(MAZINGE WA INDIA)
Dr. Zakir Naik
Dr. Zakir Naik kwa wale watazamaji wa TV iitwayo Peace Tv inayo endesha vipindi vya dini sio sura ngeni kwa mtaalamu huyu.Dr. Zakir Naik
Dr. Naik ni mwanaharakati wa dini ya Kiislamu nchini India, aliejizolea umaarufu mkubwa sana kwa yeye kuzunguka nchi mbalimbali za bara la Ulaya na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasilimisha Wazungu wengi kupitia hoja mbalimbali.
Dr. Naik allah kamjaalia elimu ya dini Masha Allah na elimu ya Mazingira, ni Muhindi aliefanya kazi kubwa mno nchini kwao, kwani India ndio nchi inayoongoza duniani kwa watu wake kuabudia vitu visivyokuwa na mashiko na kuviita ndio Mungu.
Dr. Naik alipoliona hilo akaanzisha mijadala kama ya kina Mazinge kuhusu dini wanazoabudia na miungu wanayoabudia huko nchini India.
Basi hapo ndipo alipoanza kujizolea umaarufu duniani kwa kupambana vikali na wahindi wenzie kwa kuwapa hoja nzito nzito kuhusu Mungu wa kweli ambae ni Allah subhanahu wataala.
Dr. Zakir Naik alianza kazi zake za ulinganiaji kwa kukutana na upinzani mkubwa sana nchini kwake, kwani ilifikia kipindi mpaka kunusurika kuuwawa mara kadhaa na kuitwa gaidi haswa kwa daawa anazozifanya nchini kwao.
Dr. Zakir aliamua kufungua shule haswa ya kutengeneza vijana ambao watakaoifanya kazi hii huko mbeleni, kwani aliamini yeye ni binaadam ipo siku anaweza akaumwa au akaondoka duniani haswaa.
Na katika hilo amefanikiwa Masha Allah kwani ana vijana wa kiume na wakike ambao amewatengeneza kwa ajili ya kuuhami Uislam kwa hoja nzito nzito.
Katika kanuni alizojiwekea katika maisha yake na kupitia kipaji alicho nacho ni kuhakikisha kila sehemu anayo tembelea na kufanya mihadhara yake ni furaha kwake kuhakikisha anawasilimisha watu na kuwaingiza ktk dini tukufu ya kiislamu.
Dr. Zakir Naik amekuwa mwiba mkubwa sana kwa watu wasio Waislamu kwa kuwaonyesha kwa maandiko upotovu walionao katika miungu wanayoabudia.
Kuna baadhi ya nchi kama vile Uingereza alipigwa marufuku ya kuingia nchini humo kwasababu ya kuwasilimisha wazungu wengi kupitia hoja mbalimbali za kwenye vitabu vitakatifu.
Dr. Zakir Naik huanzisha mijadala yenye mashiko popote pale anapokuwepo, iwe kwenye treni, ndege, daladala mpaka mitaani. Ama kweli Dr. amejitoa zaidi kwaajili ya Uislamu.
Dr. Zakir Naik alitoa mchango wake mkubwa sana kipindi Quran inatafsiriwa kwa lugha ya Kihindi, ikiwa Dr, Allah kamjaalia kuzungumza lugha kuanzia tatu yani Kiarabu, Kiingereza na Kihindi na baadhi ya lugha kwa uchache.
Tosheka na historia fupi ya mwanaharakati wa Kiislam.