Mfahamu adui yako halisi aliyekuumiza na kukujeruhi moyo wako

Showio

JF-Expert Member
May 16, 2019
255
481
"Watu wengi wanapiganana kivuli badala kupigana na adui halisi wanapokuwa wameraruliwa mioyo yao "
Maandiko matakatifu yanasema;

Waefeso 6

"11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."

Kama unafanyiwa jambo na linaifanya roho yako kuvuja damu au kuumizwa ,basi ujue hiyo ni vita ya kiroho.

'Ni kweli aliyekuumiza Ni Mwandamu mwenzako, tena mwenye mwili wa damu na nyama. Sasa haina maana upigane naye katika mwili wa damu na nyama, maana maandiko yanatuambia vita vyetu si vya damuna nyama , bali ni juu ya (falme na mamlaka, wakuu wa giza,jeshi la pepo wabaya )'

Hii ina maana kuwa mwanadamu hutumiwa tu na; (falme na mamlaka, wakuu wa giza, jeshi la pepo wabaya kwenye ulimwengu wa roho ).

Aliyekuumiza akiingiwa na hizo roho anakuwa na roho inayoitwa "roho ya kuhumiza ".Hiyo roho ikimwingia ndipo inapomsukuma kufanya jambo la kukumiza wewe. Hapo shetani anakuwa amevaa mwili wake kukuumiza wewe. Maana pepo au Wakuu wa giza au Falme Ni roho za shetani.

Sasa kwa juu utaona Ni "fulani " Kumbe Ni shetani kavaa roho ya kuumiza ndani "jambo ulilotendewa la kuumiza ".

Yesu alimwambia Petro ,"rudi nyuma yangu shetani " Mathayo 16:23 ..SI kwamba Petro alikuwa Ni shetani, Hapana, Bali Yesu kwa macho ya rohoni alimwona jinsi shetani alivyoingia ndani ya Petro na kujaribu kutaka kumpa ushauri ambao Yesu angausikiliza basi "Yesu asingekwenda msalabani" Jiulize kama Yesu asingekwenda msalabani nini kingetokea ?Usingekuwa na wokovu.

Mfano 1
Ukisoma habari za Ayubu, aliyeleta majipu Na kuwaua wanyama wake na watoto wake alikuwa ni shetani. Ayubu aliumia sana. Soma Hiyo habari. Lakini kwa juu utaona shetani aliwaingia Washeba na Wakaldayo wakamvamia Ayubu (Ayubu 1:15,17.
Lakini Ukisoma Hiyo habari utagundua (Ayubu 1:10-11) ,Utaona Shetani ndiye anaunyoosha mkono wake kugusa maisha ya Ayubu na watoto wake na wanyama wake.

Usipigane na Mtu; Kaa Magotini pambana na roho ya kuumiza.
Au umesahau Yesu alisema, (Mwombee adui yako ), Yesu , alijua unayemwona ni adui ukimwombea, ile roho ya kuumiza inayomtumia inamwachia maana maombi yako kwake yanakwenda kama makaa ya moto juu ya hiyo roho ya kuumiza na kumwachilia huyo mtu unayemwona ni adui .


mwanadamu ni kivuli tu, shetani ndiye adui halisi akiitumia "roho yake ya kuumiza "

(Mwombee adui yako na akiwa na njaa mpe chakula maana utampalia makaa ya moto kichwani. Mithali 25 :21-22)
 
Amina sana mjoli wa Bwana.

Huyo jamaa a.k.a devil ana ugomvi na mimi asee yaani lile andiko UFUNUO 12:17 huwa naliona linavyonionyesha uhalisia wa hii kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom