Mfahamu Black Alien: Mtu mwenye ndoto ya kufanana na viumbe vya ulimwengu mwingine (Aliens)

Nachojiuliza hizi gharama za kufanyiwa upasuaji nani analipia?kama ni yeye anafanya kazi kazi kumudu hizo gharama?
 

Anthony Loffredo pia anajulikana kama black alien. Anashikilia rekodi ya mtu aliyejifanyia maboresho mengi makubwa kabisa katika mwili wake kuliko binadamu mwingine kwa karne hii.

Ameendelea kushika vichwa mbalimbali vya vyombo vya habari kwa ujasiri wake kwa kuamua kutenganisha kati ulimi wake, kukata masikio, kutapakaza tatoo toka kichwani mpaka kwenye nyayo, kujitoboa na mwili kwa kuongeza vyuma na hata kukata pua.

Mpaka sasa amesha fanikisha maboresho muonekano kiupasuaji 34%.


Mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 33 sasa, kutoka Ufaransa amejidhamiria haswa katika ndoto yake ya kufanana na elieni "black elien". Kwa sasa sio mgeni katika meza za uparation tena. Hivi karibuni aliamua kufanya maboresho zaidi kwa kuondoa vidole vyake viwili ili kufananisha na ukucha haijatosha alishatoa pia hata mdomo wake wa juu kwa siku zilizopita mapema mwaka huu.

Anthony - amekuwa akijifanyia mabadiliko mwilini kwake karibia miaka kumi sasa - amekuwa jasiri hata kujaribu kuchora tatoo kwenye jicho pamoja na kujua angeweza kupofuka.

Mwaka jana, Anthony alisafiri kwenda Spain kufanya uparasheni ya kuondoa pua kwa sababu aina hizo za uparasheni ni kosa kwenye nchi yake.


Ana matumaini ya kupunguza uonekano wa kibinadamu, pia alishapandikiza vipandikizi kwenye uso vinavyoipa ngozi yake muonekano wa vinundu pia na muonekano wa reptilia kwenye paji la uso na alama ya mpasuko kukatiza kwenye mfupa wa shavu.


Anthony anasema ndiyo kwanza yupo hatua ya tatu katika mabadiliko yake anayoyategemea.

Katika maboresho yake ya hivi karibuni alisikika akisema " najitengenezea amani yangu ya ndani."

usituaminishe stori za kwenye movie mkuu, sisi sio watoto.
 
Kuna wakati unaweza kujifikiria kua wewe ni mjinga sana ila kumbe kuna wajinga zaidi yako.sasa huyo hizo shida zote za nini.ila hawa watu wenye hii rangi kama yule mfugo wana mambo mengi sana ya ajabu ajabu.
 
Kuna wakati unaweza kujifikiria kua wewe ni mjinga sana ila kumbe kuna wajinga zaidi yako.sasa huyo hizo shida zote za nini.ila hawa watu wenye hii rangi kama yule mfugo wana mambo mengi sana ya ajabu ajabu.
Watu washavurugwa sana na hili lyfu, hawana furaha ingawa hela ipo unafikiri nini kitatokea hapo?
 
Back
Top Bottom