Mfahamu Generali Muhammad Suharto: Mbabe wa Kivita, Chinja Chinja, Gaidi na Kibaraka wa Marekani

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
487
1,000
ALIYETUMIKA KUMNG'OA MWANAMAJUMUI NA MUASISI WA TAIFA LA INDONESIA CHIEF SURKANO

Suharto.png

BY LUGETE MUSSA LUGETE

Tunapozungumzia uongozi wa kimkakati tunamaanisha mpango wa maendeleo wa mda mrefu wenye lengo la kuivusha nchi kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa miaka kadhaa, uongozi huo utajikita kuishi na kufuata mpango wa muda mrefu wa Taifa mfano mpango wa maendeleo wa miaka hamsini au Mia moja.

Kama Taifa wananchi, vyombo vya ulinzi na usalama, vyombo vya habari, wanasiasa, wadau wa maendeleo na mashirika binafsi wanapaswa kuelezwa dira ya Taifa kwa miaka ijayo, kila kiongozi atapaswa kufuata dira hiyo ili kulifanya Taifa kuwa na mwelekeo.

Nchi ya Indonesia ni moja ya nchi maarufu duniani kutoka ukanda wa mashariki ya mbali kulingana na historia yake, uchumi na siasa zake, maendeleo na ustaraabu wa Indonesia ni matokeo ya mpango na uongozi wa kimkakati wa dikteta Generali Muhammad Suharto, kiongozi wa kijeshi wa Indonesia kuanzia mwaka 1965_1998.

Muhammad Suharto alizaliwa tarehe 8/6/1921 katika kijiji kidogo cha Kemusuk mashariki mwa mji wa Yogyakarta, katika kabila la Javana ambalo kimsingi ndio wenyeji wa nchi ya Indonesia. Enzi hizo kulikuwa na utawala wa kikoloni kutoka kwa wadachi yaani makaburi. Baba yake Suharto alikuwa anaitwa Kertosudiro na kazi yake ilikuwa ni afisa kilimo wa kijiji wakati mama yake alikuwa anaitwa Sukira ambaye alikuwa ni Mkulima wa mpunga.

Wiki tano baada ya Suharto kuzaliwa mama yake alipata ugonjwa wa kichaa cha uzazi ikabidi mtoto Suharto awe chini ya Malezi ya shangazi yake, baadae wazazi wake Suharto waliachana kutokana na ugonjwa wa kichaa cha uzazi. Mwaka 1929 Mama yake Suharto alipona kichaa cha uzazi na kuolewa na mwanaume mwingine. Mwaka 1931 akiwa na miaka kumi mtoto Suharto alihamia katika kijiji cha Wonogiri ili apate huduma ya elimu. Mwaka 1935 mtoto Suharto alifukuzwa shule kwa kukosa ada kutokana na kutengana wazazi wake na umasikini uliotopea zama zile nchini Indonesia.

Suharto alikuwa mtoto mwenye nidhamu sana halafu mcheshi kutokana na umbile lake la ufupi na unene kiasi hivyo alikuwa kibonge wa darasa. Baadae mtoto Suharto alianza kubadilika kitabia kama ujuavyo kwamba mwanadamu hubadilika kitabia na haiba kulingana na Malezi, historia, mazingira, dini na mfumo wa siasa katika jamii yake. Baba yake alimchukua mtoto Suharto na kumpeleka shule ya kiislamu inayotambulika kwa jina la Muhammadiya ambapo mtoto Suharto alianza kujifunza masomo ya dini ya kiislamu kama kusoma Qur’an, Fiqih (Sheria za dini ya kiislamu), Tawheed yaani sifa na upekee wa Mungu na sira yaani visa na historia enzi za Mtume Muhammad (S.A.W).

Mwaka 1939 akiwa na miaka 18 Muhammad Suharto alianza kazi ya benki katika mji mdogo wa Wuryantaro, baada ya vita vya pili vya dunia kuanza Jeshi la kikoloni la Indonesia yaani Royal Nertherland East indies Army (KNIL) lilitoa tamko kwa vijana kuingia Jeshini ili kuokoa jahazi kwa sababu Japan ilikuwa inamshambulia Indonesia katika ukanda wa pasifiki ili kurejesha makoloni yake. Mwaka 1940 Muhammad Suharto alijunga na jeshi la Uhoranzi na kupelekwa kwenye kambi ya Gombong kwa mafunzo karibu na kijiji cha kwao Yogyakarta. Baada ya kuonyesha juhudi na umakini katika mafunzo ya kijeshi Muhammad Suharto alitunukiwa cheo cha Sajenti.

Mwaka 1942 Generali wa Japan Hideki Tojo aliuteka mji wa Jarkata na jeshi la kidachi likasalimu amri. Muhammad Suharto aliacha kazi kwenye Jeshi la kidachi na kuunga mkono serikali ya Japan, Japan na Uhoranzi walikuwa wanagombania utajiri wa mafuta na dhahabu kutoka Indonesia na jimbo la watu wenye asili ya Afrika yaani Melanesian West Papua Guinea.

Mwaka 1943 mwezi septemba Muhammad Suharto alipelekwa kwenye mafunzo ya polisi ili kudhibiti uhalibifu na wizi na alimudu vizuri mafunzo ya upolisi. Mwaka 1945 mwezi August Japan ilipigwa na Marekani kwenye shambulio la anga hasa majimbo ya Hiroshima na Nagasaki na kupelekea Japan kukosa nguvu za kutawala nchi za mashariki ya mbali hivyo Indonesia ikajipa uhuru.

Chief Surkano (1901-1970) akajipa uraisi wa kwanza wa nchi ya Indonesia kuanzia mwaka huo 1945_1967 na Muhammad Hatta (1902_1980) akawa makamu wa Raisi Indonesia. Wakati uhuru unatokea Muhammad Suharto hakuwepo mji wa Jarkata alikuwa kambini akisimamia askari wachanga. Baadae chief Surkano akaunda Jeshi la nchi ya Indonesia na Muhammad Suharto akapewa cheo cha Luteni Kanali. Chama cha kijamaa cha serikali ya Indonesia kilianza kumtuhumu Luteni Kanali Muhammad Suharto kwa kashfa za kuuza madawa ya kulevya na ulanguzi. Kashfa hizo ziligomba mwamba kwa sababu Jeshi la Indonesia lilisema haliingiliwi na wanasiasa wenye majungu na fitina.

Mwaka 1946 serikali ya kidachi ilitaka kurudi kutawala Indonesia na Chief Surkano na Muhammad Hatta walikamatwa lakini mwaka 1949 Jeshi la Indonesia lilifanikiwa kudhibiti hali hiyo na amani ikarejea, Luteni Kanali Muhammad Suharto alifanya kazi kubwa sana kuwafukuza mabeberu wa kidachi. Mkuu wa majeshi wa kwanza wa Indonesia Generali Abdul Nasution (1918_2000) alimsifu sana Muhammad Suharto.

Mwaka 1967 wakati wa mapinduzi ya Indonesia Muhammad Suharto alifunga ndoa na Siti Hartinah (1923_1996) waliishi kuanzia mwaka 1967_1996 mpaka Madam Siti anafariki mwaka 1996 walikuwa na watoto sita ambao ni Siti Hardiyanti Rukmana, Sigiti Harjojudanta, Bambang Trihatmodjo, Siti Hediat, Hutomo Mandala Putra na Siti Hutami.

Mwaka 1950 Muhammad Suharto alipanda cheo na kuwa Kanali katika kikosi cha mji wa Java.

The Makassar Rebellion April 1950.

Katika mji wa Makassar Jeshi la Indonesia liligoma na kugawanyika makundi mawili kwa sababu kuna baadhi ya wanajeshi walitaka kuwa chini ya Uhoranzi na wengine chini ya serikali ya Indonesia hivyo Mamluki wenye itikadi za kidachi walikuwa chini ya Kepteni Andi Azizi hivyo Raisi Surkano akamtuma Kanali Muhammad Suharto kutuliza mazingaombwe hayo, wataalamu wanasema kwamba zaidi ya wanajeshi Mia mbili walichinjwa chini ya amri ya Kanali Muhammad Suharto, baadae Muhammad Suharto alipandishwa cheo kuwa Brigedia General, baadae akapelekwa kwenye mji wa Bandung kupambana na magaidi wa madawa ya kulevya na ulanguzi huku nako aliua watu wengi sana hasa wahalifu na wema, alifanya operesheni usiku na mchana kusaka magenge ya wauza unga na makundi mbalimbali ya waasi. Mwaka 1960 alipandishwa cheo na kuwa Major Generali Muhammad Suharto.

