika maisha ya Hussein Shekilango uangalie wapi ningeweza
kumpachika.

Sikulazimishi kuwa msomi kwani usomi unajengwa na uwezo wa ubongo wa mtu.

Ila nitakuomba ujitahidi uwe na adabu na ujifunze namna nzuri ya kufanya mjadala
hadharani.

Hapa tunasomwa na dunia nzima na haipendezi ukatokeza kuwa wewe ni mpuuzi,
usiye na adabu na hujui kitu.

Ninakuwekea picha yangu nikiwa Library of Congress, Washington.
Ukiwa huijui hiyo ni nini ingia tena, ''Google.''

Katika maktaba hii kumehifadhiwa mengi niliyoandika na hawa si watu wa ''hekaya.''

_Ps4wU1f63h3FL6jIskOVelzyOmKvjtFFgE84ktDY4pFpijYdu6yl2Hlq95vaiziHWceDW9sCjUvjuwuAtpP5uBmguro9JiwNgiwCPwRhixtVTvPdub9zfafDfZheGkKrfyEKAwtIVS00-cAn6ynJoRfyGyGCgCIjm8Q7GG3lVhCZQXkqGRbyuB5hnMGuzxgPnLSCSTaRxZ5bGrmFA-smR2PevyfZ78CBrcx0gM87LD2-xeFv6mTY4wRfG6MWut_kEzC4BrbkMBMZRjdwIfDFCZlZf1-xRZnjqCWH0L3QxITpKTQVPqhFtly235lQO5cjkefwgvvAYdlyRiYvLxMWznuvSYPgXOZnGGkTKJofUy3oB1FJtxvzYge2xxgLK5hy4ZV1zgwsUTy2xypUc7_ejRH7I04JHrm-hJdeLeBUtpdh-MDwZ9PWeBsB1dXEtBkQRy6YpGRtmR3kvzklGMzWADuo-F-5lVFeWbG5qQY4CheQ9ueCvU735RmhgcpBbg-fNpcTO7uBR-A_2vALZTgT-U1t4-5Qk7CaPxGbSV_RgLy69ThfaE528gKVWFEojgcxCcYIcSgS6iTe-x-A-9hqHLZ4219YkjYccGGGCAH6K-pMIzxYSHO=w971-h650-no
 
Haaa haaa huyu hawezi kumtia katika hekay zake kwakuwa si mzee wake wa Kariakoo.Halafu ukimweka katika hekaya zake hakika kutafifisha histohisia zake kabisa.
historia

Ngongo,
Tunaweza tukaanza mjadala wetu hapa mimi naweka historia
ya watu wa Kariakoo na wewe weka ya kwenu ulikotoka:

Naam, na ndiyo maana tunapeana darsa.

Kwa hakika uongo ukisemwa sana mwishowe huwaingia watu na kuuona ni ukweli na hata anafundishwa ukweli bado haumuingii akilini.

Kuna watu chungu nzima humu wakiambiwa TANU haikuasisiwa na Nyerere na hata jina la TANU hajalitowa yeye, basi hiyo kabisa haiwaingii akilini kwa kuwa tu wameshajazwa ujinga.

Nyerere alikuwepo wakati TANU inaundwa 1954 lakini hakuwa muasisi wala hakuwa mtoa wazo, wazo lilikuwepo kabla hajajiunga na waasisi wa kupigania Uhuru wa Tanganyika waliokuwepo Dar.

Of course Nyerere alikuwa msomi wa kutokea Ulaya na alikuwa ni nguzo kubwa alipojiunga na wapigania Uhuru wa Dar lakini hakuwa muasisi.

Hilo ni ngumu sana watu kulikubali, kwanini?

Maalim Faiza,
Umeeleza vyema sana hali ya watu kuukubali ukweli baada ya kulishwa
uongo kwa muda mrefu.

