Mfahamu Bi. Nancy Pelosi, Spika wa kwanza mwanamke katika Bunge la Wawakilishi la Marekani

Aug 15, 2013
50
95
NA COMRADE Leonard Waziri

Nancy Pelosi ni mama wa watoto watano mwenye damu ya Kiitaliano aliyezaliwa na kukulia kwenye familia yenye misingi ya kisiasa.

Baba yake mzazi mzee Thomas D'Alesandro Jr. alikuwa mbunge wa Maryland mnamo mwaka 1939-47 kabla ya kuwa Meya wa jiji la Baltimore hadi mwaka 1959. Jiji la Baltimore ndilo alilozaliwa na kukulia Bi. Nancy Pelosi alizaliwa 26 Machi mwaka 1940 kipindi hicho baba yake ni mbunge wa jimbo la Maryland.

Mama yake Nancy, aitwaye Annunciata Lombardi ni muitaliano aliyezaliwa mjini Campobas nchini Italy kabla ya kuhamia Marekani katika mji wa Baltimore uliosheheni raia wengi wa kigeni wakiwemo wayahudi na waitaliano. Wazazi wa baba yake D'Alesandro yaani Babu na Bibi yake Nancy Pelosi wote ni wazaliwa wa Italy waliohamia nchini Italy na kuishi katika mji wa Baltimore, katika sehemu ambayo leo hii inaitwa 'Little Italy' kutokana na wingi wa Waitaliano.

Ukiachilia mbali baba, hata kaka yake Nancy Pelosi aitwaye Thomas D'Alesandro III, aliwahi pia kuwa meya katika jiji hilo hilo la Baltimore kuanzia mwaka 1967 hadi 1971 akikumbukwa kwa kuongoza bila kujali tofauti za rangi wala kabila kitu kilichopelekea apendwe na watu wa asili zote pale jijini Baltimore. Mfano jamii ya wayahudi waishio Baltimore walitokea kumkubali sana meya wao kiasi cha kujenga uwanja wa michezo huko nchini Israel na kuupa jina 'Thomas D'Alesandro Stadium' kwa heshima ya kaka wa Bi. Nancy Pelosi, Thomas D'Alesandro III aliyetumikia jeshi la Marekani katika miaka ya nyuma na kufariki oktoba 2019

Kabla ya kuwa mbunge mwaka huo 1987, Bi Nancy Pelosi alishakuwa mwenyekiti wa chama cha Democrat katika jimbo la California mnamo 1981 hadi 1983. Pia amekua akishuhudia mikikimikiki ya siasa za Marekani wakati baba yake mbunge. Alipenda sana siasa za nchi yake ndio mana hakukubali kukosa kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais John F. Kennedy mwaka 1961. Alishawahi kufanya kazi kwenye ofisi ya seneta Daniel Brewster wa jimbo la Maryland. Kwa kifupi niseme kwamba Bi. Nancy Pelosi anazijua na kuzipenda siasa za Marekani ndio maana aliamua kwenda kusomea shahada ya sayansi ya siasa katika chuo cha Trinity College mwaka 1962. Kwahiyo kwa maelezo hayo mafupi utaona kuwa Bi. Nancy Pelosi naturally ni mwanasiasa tena by profession.

Mwaka 1977, Bi Nancy Pelosi alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la California kwenye kamati ya taifa ya chama cha Democrat nafasi aliyoishika kwa miaka ishirini sambamba na kuwa mwenyekiti wa chama hiko katika jimbo la California tangu 1976 na 1983. Vilevile alihudumu kama kiongozi wa kamati ya fedha katika kampeni za uchaguzi wa chama chake cha Democrat mnamo mwaka 1985 hadi 1986. Sasa si unaona jinsi mtu alivyozama kwenye siasa za Marekani na tena anaonekana ni mwanachama 'kindakindaki' wa chama cha Democrat kwani amedumu kwenye chama hiko tangu mwanzo,

Mwaka 1983, aliyekuwa mbunge wa California, Philip Burton alifariki dunia. Hivyo ilibidi kufanyike uchaguzi maalumu huku tunaita 'By election' kujaza nafasi ya mbunge huyo ambapo mkewe, aitwaye Sala Burton alichaguliwa kuwa mbunge wa California. Sala naye hakudumu sana kutokana na matatizo ya kiafya, akafariki mwaka 1987 hivyo ilibidi kufanyike tena uchaguzi mdogo wanaita 'special election' kuziba nafasi ya mbunge Sala Burton. Hapo ndipo sasa Bi Nancy Pelosi anapata nafasi ya kuingia katika bunge la Congress kama mbunge wa California 5th District kwa tiketi ya chama cha Democrat baada ya kushinda uchaguzi ule.

