Mfahamu Anastazia Muro Mama anayekamua Lita 40 za Maziwa yake mwenyewe

Arobain kwa siku mbona ni mengi kuliko ya ng'ombe wa kisasa wa maziwa?
...Hajasema kwa Siku Mkuu. Amesema amekusanya hizo Lita 40 kwa Miezi Miwili toka aanze kuyakamua na kuyaweka kwenye pakti ndani ya friji kwa maana kwamba anapotaka kumpa mwanawe ni kiasi cha kuyapasha moto tu!!....
 
Dar es Salaam. Wakati baadhi ya wanawake wakiogopa kuwanyonyesha watoto wao kwa madai kuwa wataharibu muonekano wa matiti, hali ni tofauti kwa wakili Anastazia Muro (33), aliyeweka nadhiri ya kunyonyesha watoto wake kwa miezi sita bila kuwapa chochote huku akiwa ameanza kukamua maziwa na kuweka kwenye pakiti.

Tangu anaanze kukamua maziwa yake miezi miwili iliyopita ameshahifadhi pakiti 200 za maziwa zenye ujazo wa mililita 100 ambayo ni sawa na lita 40 au ndoo kubwa mbili za maji.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, maziwa ya mama pekee ni chakula na kinywaji tosha kwa mtoto mchanga kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha yake.

Anastazia, ambaye ni Meneja Programu katika Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), mtoto wake wa kwanza, Raphana ametimiza miezi mitatu.

Anasema aliamua kukamua maziwa na kuyaweka kwenye pakiti, baada ya kujifunza kutoka katika mitandao ya kijamii wakati akijiandaa kumpokea mtoto wake.

MCL
Mumewe anafaidi
 
...Hajasema kwa Siku Mkuu. Amesema amekusanya hizo Lita 40 kwa Miezi Miwili toka aanze kuyakamua na kuyaweka kwenye pakti ndani ya friji kwa maana kwamba anapotaka kumpa mwanawe ni kiasi cha kuyapasha moto tu!!....
Got you I thought per day
 
Hata mie sijui ila ndoo yote hio ya maziwa ya nini si angeacha mtoto anyonye direct kuliko kukesha anampa ya chupa kisa amekamua mengi. Kisingizio kisije mchana akiwa kazini
Bora kumyonyesha tu direct hii kamua kamua inahitaji high personal hygiene kuna mtu niliona ana kamua na kumpashia maziwa mtoto ukuaji wake ukawa haueleweki sana.nikianza nyonyesha nitatafta nyumba karibu na ofisini niwe naenda kunyonyesha mara kwa mara hii kamua kamua itakuwa last option when other means zikifeli maana kumwachia dada wa kazi atakosa umakini.
 
Mama aliekamua lita 40 za maziwa yake huyu hapa.
mothersduty~p~CRiiDYdrFDv~2.jpg
mothersduty~p~CRiiDYdrFDv~1.jpg


Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Nasikia maziwa ya mama ni mazuri uyatumiapo kuondoa hangover,

Wanaopata changamoto ya hangover wanaweza nunua hizo pakiti wakatuthibitishia ka ni kweli, mjini kila kitu biashara
 
Anakamua na kuyaweka pembeni kwani yakibaki kwenye ziwa lake yataharibika? Fujo tu kama Miguna wa Miguna.
 
Kwa ukoo wetu mtoto akitimizia mwezi there is no way maziwa ya mama pekee yanamtosha.

Kinachofuata ni uji mwepesi na maziwa ya mama
 
Back
Top Bottom