Ujamaa na Falsafa za Jeshi.

Tafrani na mtafaluku ulianza baada ya Raisi wa kwanza chief Surkano na makamu wa Raisi Muhammad Hatta kutaka wanajeshi kupunguziwa mishahara kwa sababu Indonesia ilikuwa na jukumu la ukombozi kwa nchi za Afrika na Asia (Rejea makubaliano ya mkutano wa Bandung mwaka 1955). Pia serikali ya Marekani na Uingereza waliweka vikwazo vya kiuchumi kwa Indonesia baada ya mzozo kati ya India na Pakistan ilionekana kwamba Indonesia ipo upande wa Pakistan kwa sababu ya udini yaani uislamu. Jeshi la Indonesia likaanza kuipinga serikali ya Raisi Surkano. Baadae chief Surkano akaenda kuomba misaada Urusi na China hata hivyo Jeshi liliendelea kumpinga.

Hapa kuna dhana mbili juu ya hili suala mosi serikali ya Marekani ilimtumia Major General Muhammad Suharto ili kudhibiti Ujamaa nchini Indonesia na kumuondoa madarakani Raisi Surkano. Pili Jeshi la Indonesia lilikuwa linapigania maslahi yake dhidi ya serikali.

Serikali ya Marekani enzi za vita baridi yaani kuanzia mwaka 1945_1991 ilifanya hujuma nyingi dhidi ya viongozi mbalimbali wenye itikadi za kijamaa mfano mwaka 1966 Jeshi la Ghana chini ya Generali Joseph Arthur Ankrah lilimpindua Kwame Nkrumah kwa sababu alikuwa mwiba kwa maslahi ya Marekani na mabeberu Afrika. Hata nchini Congo kinshasa mwaka 1961 Waziri Mkuu Patrick Lumumba aliuawa kwa hisani ya nchi za Magharibi hasa Marekani, uingereza, Ufaransa na Uberigiji.

Mnamo tarehe 1/10/1965 Majenerali sita wa Jeshi la Indonesia walitekwa na kuuawa kwa amri za Generali Muhammad Suharto na serikali ya Marekani iliunga mkono huku General Muhammad Suharto akitangazwa kama shujaa wa mabeberu.

Mauaji ya halaiki kwa wanasiasa nchini Indonesia 1965_1966.

Haya yalikuwa mauaji dhidi ya viongozi na wafuasi wa chama cha kikomonisti wa Indonesia, zaidi ya wanachama laki tano waliuawa kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la umoja wa mataifa, Hii ilikuwa ni mbinu ya Generali Muhammad Suharto kuwafunga mdomo watu wenye mawazo hasi dhidi ya utawala wa kijeshi.

Mwaka 1965 Generali Muhammad Suharto alimuweka chini ya ulinzi raisi wa Indonesia Surkano na baadae kutangaza kwamba Raisi Surkano ameacha kazi kwa hiari kumbe ni mapinduzi ya kijeshi.

Utawala wa General Muhammad Suharto 1965-1998.

General Muhammad Suharto alikuwa ni dikteta, Shujaa na mwanamapinduzi. Kwanza alitengeneza mpango wa maendeleo ya nchi ya Indonesia wa miaka sabini. Yaani Indonesian Development plan 1965 _2035. Mpango huo ulijikita kwenye kilimo, biashara, viwanda na watu kufanya kazi kwa bidii huku akilipa Jeshi uwezo wa kuingilia kati sera za maendeleo ya nchi. Watu wazembe, wavivu na walevi walipata adhabu kali na watumishi wa umma wenye tamaa na Rushwa walinyongwa. lengo kuu ilikuwa kuivusha Indonesia kutoka kwenye umasikini uliotopea mpaka kuwa nchi bora ya mfano mashariki ya mbali.

Mwaka 1969 Generali Muhammad Suharto alibadilisha katiba na kulipa uwezo Bunge kumchagua raisi hivyo akawa anapitishwa na Bunge bila kupingwa hapo pia kuna nadharia mbili Kuhusu hilo mfano utendaji wake bora ndio sababu Bunge lilimpitisha au udikteta wake na utawala wa kijeshi. Kiujumla nidhamu, hofu, uchapakazi na moyo wa kizalendo viliwajaa na kuwajenga wananchi wa Indonesia chini ya utawala wa General Muhammad Suharto.

Nchi za Magharibi kama Marekani, uingereza na Ufaransa zilimpenda sana Generali Muhammad Suharto kwa sababu alipinga Ujamaa hasa urafiki na Urusi ulikufa. Viongozi mbalimbali wa kibeberu walitembelea nchini Indonesia kujionea juhudi na maarifa ya uongozi wa kimkakati na udikteta wa Generali Muhammad Suharto mfano Waziri Mkuu wa Australia John Gorton mwaka 1968, Raisi wa 38 wa Marekani ndugu Gerald Ford alitembelea Indonesia akiwa na katibu Mkuu wa Marekani Henry Kissinger.

Faida za uongozi wa kimkakati na udikteta wa Generali Muhammad Suharto 1965-1998.

Nchi ilisonga mbele kwa ubabe, mauaji na watu kufundishwa mipango mizito ya kuivusha Indonesia ili iwe Taifa bora.

_Alijenga miundombinu nchi nzima kwa kutumia Jeshi la Indonesia kuanzia barabara, viwanja vya ndege, nyumba za watumishi wa umma, madaraja na viwanda.

_Alipunguza umasikini kutoka asilimia 70 mwaka 1965 mpaka asilimia 11 mwaka 1996.
Uwezo wa watu kufanya kazi kwa bidii hasa kilimo na viwandani.

-Pato la Taifa lilikuwa kwa asilimia 70 Kutoka mwaka 1965 ambapo ilikuwa Dola laki tatu mpaka mwaka 1996 ambapo ilifikia zaidi ya Dola million Mia nane. Hii ilitokana na mafuta, chakula Madini.

_Mawasiliano yaliimalishwa kwa kiwango kikubwa sana hasa makampuni kutoka China na Marekani yalikaribishwa kuwekeza kwa mikataba yenye maslahi kwa Taifa. Mfano mwaka 1994 Generali Muhammad Suharto alinyonga wanasheria 20 kwa kosa la kusaini mkataba wenye kulihujumu Taifa.

_Kilimo kilipanda kwa asilimia tisini mfano mwaka 1984 shirika la chakula duniani FAO lilimpa tuzo Generali Muhammad Suharto kwa kuzalisha mchele mwingi duniani. Miaka hiyo kulikuwa na njaa sana Afrika na mashariki ya kati. Hakika huyo ndio Muhammad Suharto.

_Mwaka 1977 Generali Muhammad Suharto alifungua masoko kumi ya hisa nchini Indonesia.

Mwaka 1997 nchi ya Indonesia iliingia kwenye mtikisiko wa Kiuchumi baada ya serikali na makampuni kutoka China kupewa tenda na zabuni nyingi hivyo Marekani wakaamua kumuwekea vikwazo vya kiuchumi Generali Muhammad Suharto, hivyo mwaka 1998 Mbabe wa kivita na mwanamapinduzi wa uchumi wa Indonesia Generali Muhammad Suharto aliamua kujiuzuru kutokana na sababu za kiafya pia uzee tayali ulikuwa unamuandama huku wadau wa siasa za mashariki ya mbali wanadai ni kwa sababu ya vuguvugu za maandamano.

Baada ya kujiuzuru Bunge la Indonesia lilifanikiwa kumchagua Bacharuddini Jusuf Habibie kuwa Raisi wa muda wa Indonesia kuanzia mwaka 1998_1999, ambapo baadae mwaka 1999 Mwishoni uchaguzi Mkuu ulifanyika nchini Indonesia na Abdurrahman Wadi alichaguliwa kuwa Raisi wa Indonesia kuanzia mwaka 1999_2002 yaani miaka minne kwa mujibu wa katiba ya Indonesia.

Tarehe 27/1/2008 Generali Muhammad Suharto aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 87.
 
Top Bottom