Miaka ile bunge la Congress lilidhibitiwa na chama cha Republican kwa kuwa na wabunge wengi zaidi. Chama chenye wabunge wengi huitwa 'majority' na kiongozi wake ni 'majority Leader' huku kile chenye wachache huitwa 'minority' na kiongozi wake aitwaye 'Minority Leader' ambapo kwa wakati huo alikuwa ni bwana mmoja aitwaye Dick Gephardt mbunge wa Missouri. Bi. Nancy Pelosi yeye alichaguliwa kuwa 'Minority Whip' yaani mnadhimu ambaye baada ya minority leader anafuata yeye kimamlaka.

Mwaka 2002, Dick Gephardt alijiuzulu nafasi yake kama Minority Leader ili awanie nafasi ya kukiwakilisha chama chake cha Democrat katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka 2004. Kwa kujiuzulu nafasi hiyo, kulimpa nafasi Bi. Nancy Pelosi kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama chenye wabunge wachache bungeni yaani House Minority Leader. Mnamo mwaka 2006 kwenye uchaguzi wa nusu muhula, chama cha Democrat 'kilifanya mapinduzi' kwa kufanikiwa kudhibiti bunge kwa kupata idadi kubwa ya wabunge.

Mabadiliko hayo yalimfanya Bi. Nancy Pelosi kuwa Majority Leader ambaye aliteuliwa na chama chake kuwania nafasi ya Uspika dhidi ya mRepublican John Boehner wa jimbo la Ohio. Uchaguzi ulifanyika siku ya January 3 2007 na kumshuhudia Bi Nancy Pelosi anafanikiwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la wawakilishi na kumfanya aandike historia ya kuwa

MWANAMKE WA KWANZA KUWA SPIKA WA BUNGE LA MAREKANI

Aliongoza bunge la wawakilishi hadi mwaka 2010 kwenye uchaguzi wa nusu muhula ambapo chama chake kikipata kura chache na hivyo kuangushwa na chama cha Republican katika kulidhibiti bunge. Hivyo bi Nancy Pelosi akangolewa kwenye uspika na kurudi kuwa Minority Leader nafasi aliyoshika hadi mwaka 2018 kwenye uchaguzi wa nusu muhula ambapo chama Cha Democrat kilifanikiwa tena kutwaa udhibiti wa bunge na kumfanya bi Nancy Pelosi achaguliwe tena kuwa spika wa bunge nafasi anayoishikilia hadi sasa!.

Hadi hapo utakuwa tayari umeshafahamu wasifu wa Bi.Nancy Pelosi, spika wa kwanza mwanamke katika bunge la congress.

Kwa kuhitimisha Alichonifurahisha zaidi ni namna anavyojiamini na kusimamia misingi yake ya kiuongozi Huyo ndio aliongoza mchakato wa kumng'oa Donald Trump na amefanikiwa katika bunge lake na hakupoteza muda kilichobaki ni katika bunge la senete ambalo mpaka sasa mchakato unaendelea.

Hakika amejua hasa namna ya kumpanikisha rais Trump tazama alivyomuandikia barua yenye maneno matatu 'Resign or Impeached' yaani 'Jiuzulu au Tukushtaki'. Barua hiyo ilimchukiza sana Trump ambaye aliamua kujibu kwa barua yenye kurasa sita iliyosheheni maneno makali dhidi ya spika, Bi. Nancy Pelosi

Ahsante kwa kusoma Makala hii fupi ya Kumtambua mtu huyu mashuhuri katika siasa za Marekani na Dunia kwa Ujumla

Comrade Leonard Waziri
2020

#TukutaneKazini
#Tujifunzekwawenzetu

images%20(2).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
4,951
2,000
Kitendo cha kuchana nakala ya hotuba ya Trump "dramatically" nimemuona naye ni wale wale tu!
 
NYAMUHANZI

Senior Member
Apr 7, 2017
135
250
Somo lako zuri ila hujaeleza alisomea wapi, hao watoto watano aliwapata katika ndoa au nje ya ndoa, vipi kuhusu jina maana sioni akitumia jina la baba yake (Pelosi alilitoa wapi?). nje ya siasa anajishughulisha na nini?
 
The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,379
2,000
Somo lako zuri ila hujaeleza alisomea wapi, hao watoto watano aliwapata katika ndoa au nje ya ndoa, vipi kuhusu jina maana sioni akitumia jina la baba yake (Pelosi alilitoa wapi?). nje ya siasa anajishughulisha na nini?
ikijibiwa nitag
 
jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
6,764
2,000
Leonard Waziri,

Iron Lady, Trump is a liar, sexist, racist redneck, kuna siku FBI files zitakuwa disclassified kuhusu yeye ndipo mtaelewa.
 
mwimbule

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
559
250
Huyu kwa kuwa mwanamke wa kwanza spika wa baraza la wawakilishi Marekani amefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa na Maspika waote waliotangulia, la kuchana hotuba ya Raisi wa nchi yake,, hii inaonyesha asivyoweza kudhibiti hisia zake,, na pia kwa kitendo chake cha kundesha mashtaka dhidi ya Raisi bila kuzingatia haki, kumepelekea kuonyesha udhaifu mkubwa kwa barza la wawakilishi na uongozi wao.

