Mfahamu Hoyce Temu katika ulimwengu wa Diplomasia na Mahusiano ya Kimataifa

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
MFAHAMU HOYCE TEMU KATIKA ULIMWENGU WA DIPLOMASIA NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA

IMG-20210523-WA0011.jpg
📍Hoyce Temu alisoma Stashahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Mahusiano ya Kigeni yaani Post Graduate Diploma in Management of Foreign Relations (PGD-MFR) kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini Dar es Salaam ama Mozambique-Tanzania Centre for Foreign Relations (CFR).

📍Hoyce Temu aliwahi kuhudumu Umoja wa Mataifa Tanzania (UN-Tanzania) kama Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano lakini pia alipata kuhudumu kama Mtaalamu wa Mawasiliano UN-Tanzania (UN Communication Specialist) na pia Mchambuzi wa Mawasiliano au UN Communication Specialist.

📍Hivyo Hoyce Temu ana taaluma ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia na zaidi ya hilo ana weledi wa masauala ya kidiplomasia kutokana na kufanya kazi UN ofisi ya Tanzania.

📍kwa kifupi, alichosoma Hoyce Temu ndicho walichosoma maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao kikanuni ni lazima wasome kozi za Chuo cha Diplomasia (CFR) kama kigezo kimojawapo cha kutoka ngazi moja ya daraja kwenda lingine ili waweze kumudu majukumu yao ipasavyo.
 
Nilifikiri ni ulimbwende tu, kumbe yuko vizuri nafikiri kapelekwa katika eneo lake haswa.

Nafikiri Mama anataka kuirejesha Tanzania katika Diplomasia ambayo ilichezewa na kuchafuliwa wakati wa Mwendazake.

Hongera Mama umeanza vyema kasoro moja hizi habari za kuteuwa Balozi 60+ zimepitwa na wakati.
 
Nilifikiri ni ulimbwende tu,kumbe yuko vizuri nafikiri kapelekwa katika eneo lake haswa...
Hakuna mtu aliyechafua diplomasia ya hii nchi kama Kikwete,nakumbuka ni wakati wa Kikwete ndipo tulipopata COW of Uganda,Kenya and Rwanda,ni kipindi cha Kikwete ndipo Malawi walitaka kujikatia Ziwa lao,nambie sasa nani kati ya JK na Magu aliyevurunda,usiniambie ile tabia ya kujikomba kwa Wazungu ndo diplomasia
 
Prof Jay huita Zali la mentali
Si zali bali anastahili.tatizo la nchi yetu wengi walio ktk nafasi za uongozi sio viongozi bali wameshika nafasi za watu wanaoweza kuwa na tija kwa jamii na Taifa. Nimependa Mfumo wa mama wa wa kufukua viongozi sahihi huko walipo. Hata anayoyafanya sasa Balozi Hoyce katika jamii ni sifa kubwa ya aina ya watu wanaotakiwa kuwa viongozi.
 
Back
Top Bottom