Kuna barua ya Kleist Sykes anajibu barua ya Mzee bin Sudi mwaka wa
1933, Kleist akitabiri kuwa kazi hii ya African Association walioianza wao
itakujwa kumalizwa na watakaokuja baada yao.

Hebu tustaladhi na kipande hiki hapo chini:

Abdulwahid sasa akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa amekamilisha lile
lengo lake kubwa katika maisha yake, lengo ambalo lilianza kwa marehemu
baba yake ambaye miaka 21 iliyopita alitabiri kuendelea kwa mapambano
kati ya Waafrika wa Tanganyika na serikali ya kikoloni.

Kleist Sykes alikuwa halikadhalika ametabiri jukumu la kizazi kijacho. Katika
barua aliyomwandikia Mzee bin Sudi, rais wa African Association, mwaka
wa 1933, Kleist katika umri mdogo wa miaka 29, akiwa kijana mdogo sana
aliandika maneno haya:

‘’Tupambane kwa nguvu zetu zote kuelekea njia ya ustaarabu kama vile watu
wa makabila mengine wanavyofanya.

Haidhuru kitu ikiwa hatukamilishi kila kitu.

Wale watakaokuja baada yetu watakamilisha yatakayobakia.’’

Kwa hakika Kleist alikuwa mtu wa fikra.

Alizungumzia kuhusu ''ustaarabu,'' ambao hivi leo ungemaanisha ''kujitawala,''
na kuhusu, ''makabila,'' ambayo TANU imeyageuza kuwa ''taifa.''

Katika mwaka wa 1954 robo karne baadaye katika jengo lilo hilo, 25 New Street
ambalo Kleist alisaidia kulijenga kwa njia ya kujitolea, kizazi kipya nchini
Tanganyika kilikuwa kikiigeuza African Association aliyoiunda katika mwaka 1929
kuwa chama cha siasa.

DSCN1154.JPG

Lengo lake lilikuwa kuwatayarisha Watanganyika kujitawala.

Miongoni mwa waliokuwa wakiongoza harakati za kudai uhuru zilizokuwa zikiibuka
walikuwa watoto wake watatu, Abdulwahid, Ally na Abbas.

-8tehr0qBv0b_wnTNDACSkxzxk9wvrwI_0amhzzjPVNLtc48_KLfeIhWgL2Oufq09DzK0DO20GRAqL5KAmzkC_sQcKM45nY8IKrUAWLPQM1WWjVvgIRA5rcsFg_O3HqusPklgdXoGxCvi-Bvhd3bp9EhGhybIuJRnS0pwdPV5rKKHymJiM-lf-Zy3OK5h8gxd8YAfGZP_wpmiqv1i-5D-mzQn5ElNrKc3y_6eiw1_QtS66QGo_sFaqQsR6S09xf1f1i0BOTExtHUEkJIznQ7yCZtNDLEL4SJa1mFbpezHDr_t8IT_7-awc5TBDK06cqfTUmjU2l2n4ZdLxnrGV_JB6myr9A7PuV6UKN3clp_Jgo8tmZDVurulrhDmykObqbL5N_86oekEGSUfPUYG3dvYA5kYiPQ2JWgdBOVw2lHBTIZ-ZYwLwvs2JgqubCRxohr823CudC3D35Yyumpcxn1CSpP5XeoVzTVZdnK9suhErtbCqJRy7LwnSjMGwbCo0IStqogQMGqmL33zpfXm0WpUGIscZvlIYSg9Jb-c8aOMZAyEYSBRiqlcxFFIWQYtfWESsW8ywlALAyUk9efwTv75hCxYBdzNrvWn3Y1ph8xRPRaxzI4nooK4Q=w352-h480-no
Kushoto: Kleist Sykes, Abbas nyumna ni Ally na Abdul
picha hii ilipigwa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam
kutoka Kabete Kenya alipokuwa akifanya mafunzo ya kijeshi
katika KAR kabla hajaondoka kwenda Burma katika Vita Vya
Pili Vya Dunia.