Pia hii ndio jambo ambalo linafanya wamarekani wengi wasiwaamini wanawake na nafasi mbili kubwa za juu , Uraisi na Umakamu. Kihistoria hawajawahi kuwa na Mwanamke Raisi wala Makamu,, .Kwa vitendo alivyofanya Nancy Pelosi, kitawasaidia sana wafadhihina kuimraisha msimamo wao wa kuona wanawake hawafai kuaminiwa kwa nafasi kubwa,,kwa sababu ya kushindwa kuzuia hisia zao. Pili amewaangusha sana wanawake wenzake wengi wwaliopenda kushika nafais hizo za juu.
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
2,328
2,000
NA COMRADE Leonard Waziri

Nancy Pelosi ni mama wa watoto watano mwenye damu ya Kiitaliano aliyezaliwa na kukulia kwenye familia yenye misingi ya kisiasa.

Baba yake mzazi mzee Thomas D'Alesandro Jr. alikuwa mbunge wa Maryland mnamo mwaka 1939-47 kabla ya kuwa Meya wa jiji la Baltimore hadi mwaka 1959. Jiji la Baltimore ndilo alilozaliwa na kukulia Bi. Nancy Pelosi alizaliwa 26 Machi mwaka 1940 kipindi hicho baba yake ni mbunge wa jimbo la Maryland.

Mama yake Nancy, aitwaye Annunciata Lombardi ni muitaliano aliyezaliwa mjini Campobas nchini Italy kabla ya kuhamia Marekani katika mji wa Baltimore uliosheheni raia wengi wa kigeni wakiwemo wayahudi na waitaliano. Wazazi wa baba yake D'Alesandro yaani Babu na Bibi yake Nancy Pelosi wote ni wazaliwa wa Italy waliohamia nchini Italy na kuishi katika mji wa Baltimore, katika sehemu ambayo leo hii inaitwa 'Little Italy' kutokana na wingi wa Waitaliano.

Ukiachilia mbali baba, hata kaka yake Nancy Pelosi aitwaye Thomas D'Alesandro III, aliwahi pia kuwa meya katika jiji hilo hilo la Baltimore kuanzia mwaka 1967 hadi 1971 akikumbukwa kwa kuongoza bila kujali tofauti za rangi wala kabila kitu kilichopelekea apendwe na watu wa asili zote pale jijini Baltimore. Mfano jamii ya wayahudi waishio Baltimore walitokea kumkubali sana meya wao kiasi cha kujenga uwanja wa michezo huko nchini Israel na kuupa jina 'Thomas D'Alesandro Stadium' kwa heshima ya kaka wa Bi. Nancy Pelosi, Thomas D'Alesandro III aliyetumikia jeshi la Marekani katika miaka ya nyuma na kufariki oktoba 2019

Kabla ya kuwa mbunge mwaka huo 1987, Bi Nancy Pelosi alishakuwa mwenyekiti wa chama cha Democrat katika jimbo la California mnamo 1981 hadi 1983. Pia amekua akishuhudia mikikimikiki ya siasa za Marekani wakati baba yake mbunge. Alipenda sana siasa za nchi yake ndio mana hakukubali kukosa kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais John F. Kennedy mwaka 1961. Alishawahi kufanya kazi kwenye ofisi ya seneta Daniel Brewster wa jimbo la Maryland. Kwa kifupi niseme kwamba Bi. Nancy Pelosi anazijua na kuzipenda siasa za Marekani ndio maana aliamua kwenda kusomea shahada ya sayansi ya siasa katika chuo cha Trinity College mwaka 1962. Kwahiyo kwa maelezo hayo mafupi utaona kuwa Bi. Nancy Pelosi naturally ni mwanasiasa tena by profession.

