Mfahamu Gerald Ford, Rais wa 38 wa Marekani, miongoni mwa watu wenye bahati Duniani

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,783
66,962
Habari wakuu,

Leo nawaletea uzi unaomuhusu Gerald Ford aliyepata kuwa Rais wa 38 wa Marekani. Pengine huyu ni mmoja wa wanadamu wenye bahati zaidi kuwahi kutokea. Je, Tanzania tunaweza kupata mtu mwenye bahati kama huyu?

Yafuatayo ni mambo muhimu kuhusu Rais Gerald Ford.

1. Jina lake kamili ni Gerald Rudolph Ford Junior alizaliwa 14 July 1913 huko Nebraska.
Alifariki 26 December 2006 na kuzikwa kitaifa. Kitaaluma alikuwa ni mwanasheria ambapo alisoma katika chuo kikuu cha Michigan. Pia alipitia jeshini kwa miaka minne kutoka mwaka 1942 a 1946 na kushiriki vita kuu ya pili ya dunia.

2. Alikuwa ni sehemu ya bunge la Marekani kupitia chama cha Republican kuanzia mwaka 1949 mpaka 1973 akiwakilisha jimbo la Michigan. Mmoja kati ya viongozi mahiri kuwahi kutokea jimboni Michigan.

3. Ndoto zake za kujaribu kuwa Spika wa Bunge la Marekani ziliyeyuka baada ya kuwekewa mizengwe mingi ndani ya bunge na chama chake kutokana na misimamo yake isiyoyumba.

4. Mara baada ya mauaji ya Rais John F. Kennedy, Gerald Ford aliteuliwa kwenye tume iliyoundwa na Rais Lyndon B. Johnson chini ya Jaji Mkuu Earl Warren kuchunguza kifo cha John F. Kennedy. Ni kutokana na umahiri wake ndio ulimfanya awepo kwenye tume hiyo iliyojulikana kama "The Warren Commission"

5. Mwaka 1973, ndio mwaka ambao bahati ilianza kumdondokea Gerald Ford. Aliteuliwa na Rais Richard Nixon kutoka katika Bunge la Marekani na kwenda kuwa Makamu wa Rais wa 40 wa USA. Hivyo kumfanya kuwa Makamu wa Rais ambaye hakuchaguliwa na kura za wananchi.

6. Hii ni baada ya kujiuzulu kwa Makamu wa Rais wa wakati huo Spiro Agnew ambaye alikumbwa na tuhuma za rushwa, utakatishaji wa pesa na ukwepaji wa kodi kipindi akiwa Gavana wa Maryland. Makamu mpya wa Rais Gerald Ford akadumu kwenye wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu, 1973 - 1974.

7. Mwaka 1974 kukazuka skendo maarufu ya kisiasa ijulikanayo kama "Watergate Scandal" ambapo Rais Richard Nixon alituhumiwa kuwarekodi mazungumzo ya wapinzani wa chama cha Democratic kinyume na sheria za nchi, pia mbinu chafu za hila dhidi ya wapinzani hao. skendo ikavuja, wananchi wakashinikiza hatua zichukuliwe, Rais Richard Nixon akajiuzulu.

8. Katiba inasema Rais akijiuzulu basi Makamu wa Rais atakuwa Rais mpya. Hapo ndipo Makamu wa Rais Gerald Ford akaapishwa kuwa Rais wa 38 wa Marekani na kumalizia kipindi cha Urais kutoka 1974 - 1977. Rais Gerald Ford akawa Rais pasipo kuchaguliwa katika sanduku la kura na wananchi, na mpaka leo anabaki kuwa mtu pekee kushika nyadhifa za Makamu wa Rais pamoja na Rais wa Marekani pasipo kuchaguliwa kupitia Uchaguzi.

9. Mara baada ya kuwa Rais, Gerald Ford akaamua kwenda kinyume na matarajio ya wananchi wengi ni baada ya kuamua kumfutia mashtaka Rais mstaafu Richard Nixon. Yaani mashtaka yote yale ya Watergate Scandal yakafutwa, Nixon akapata kinga ya kutoshtakiwa, hii iliwachukiza Wamarekani wengi sana.

10. Wananchi wa Marekani wakamsubiria Rais Gerald Ford kwenye sanduku la kura na kumuangusha kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1976, ambapo mgombea wa upinzani Jimmy Carter alishinda kiti cha Urais na kutamatisha upepo wa bahati ya madaraka kwa Gerald Ford.

11.Pamoja na yote, Gerald Ford anabakia kama mmoja kati ya binadamu wenye bahati duniani na mtu pekee kuwahi kushika nyadhifa za Makamu wa Rais pamoja na Rais wa Marekani bila ya kuchaguliwa kwenye sanduku la kura. Lakini ulipowadia wakati wa Uchaguzi na kwakuwa wenzetu uchaguzi wao ni huru, Gerald Ford alianguka vibaya sana. Sijui kwa yanayoendelea hapa kwetu kama yanaweza yakaja kutokea?

IMG_7557.jpg

MWISHO
 
View attachment 1728737

MWISHO
Je wajua rais Magufuli ni rais aliye ongoza kwa mda mchache Tanzania
 
Back
Top Bottom