DSCN1138.JPG
Kutoka Dictionary of African Biography, Oxford University Press, New York 2011

Hii ndiyo historia ya TANU.
 
Yamakagashi,
Ingekuwa wewe unahitaji kujua kwa nini sijaandika lolote kuhusu Hussein
Shekilango
ungeniuliza lakini wewe umeaanza kwa kejeli na dharau juu
yangu.

Hapo ukawa tayari ushanivunjia heshima.

Mimi nikakuwekea baadhi ya kazi zangu katika uandishi na vyuo ambavyo
nimealiikwa kwa minajili ya historia ya Afrika.

Nimekuwekea hayo yote ili niirejeshe akili yako katika hali ya kawaida ikae
mbali na mambo ya kipuuzi kwani haiyumkiniki nikawa nimehadhiri kote huko
pamoja na Northewestern University ambao ndiyo wanaongoza dunia kwa
historia ya Afrika ikawa pale mie nimealikwa kwa ajili ya ''hekaya.''

Najua ulipigwa na mshtuko na ndiyo ukawa kimya unawaza nini ufanye.
Angalau ungerudi na heshima zako.

Umerudi na upuuzi haba jana kushinda ule wa mwanzo.
Kaa ukijua kuwa huwezi kujitoa kimasomaso kwa kuongeza upuuzi juu ya upuuzi.

Sasa nakurudisha katika darsa.

Katika uandishi kuna kitu kinaitwa, ''demarcation,'' ikiwa unasoma Kiingereza ingia
hata ''Google,'' utapata maana yake.

Mimi nimetafiti na kuandika historia ya TANU na harakati za uhuru wa Tanganyika.
Hii ndiyo ilikuwa mipaka yangu.

Sasa hebu rejea katika maisha ya Hussein Shekilango uangalie wapi ningeweza
kumpachika.

Sikulazimishi kuwa msomi kwani usomi unajengwa na uwezo wa ubongo wa mtu.

Ila nitakuomba ujitahidi uwe na adabu na ujifunze namna nzuri ya kufanya mjadala
hadharani.

Hapa tunasomwa na dunia nzima na haipendezi ukatokeza kuwa wewe ni mpuuzi,
usiye na adabu na hujui kitu.

Ninakuwekea picha yangu nikiwa Library of Congress, Washington.
Ukiwa huijui hiyo ni nini ingia tena, ''Google.''

Katika maktaba hii kumehifadhiwa mengi niliyoandika na hawa si watu wa ''hekaya.''

_Ps4wU1f63h3FL6jIskOVelzyOmKvjtFFgE84ktDY4pFpijYdu6yl2Hlq95vaiziHWceDW9sCjUvjuwuAtpP5uBmguro9JiwNgiwCPwRhixtVTvPdub9zfafDfZheGkKrfyEKAwtIVS00-cAn6ynJoRfyGyGCgCIjm8Q7GG3lVhCZQXkqGRbyuB5hnMGuzxgPnLSCSTaRxZ5bGrmFA-smR2PevyfZ78CBrcx0gM87LD2-xeFv6mTY4wRfG6MWut_kEzC4BrbkMBMZRjdwIfDFCZlZf1-xRZnjqCWH0L3QxITpKTQVPqhFtly235lQO5cjkefwgvvAYdlyRiYvLxMWznuvSYPgXOZnGGkTKJofUy3oB1FJtxvzYge2xxgLK5hy4ZV1zgwsUTy2xypUc7_ejRH7I04JHrm-hJdeLeBUtpdh-MDwZ9PWeBsB1dXEtBkQRy6YpGRtmR3kvzklGMzWADuo-F-5lVFeWbG5qQY4CheQ9ueCvU735RmhgcpBbg-fNpcTO7uBR-A_2vALZTgT-U1t4-5Qk7CaPxGbSV_RgLy69ThfaE528gKVWFEojgcxCcYIcSgS6iTe-x-A-9hqHLZ4219YkjYccGGGCAH6K-pMIzxYSHO=w971-h650-no
Hivi mzee mbona unapendaga kukimbilia kwenye mwamvuli wa kuvunjiwa heshima ? Nimekuvunjia heshima wapi ? Mimi mpaka nakufa huwezi kubadili mtazamo wangu juu ya makala zako kwamba ni Hekaya

Ipo hivyo mzee kwangu nyeusi ni nyeusi sio zaidi ya hapo.

Nikaenda mbali kusema mimi nachukulia ni Hekaya na pengine kuna wenye mtazamo tofauti wanakuona mungu na mkombozi sina tatizo na hilo, hivyo ndivyo tulivyo binadamu.

Nilishakuuliza swali moja ni wapi kwenye hizi hekaya zako uliwahi kuongelea kwanini wakiristo hawawi marais wa Zanzibar hukunijibu ,ukaishia kusema sijui umevunjiwa heshima ,unajua heshima iliyovunjwa mzee?

Hivyo sitashangaa usiposema kwanini Shekilango hukumuweka kwenye hekaya zako

Halafu unaniita mpuuzi huku wewe unalalamika kuvunjiwa heshima haya si maajabu ?

Ningeita hekaya zako upuuzi si ndio ungenitumia grenade kabisa ?
 
Hivi mzee mbona unapendaga kukimbilia kwenye mwamvuli wa kuvunjiwa heshima ? Nimekuvunjia heshima wapi ? Mimi mpaka nakufa huwezi kubadili mtazamo wangu juu ya makala zako kwamba ni Hekaya
Ipo hivyo mzee kwangu nyeusi ni nyeusi sio zaidi ya hapo
Nikaenda mbali kusema mimi nachukulia ni Hekaya na pengine kuna wenye mtazamo tofauti wanakuona mungu na mkombozi sina tatizo na hilo ,hivyo ndivyo tulivyo binadamu

Nilishakuuliza swali moja ni wapi kwenye hizi hekaya zako uliwahi kuongelea kwanini wakiristo hawawi marais wa Zanzibar hukunijibu ,ukaishia kusema sijui umevunjiwa heshima ,unajua heshima iliyovunjwa mzee ?

Hivyo sitashangaa usiposema kwanini Shekilango hukumuweka kwenye hekaya zako

Halafu unaniita mpuuzi huku wewe unalalamika kuvunjiwa heshima haya si maajabu ?

Ningeita hekaya zako upuuzi si ndio ungenitumia grenade kabisa ?

Yamakagashi,
Yawezekana katika malezi yako hukufunzwa adabu kwa hiyo unadhani unaweza
kusema lolote na chochote hadharani kwa namna yoyote.

Inawezekana pia uwezo wako wa akili ni hafifu kiasi hujui tofauti ya kitabu cha Aesop
na kazi ya kisomi inayochapwa katika jarida la kisomi ikawa haya yote kwako ni sawa
kama unavyosema kuwa ni ''hekaya.''

Inawezekana nikakueleza kuwa majarida makubwa kama Cambridge Journal of African
History wamechapa mapitio ya kitabu changu yalioandikwa na wanahistoria mashuhuru
duniani kama John Iliffe, James Brennan na Jonathon Glassman ikawe wewe hulijui hilo
jarida wala huwajui hao wanahistoria.

Inawezekana dunia yako imezungukwa na ujinga.

Sasa tuje katika swali la kwa nini Mkristo hawi rais Zanzibar.
Unataka mimi nikujibu swali hilo.

Hakika swali hilo nimeliona na nililipuuza kwa kuwa si kawaida yangu kujibu maswali
ya vichekesho.

Lakini ili kuistua akili yako nami nitakuuliza swali unazijua takwimu za Zanzibar katika
mgawanyo wa watu na imani zao?

Unaijua historia ya Zanzibar?
Fanya utafiti jibu lako utalipata hapo.