Mwaka 1977, Bi Nancy Pelosi alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la California kwenye kamati ya taifa ya chama cha Democrat nafasi aliyoishika kwa miaka ishirini sambamba na kuwa mwenyekiti wa chama hiko katika jimbo la California tangu 1976 na 1983. Vilevile alihudumu kama kiongozi wa kamati ya fedha katika kampeni za uchaguzi wa chama chake cha Democrat mnamo mwaka 1985 hadi 1986. Sasa si unaona jinsi mtu alivyozama kwenye siasa za Marekani na tena anaonekana ni mwanachama 'kindakindaki' wa chama cha Democrat kwani amedumu kwenye chama hiko tangu mwanzo,

Mwaka 1983, aliyekuwa mbunge wa California, Philip Burton alifariki dunia. Hivyo ilibidi kufanyike uchaguzi maalumu huku tunaita 'By election' kujaza nafasi ya mbunge huyo ambapo mkewe, aitwaye Sala Burton alichaguliwa kuwa mbunge wa California. Sala naye hakudumu sana kutokana na matatizo ya kiafya, akafariki mwaka 1987 hivyo ilibidi kufanyike tena uchaguzi mdogo wanaita 'special election' kuziba nafasi ya mbunge Sala Burton. Hapo ndipo sasa Bi Nancy Pelosi anapata nafasi ya kuingia katika bunge la Congress kama mbunge wa California 5th District kwa tiketi ya chama cha Democrat baada ya kushinda uchaguzi ule.

Miaka ile bunge la Congress lilidhibitiwa na chama cha Republican kwa kuwa na wabunge wengi zaidi. Chama chenye wabunge wengi huitwa 'majority' na kiongozi wake ni 'majority Leader' huku kile chenye wachache huitwa 'minority' na kiongozi wake aitwaye 'Minority Leader' ambapo kwa wakati huo alikuwa ni bwana mmoja aitwaye Dick Gephardt mbunge wa Missouri. Bi. Nancy Pelosi yeye alichaguliwa kuwa 'Minority Whip' yaani mnadhimu ambaye baada ya minority leader anafuata yeye kimamlaka.

Mwaka 2002, Dick Gephardt alijiuzulu nafasi yake kama Minority Leader ili awanie nafasi ya kukiwakilisha chama chake cha Democrat katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka 2004. Kwa kujiuzulu nafasi hiyo, kulimpa nafasi Bi. Nancy Pelosi kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama chenye wabunge wachache bungeni yaani House Minority Leader. Mnamo mwaka 2006 kwenye uchaguzi wa nusu muhula, chama cha Democrat 'kilifanya mapinduzi' kwa kufanikiwa kudhibiti bunge kwa kupata idadi kubwa ya wabunge.

Mabadiliko hayo yalimfanya Bi. Nancy Pelosi kuwa Majority Leader ambaye aliteuliwa na chama chake kuwania nafasi ya Uspika dhidi ya mRepublican John Boehner wa jimbo la Ohio. Uchaguzi ulifanyika siku ya January 3 2007 na kumshuhudia Bi Nancy Pelosi anafanikiwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la wawakilishi na kumfanya aandike historia ya kuwa

MWANAMKE WA KWANZA KUWA SPIKA WA BUNGE LA MAREKANI

Aliongoza bunge la wawakilishi hadi mwaka 2010 kwenye uchaguzi wa nusu muhula ambapo chama chake kikipata kura chache na hivyo kuangushwa na chama cha Republican katika kulidhibiti bunge. Hivyo bi Nancy Pelosi akangolewa kwenye uspika na kurudi kuwa Minority Leader nafasi aliyoshika hadi mwaka 2018 kwenye uchaguzi wa nusu muhula ambapo chama Cha Democrat kilifanikiwa tena kutwaa udhibiti wa bunge na kumfanya bi Nancy Pelosi achaguliwe tena kuwa spika wa bunge nafasi anayoishikilia hadi sasa!.

Hadi hapo utakuwa tayari umeshafahamu wasifu wa Bi.Nancy Pelosi, spika wa kwanza mwanamke katika bunge la congress.

Kwa kuhitimisha Alichonifurahisha zaidi ni namna anavyojiamini na kusimamia misingi yake ya kiuongozi Huyo ndio aliongoza mchakato wa kumng'oa Donald Trump na amefanikiwa katika bunge lake na hakupoteza muda kilichobaki ni katika bunge la senete ambalo mpaka sasa mchakato unaendelea.

Hakika amejua hasa namna ya kumpanikisha rais Trump tazama alivyomuandikia barua yenye maneno matatu 'Resign or Impeached' yaani 'Jiuzulu au Tukushtaki'. Barua hiyo ilimchukiza sana Trump ambaye aliamua kujibu kwa barua yenye kurasa sita iliyosheheni maneno makali dhidi ya spika, Bi. Nancy Pelosi

Ahsante kwa kusoma Makala hii fupi ya Kumtambua mtu huyu mashuhuri katika siasa za Marekani na Dunia kwa Ujumla

Comrade Leonard Waziri
2020

#TukutaneKazini
#Tujifunzekwawenzetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Je ana mume na watoto wangapi,tumeaminishwa watu kama hawa huwa hawakaa kwenye ndoa
 
Top Bottom