Mfadhaiko, namna ya kukabiliana na hasira na akili sumbufu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,798
34,170
Mfadhaiko

Mfadhaiko ni nini? Ni hali inayotokana na shida, matatizo au dhiki. Jamii, pesa, kazi, na shule ndio chanzo kikubwa cha mfadhaiko. Watu wanapokumbana na hali ya mfadhaiko huleta shida za kukabiliana na hasira.
Ishara ni zipi?

Mtembelee daktari kila mara. Ishara zifuatazo zaweza sababishwa na kitu kingine. Magonjwa yaweza changia kwa mfadhaiko wako:

  • Kuumwa na kichwa na mgongo
  • Kukosa usingizi
  • Kuhisi njaa na kukosa matumaini
  • Kutokuwa mmakinifu
  • Kulia
  • Kujificha kutoka kwa watu
  • Ulcers na kusokotwa na tumbo
  • Vipele
  • Shinikizo la damu ugonjwa wa moyo na pigo.
Utaikinga vipi na kutibu

  • Fanya mazoezi ya kila siku dakika 20-30, tembea, kimbia, au tembia kidogo wakati wa mapumziko.
  • Sikiza muziki muororo na ufunge macho kwa dakika 10-20 vuta pumzi.
  • Zungumza na mtu yeyote auandika chini hisia zako
  • Kula vya kula bora pia husaidia kumliwaza mtu
  • Jifunze kusema LA. Usifanye mambo mengi kuliko uwezo wako.
 
Dhuluma ya kujamiiana

Ni hali ya kujamiiana ambayo inatokea bila hiari ya mtu. Una haki ya kusema ‘hapana'. Wanaodhulumu ni pamoja na watu wasiowajua, marafiki au jamaa. Hali ambapo watu wa familia moja huonana kimapenzi huitwa ‘najisi'.

Dhuluma hizi ni pamoja na kunajisi, kushikashika, kumtesa mtu kwa maneno makali, hata kumlazimisha kuona picha au filamu chafu chafu. Wakati mwingine unakubali tu kwa sababu umeogopa au unaona maisha yako yakiwa hatarini.

Unaweza kukubali na pia uwe na mhasiriwa na dhulumwa za kingono.

Hakuna mtu aliye na haki ya kukushika, kuongea nawe maneno yanayohusu ngono, kukufanya utazame filamu chafu chafu za ngono au picha; ama hata kushiriki ngono ya mdomoni, utuputupu wa nyuma au ya utupu wa mbele iwapo hautaki. Kuna makundi yanayoweza kukusaidia iwapo umenajisiwa yatahakikisha kuwa haki zako zimetunzwa.


Unapaswa kufanya nini iwapo umenajisiwa au kudhulumiwa kimapenzi?
Ukidhulumiwa kimapenzi, mpigie simu polisi au mtu yeyote wa kifamilia unayeweza kumwamini. Askari hawatakulazimisha kuchukua hatua lakini watakusaidia.

Usioge ama kusugua meno. Andika chini maelezo ya kila namna uliyodhulumiwa na aliyekudhulumu. Inaweza kuwa vigumu lakini ni muhimu na inahitajika kwa ushahidi.

Hakikisha kuwa polisi wanakupeleka kwanza kwenye kliniki, hospitali au kwa daktari wa upasuaji; omba kifuko cha walionajisiwa na ukaguliwe iwapo umeambukizwa magonjwa ya zinaa au u mja mzito. Ni muhimu upewe dawa za kuzuia ugonjwa wa ukimwi kwa mda was masaa 72. Iwapo ulisumishwa ambia daktari achukue mkojo wako aupime.

Tafuta mahali pa faragha, mbali na aliyekudhulumu au aliyekushambulia. Muombe rafiki mwaminifu au jamaa akusaidie kwa kukuunga mkono hata akupatie mahali pa kuishi.

Kumbuka kuwa haupaswi kulaumiwa kwa yaliyokupata. Kupona kisaikologia na kimwili huhitaji muda. Nasaha bora itakufaa zaidi.

Watu waliodhulumiwa huonyesha dalili gani?


  • Kuchanganyikiwa
  • Kushindwa kulala vizuri
  • Kuumwa na kichwa
  • Uoga ama wasiwasi
  • Kuchukilia kwa uzito zaidi jambo hata likiwa jepesi
  • Majonzi na huzuni kuu
  • Hasira
  • Ndoto mbaya ama kukumbuka yaliyopita
  • Kushindwa kabisa kuona roho au hata hisia za kimapenzi
 
Dhuluma za kinyumbani


Hizi ni dhuluma zinazoendelezwa na mme mtu au mke mtu wa kitambo, mpenzi wa kike au kiume na mtu mnayeishi naye. Mara nyingi wanawake na watoto ndio wanaotendewa dhuluma hizi. Hata hivyo pia wanaume wanaweza kutendewa dhuluma hizi.

Wanaodhulumu ni pamoja na mpenzi miliyetalikwana naye, wazazi wako, mlezi wako, mtoto wako au mtu yeyote ambaye mumewahi kuishi naye. (Hata kama mliyejumuika pamoja kwenye tafrija, mkajamiiana ama mmepata naye mtoto).

Dhuluma hizi hudhuru maisha ya anayedhulumiwa na watoto wake. Huweza kuishia kwa mtu kupelekwa hospitalini kutibiwa, kufungwa jela maisha, ama hata kusababisha kifo. Watoto ambao wamekua wakiona dhuluma hizi na watu ambao wamedhulumiwa wakiwa wazima, hata nao watawadhulumu wengine. Wanawake wanaovumilia dhuluma kwa muda mrefu mara nyingi huuawa na wapenzi (waume) wao kwa hivyo ni muhimu wapate usaidizi na wajiondoe katika mazingira haya.

Kuna msaada wakukusaidia kukabiliana na uhusiano wa kidhuluma unaotolewa bure.
 
Majonzi na huzuni


Majonzi na huzuni ni nini?
Ni ugonjwa unaohusisha mwili, kupanda na kishuka kwa hisia za hasira na mawazo. Ni hali ambayo huwezi kuiondosha mbali kwani unashindwa kujizuia na hizi hisia.

Hakuna sababu moja kunayosababisha majonzi na huzuni mwingi. Hali hii hurithishwa katika historia ya familia. Hata wale ambao hii hali haijawahi kuonekana katika familia zao hujikuta nayo, taabu na dhiki za kupambana na maisha, mpenzi ama ugonjwa mkali. Watu wengine, hata madaktari, hudhani kuwa ni hali inayokumba tu watu wazee pekee la hasha.

Dalili

  • Kuhuzunika kila mara na kujiona bure
  • Kukosa shughuli na tama katika vitendo ulivyokuwa umenipenda hapo awali
  • Kuhisi kuchukizwa hata kwa jambo dogo
  • Kulia sana
  • Kuona hufai na kujihukumu huku ukijihurumia
  • Kulala sana ama hata kutolala kabisa
  • Kula sana au hata kuishindwa kabisa kula.
  • Kupata shida katika kufanya maamuzi au kufuatilia jambo
  • Kuwa na fikira za kutaka kujitia kitanzi au kufa.
  • Kulewa na kutumia dawa za kulevya.
Unaijuaje?
Ukihisi mojawapo ya dalili hizi kwa zaidi ya majuma mawili, ni muhimu upate usaidizi na kitaalamu. Huzuni ba majonzi huweza kutokea iwapo mtu ana shida ya kiafya, hasa kuna ugonjwa wa Sukari mwilini, ugonjwa wa moyo, kupata kipigo. Matibabu yanaweza kusababisha huzuni na majonzi pia. Ugonjwa wa kiakili na matumizi ya mihadarati, kupata nasaha bora na matibabu husaidia.

Unatibuje?
Iwapo kemikali katika ubongo wako hazitoshani unaweza kupata majonzi na huzuni kwa watu wengine, matibabu husaidia kwa wengine, nasaha bora huwasaidia. Kupata matibabu pamoja na nasaha bora huweza kutibu. Iwapo dawa au nasaha haisaidii endelea kujaribu hadi pale ambapo utapata tiba kamili. Watu tu baada ya majuma machache.
 
Kuthibiti hasira

Hasira ni nini?
Ni hisia ambazo huanza polepole na kupanda kiasi cha mtu kushindwa kujizuia na kubadilika mpigo wako wa moyo kicho chochote kuwameza kusababisha hasira kuanzia kwa kusubiri kwenye mlolongo wa msongamano wa magari hadi kwa kutoelewa na kubaya.

Ni nini baadhi ya dalili?


  • Kushambulia watu wa maneno makali
  • Kuropokwa kwa sauti
  • Kupigana
  • Kuharibu vitu

Unazuiaje na kutibu hali hii?


  • Pumua hewa nje na ndani kwa kina.
  • Jaribu kulete mzaha katika hilo jambo
  • Fikiria kuhusu mahali ambapo patakufanya utulie na upumzike
  • Zungumzia na mtu ambaye amekukasirisha kuliko kukaripia
  • Kaa mbali na hali ambapo unajua zitakufanya ukasirike
  • Pata nasaha
 
Back
Top Bottom