Nimekuita mpuuzi kwa kuwa hakika wewe ni zaidi ya mpuuzi.

Hujui kitu lakini unajiaminisha kuwa unaweza kusimama na mimi katika historia ya
Tanganyika.

Mjinga tu ndiye asiweza kujipima na kujua uwezo wake.

Nakuwekea picha niliyopiga miaka 30 iliyopita nikifanya kipindi cha historia BBC
Glasgow Uskochi.

wQLwvqHnAkZvlnFj5VIOHASVbHZPbckL4k89SWZHgfVXtTAFoyCZVTTkwHvTJaTfelIsUiW5q9mlTqXotAJQ1kssRpMOgvRWl-LlATHM0e11iTzMKwTKR8PCM_NW1CtbNNi2Dr6AhqCu4y1C5fA0YXWNqSGWfx17MoXfJaeQ-yclQTHjXSgR-YFJMJH9GGxEgi5gABHV6omlPr12leVkc7IIBZHlBXLALyUf9ueedz6VcHYYsnswPgN2tBn8Vuxt1qyZpuLoZIgYOn7sn1_J8jCxHopecM7Ox4COiRxnvgmz8xUNPztaqfdjIsyX5Kd_dU3hmgILoJMWI0rJ_BGNX8ZhwQgmBb6P3ThKs-oIbwu5OlM01WCaR3YA0zvvclOSZ5NJDoXsTyw18y6X4kWyKWHkpP0WktfW1GBEDYm7rsRwJYA9fHg1F8iuBOQXLlBgVJh5ZcN9m9fH7DQc63llz_wxap2YLj-N-ZiSqu7Gq8qrY-gWLrwNWQbSpnjR4JRQVN5hpbFx_zj_ko4zqoXObGYqgdeEF7Q5RmCTdci1cNhhyzboJzAql79kXyHT60mSOtyxgRtQW9_OEYGgojBnP5BIFP3bljvvN7KcVZLtTgihs57UD5xjtF0-KLHC-lry_H29oRT-yCnCyZGzkkiVGSuAOne4a0Zo88B0PuW9CoY=w960-h692-no

Yamakagashi,
Hapo juu ndiko nilikotoka mimi na ni wakati huo nikiwa kijana mdogo nikiandika na magazeti mashuhuri Afrika kama New African, Africa Events na Africa Analysis.

Kuwa na adabu kidogo.
 
Hapo juu ndiko nilikotoka mimi na ni wakati nikiindika na magazeti mashuhuri
Afrika kama New African, Africa Events na Africa Analysis.

Kuwa na adabu kidogo.

Huku tunapoenda naona unanilazimisha kukukosea heshima

Kwa sababu iam brave enough sitofanya hivyo

Endelea na hekaya zako

Mimi nipo namsoma Shakespeare hapa ,Hekaya zako nasoma nikiwa sina cha kufanya kupoteza muda hivyo kuniwekea picha zako hazisaidii unapoteza nguvu bure

Umekosewa wapi heshima ? Hebu jiheshimu ,wazazi wangu hujui walipo wewe na hujui walivyo nilea ,kama unataka tuende personal iam good at that too

Eleza kwanini kwenye hekaya zako hujawahi kuongelea Zanzibar kutokuwa na rais Mkristo

Huwezi kujibu kwanini Zanzibar hakuna Rais mkristo ila kila siku uko na Nyerere na Uislamu ,oh uhuru ,oh bibi Titi alikuwa sijui nani ,oh Mama Maria Nyerere alikuwa sijui na duka la mafuta taa Magomeni ,Mwanae Andrew akakataa mama yake hakuwa na duka hilo

Kama sio hekaya hizi ni nini ?

Endelea na Hekaya zako

Mimi nimemaliza
 
Akina Shekilango waliobaki wanaishi pale Lushoto Kialilo nyuma au juu ya Chuo Cha Uongozi wa Mahakama
 
Back
Top Bottom