Mfahamu Daktari Aliyegundua Dawa Iliyotibu Ugonjwa Hatari wa Polio na Hati Miliki Ya Dawa Hiyo likapewa Jua

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,037
20,333
MFAHAMU DAKTARI ALIYEGUNDUA DAWA ILIYOTIBU UGONJWA HATARI WA POLIO NA HATI MILIKI YA DAWA HIYO LIKAPEWA JUA.


FB_IMG_1637039231355.jpg


Jonas Salk alikuwa mtafiti na mgunduzi wa dawa ya ugonjwa wa polio alizaliwa October 28, mwaka 1914 New York , marekani .

polio ni Ugonjwa wa kuambukiza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine , mtu akipata ugonjwa huo husababisha mwili kupooza na viungo vya mwili vinakuwa havina uwezo hata wa kutikisika.
Ugonjwa huo kwa asilimia kubwa ulikuwa ukiwathiri watoto wadogo .

mwanzoni mwa karne ya 20 Ugonjwa wa polio ulikuwa tishio na wenye kuogopwa kuliko ugonjwa wowote nchini marekani.

Utafiti mwingi ulifanywa juu ya ugonjwa huo, wananchi pia walishiriki kutoa fedha zao kufanikisha utafiti huo mmoja wa watafiti alikuwa Jonas Salk kutoka chuo kikuu cha Pittsburgh ambaye ndiye aliyefanikiwa kugundua chanjo ya ugonjwa huo ambao ulikuwa ni tishio.

Mwanzo wa utafiti wa dokta Salk ulianzia kwa wanyama kama vile nyani alipoona ya kuwa chanjo hiyo inafanya kazi ndipo mwaka 1952 aliamua kuitumia yeye pamoja na familia yake kwa mara ya kwanza dawa hiyo ilionekana kufanya kazi vizuri kabisa.

Ilipofika Machi 26, mwaka 1953 Dkt Salk alipokuwa kwenye kipindi cha redio ya kitaifa alisema kuwa amefanikiwa kupata chanjo ya ugonjwa wa polio.

Mwanzoni chanjo hii haikukubaliwa na kuweza kutumika nchini marekani hivyo majaribio ya chanjo hiyo yalifanyika sehemu nyingine nje ya marekani na kuleta mafanikio chanya.

Ilipofika mwaka 1955 chanjo ya hiyo rasmi ilikubalika na kuanza kutumika nchini marekani .

mwanahabari wa CBS Edward R. Murrow alipomuuliza mwanasayansi huyo hakimili ya dawa hiyo inakwenda kwa nani alijibu jua ndilo lenye haki ya kupata haki miliki pili alizungumza kuwa wananchi waliotoa fedha zao kufanikisha utafiti huo ndio waliokuwa na haki ya kuamua nani anapaswa kupewa hakimiliki.

Wanasayansi wengine kama vila Albert Sabin alifanikiwa pia kugundua chanjo ya ugonjwa wa polio lakini chanjo yake ilikuwa ya mdomo .

Kwa sababu chanjo ya milk ilikuwa ikiamika nchini marekani na kuleta mafanikio makubwa sabin hakuweza kupata msaada wowote juu ya utafiti wake alioufanya juu ya chanjo nyingine ya ugonjwa wa polio.

Ilipofika 1957, Sabin aliishawishi Wizara ya Afya ya Umoja wa Kisovieti kuchunguza chanjo yake ya polio , jaribio hilo lilifanyika na kumaliza mwaka 1960 na mwaka 1961 chanjo hiyo iliruhusiwa kutumika nchini marekani , hata shirika la afya duniani WHO iliunnga mkono matumizi ya chanjo hiyo.

Salk alifariki dunia huko La Jolla, California mwaka 1995
 
Alipoulizwa kama ataweka hati miliki ya chanjo yake, akasema

"Can you patent the sun? "

Jua si mali ya mtu yoyote yule, tulilikuta
Hakuna mwenye haki ya hati miliki ya jua
The same na chanjo yake

Hakulipa hati miliki jua kwa muktadha huo,alitaka chanjo yake iwe free kwa kila mtu
 
Alipoulizwa kama ataweka hati miliki ya chanjo yake, akasema

"Can you patent the sun? "

Jua si mali ya mtu yoyote yule, tulilikuta
Hakuna mwenye haki ya hati miliki ya jua
The same na chanjo yake

Hakulipa hati miliki jua kwa muktadha huo,alitaka chanjo yake iwe free kwa kila mtu
means mwandishi amekurupuka🤳
 
Alipoulizwa kama ataweka hati miliki ya chanjo yake, akasema

"Can you patent the sun? "

Jua si mali ya mtu yoyote yule, tulilikuta
Hakuna mwenye haki ya hati miliki ya jua
The same na chanjo yake

Hakulipa hati miliki jua kwa muktadha huo,alitaka chanjo yake iwe free kwa kila mtu
Asante sana mkuu kwa nyongeza
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom