Mfahamu abiria aliyesafiri peke yake katika ndege ya kuwabeba abiria 360

Nikiri wazi kabisa kwa nia njema kabisa kipengere cha hesabu nipo shallow! wee shusha nondo tuu!
Hahahaha asante mkuu kwa kunipa go ahead, kwanza kabisa mkuu ndege za boing 777 zinatumia mafuta aina ya kerosene ( aviation kerosene) ni tofaut na kerosene ya kawaida.

So twende kwa mada husika. Aviation kerosene zinatofautiana density kulingana na engine yake but mara nyingi boing 777 hutumia aviation kerosene yenye density ya 0.85kg/l.

Na aviation kerosene katika soko la mwezi huu ilikua $1.6 /gallon na 1gallon=3.7ltrs,so

Kwa hiyo kama ndege ilitumia tani 25, basi ni sawa na kilo 25000. Ambazo ni sawa na lita 29411.76470, ambayo ni sawa na gallons 7949.12.

So ni sawa na $12718.6
Hizo gharama ni za mafuta tu, but kutoa ndege safar moja kuna gharama zingine kama za attendants, engineers,pilots, refueling cost na vingine vingi.
 
Haji manara pia aliwahi kupanda ndege peke yake kipindi hicho hicho cha korona ila hakuchukua video na hapo ndipo alipobugi. Ni jambo la kumshukuru Mungu kwakweli lasivyo tusingepumua dar nzima ..
 
Haji manara pia aliwahi kupanda ndege peke yake kipindi hicho hicho cha korona ila hakuchukua video na hapo ndipo alipobugi ..
 
Kumbe ni Emirates, wale hawaendi hasara, sio leo! 🤣 🤣 🤣 Alafu safari yenyewe ni fupi, Mumbai ni hapo hapo tu. Unafkiri ingekuwa to SA wangethubutu? 😂 😂 😂
 
Hapo walipata hasara ya faida...yaani kama walitegemea kupata faida buku....basi walipata 250
 
Ndege kutoka Mumbai hadi Dubai ilipaa na kuanza safari ikiwa na abiria mmoja pekee. Mtu aliyesafiri peke yake katika ndege ya kuwabeba abiria 360.

Wanaotokewa na tukio kama hili, huchukuliwa kuwa 'bahati nzuri'.

Mahali: Uwanja wa ndege wa Mumbai

Saa: Kumi kamili

Abiria: Bhavesh Zaveri

Bhavesh, ambaye ni mkazi wa Dubai, alitembelea mji wa Mumbai wiki ya kwanza ya Mei kibiashara. Alikuwa ameshakata tiketi yake ya kurejea siku 10 kabla.

Na kama kawaida yake, huwa anasafiri katika sehemu ya tabaka la wafanyabiashara.

Lakini kwasababu ya corona, ni wazi kwamba ndege hiyo haingekuwa na watu wengi na akaamua kukata tiketi katika sehemu ya watu wa kawaida.

Mei 19 safari yake ilikuwa ni saa kumi na nusu asubuhi. Aliwasili uwanja wa ndege usiku wa manane kulingana na sheria za kimataifa. Wakati anafanyiwa ukaguzi kuingia ndani ndipo alipofahamu kuwa abiria ni yeye peke yake.

Kwa muda, hakukubaliana na hilo lakini baada ya muda akajua kuwa huo ndio ukweli wa mambo ulivyo.

Wamekuwa Dubai kwa kipindi cha miaka 20 na amekuwa akisafiri kutoka Mumbai - Dubai mara nyingi tu lakini hii ndio mara ya kwanza amekutana na tukio la namna hii, kusafiri peke yake.

Akizungumza na BBC huko Dubai, amesema: "Sio kawaida yangu kujirekodi video, lakini safari hii nimejipiga picha na kujirekodi karibu safari yote kwa kutumia simu yangu ya mkononi.

"Nataka safari hii iwe katika kumbukumbu zangu milele. Ilikuwa tajriba ya kipekee katika ndege yoyote ile ya Emirates. Yaani haijawahi kutokea abiria anasafiri peke yake katika ndege yote. Baada tu ya kupanda ndege, wahudumu wote wa ndege walinipokea kwa kunipigia makofi. Rubani alitoka kwenye chumba chake cha kuendesha ndege na kuja kunisalimia. Akanitania."

Gharama
Ndege ya shirika la Emirates ndio ambayo Bhavesh alikuwa anasafiri nayo kutoka Mumbai hadi Dubai, iliyokuwa inabeba watu 360 aina ya Boeing 777.

Sasa pengine unajiuliza, ndege iligharamika kiasi gani?

Mtaalamu wa ndege Rajesh Handa amesema, "Safari ya ndege kutoka Mumbai hadi Dubai inachukua saa moja na nusu. Safari hiyo ingekuwa imegharimu tani 25 za mafuta na gharama yake ni ya juu.

Na bila shaka gharama yake ilikuwa ya juu hasa kwa usafiri wa mtu mmoja.

Ni swali ambalo pia Bhavesh aliwauliza wahudumu wa ndege.

Lakini Bhavesh alikuwa na haya ya kusema:

"Nilifikiria uwanja wa ndege hautakuwa na watu wengi. Abiria kutoka India sasa hivi wamepigwa marufuku UAE kwasababu ya janga la virusi vya Corona. Wanaoruhusiwa ni wenye Viza maalum, wanasiasa na raia wa UAE kusafiri kutoka India hadi Dubai.

Makundi hayo matatu pekee ya abiria ndio wanaoweza kusafiri kuingia Dubai kwa ndege za kibiashara. Ndege ilikuwa imetua Mumbai. Na ingerejea bila abiria. Nilikuwa nimekata tiketi kabla kwahiyo niliruhusiwa kusafiri kwa ndege hii."

Bhavesh ni mfanyabiashara wa madini ya almasi ikiwa ni taaluma yake.
Ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya StarJames Group.
Anaishi Dubai na mke wake na watoto wao wawili.

Video aliyokuwa amepiga inamuonesha akisafiri peke yake katika ndege ya abiria 360 ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huko Mumbai na Dubai.

Anaelezea safari yote kama ya kupendeza. Kulingana na yeye, fursa kama hiyo inakuja kwa bahati. Pesa haiwezi kununua furaha.

"Ndege niliyokuwa nasafiria ilikuwa inatoka asubuhi sana kwahiyo, siku ile sikulala vizuri. Sikutaka kulala nikiwa safarini lakini ilifika wakati sikujua kulitokea nini, nikaibwa na usingizi. Nilipofika nyumbani, nilieleza familia yangu tajriba niliyopita "

View attachment 1800097
Hili nalo ni janga inatakiwa Kabula halijatokea tanzania kwa njiwa wetu kutoka Chato - Dar es Salaam lijadiliwe bungeni
 
Back
Top Bottom