Mfadhaiko, namna ya kukabiliana na hasira na akili sumbufu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfadhaiko, namna ya kukabiliana na hasira na akili sumbufu

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Apr 23, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Wengi wetu hukumbana na shida za kikazi na kinyumbani, hii huleta mfadhaiko wa akili ambalo ni jambo la kiafya.
  Jifahamishe jinsi ya kugundua ikiwa una shida na jinsi ya kutibu, kulipia gharama za matibabu ni ghali mno lakini Beehive ipo hapa kukusaidia.
  Kuna mfadhaiko mzuri na mbaya.Mfadhaiko huleta shida za kiafya na kuharibu uhusiano na jamiina marafiki. Kuna njia za kukabiliana na mfadhaiko huu.

  Mfadhaiko

  Mfadhaiko ni nini? Ni hali inayotokana na shida, matatizo au dhiki. Jamii, pesa, kazi, na shule ndio chanzo kikubwa cha mfadhaiko. Watu wanapokumbana na hali ya mfadhaiko huleta shida za kukabiliana na hasira.
  Ishara ni zipi?

  Mtembelee daktari kila mara. Ishara zifuatazo zaweza sababishwa na kitu kingine. Magonjwa yaweza changia kwa mfadhaiko wako:

  • Kuumwa na kichwa na mgongo
  • Kukosa usingizi
  • Kuhisi njaa na kukosa matumaini
  • Kutokuwa mmakinifu
  • Kulia
  • Kujificha kutoka kwa watu
  • Ulcers na kusokotwa na tumbo
  • Vipele
  • Shinikizo la damu ugonjwa wa moyo na pigo.
  Utaikinga vipi na kutibu

  • Fanya mazoezi ya kila siku dakika 20-30, tembea, kimbia, au tembia kidogo wakati wa mapumziko.
  • Sikiza muziki muororo na ufunge macho kwa dakika 10-20 vuta pumzi.
  • Zungumza na mtu yeyote auandika chini hisia zako
  • Kula vya kula bora pia husaidia kumliwaza mtu
  • Jifunze kusema LA. Usifanye mambo mengi kuliko uwezo wako.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Wanawake wengi hujikuta katika hali ambayo wamedhulumiwa; kihisia, numbani, na kijinsia. Usione haya ukijikuta katika hali hii kwa maana kuna watu wengi sana wanaopitia hali moja sawa na yako. Ukipata usaidizi mapema ni vizuri. Bonyeza kwenye vivukio vifuatavyo ili upate maelezo ziaidi.
  Dhuluma ya kujamiiana Ni hali ya kujamiiana ambayo inatokea bila hiari ya mtu. Una haki ya kusema ‘hapana’. Wanaodhulumu ni pamoja na watu wasiowajua, marafiki au jamaa. Hali ambapo watu wa familia moja huonana kimapenzi huitwa ‘najisi’.

  Dhuluma hizi ni pamoja na kunajisi, kushikashika, kumtesa mtu kwa maneno makali, hata kumlazimisha kuona picha au filamu chafu chafu. Wakati mwingine unakubali tu kwa sababu umeogopa au unaona maisha yako yakiwa hatarini.

  Unaweza kukubali na pia uwe na mhasiriwa na dhulumwa za kingono.

  Hakuna mtu aliye na haki ya kukushika, kuongea nawe maneno yanayohusu ngono, kukufanya utazame filamu chafu chafu za ngono au picha; ama hata kushiriki ngono ya mdomoni, utuputupu wa nyuma au ya utupu wa mbele iwapo hautaki. Kuna makundi yanayoweza kukusaidia iwapo umenajisiwa yatahakikisha kuwa haki zako zimetunzwa.


  Unapaswa kufanya nini iwapo umenajisiwa au kudhulumiwa kimapenzi?
  Ukidhulumiwa kimapenzi, mpigie simu polisi au mtu yeyote wa kifamilia unayeweza kumwamini. Askari hawatakulazimisha kuchukua hatua lakini watakusaidia.

  Usioge ama kusugua meno. Andika chini maelezo ya kila namna uliyodhulumiwa na aliyekudhulumu. Inaweza kuwa vigumu lakini ni muhimu na inahitajika kwa ushahidi.

  Hakikisha kuwa polisi wanakupeleka kwanza kwenye kliniki, hospitali au kwa daktari wa upasuaji; omba kifuko cha walionajisiwa na ukaguliwe iwapo umeambukizwa magonjwa ya zinaa au u mja mzito. Ni muhimu upewe dawa za kuzuia ugonjwa wa ukimwi kwa mda was masaa 72. Iwapo ulisumishwa ambia daktari achukue mkojo wako aupime.

  Tafuta mahali pa faragha, mbali na aliyekudhulumu au aliyekushambulia. Muombe rafiki mwaminifu au jamaa akusaidie kwa kukuunga mkono hata akupatie mahali pa kuishi.

  Kumbuka kuwa haupaswi kulaumiwa kwa yaliyokupata. Kupona kisaikologia na kimwili huhitaji muda. Nasaha bora itakufaa zaidi.

  Watu waliodhulumiwa huonyesha dalili gani?
  • Kuchanganyikiwa
  • Kushindwa kulala vizuri
  • Kuumwa na kichwa
  • Uoga ama wasiwasi
  • Kuchukilia kwa uzito zaidi jambo hata likiwa jepesi
  • Majonzi na huzuni kuu
  • Hasira
  • Ndoto mbaya ama kukumbuka yaliyopita
  • Kushindwa kabisa kuona roho au hata hisia za kimapenzi


   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Dhuluma za kinyumbani Hizi ni dhuluma zinazoendelezwa na mme mtu au mke mtu wa kitambo, mpenzi wa **** au kiume na mtu mnayeishi naye. Mara nyingi wanawake na watoto ndio wanaotendewa dhuluma hizi. Hata hivyo pia wanaume wanaweza kutendewa dhuluma hizi.

  Wanaodhulumu ni pamoja na mpenzi miliyetalikwana naye, wazazi wako, mlezi wako, mtoto wako au mtu yeyote ambaye mumewahi kuishi naye. (Hata kama mliyejumuika pamoja kwenye tafrija, mkajamiiana ama mmepata naye mtoto).

  Dhuluma hizi hudhuru maisha ya anayedhulumiwa na watoto wake. Huweza kuishia kwa mtu kupelekwa hospitalini kutibiwa, kufungwa jela maisha, ama hata kusababisha kifo. Watoto ambao wamekua wakiona dhuluma hizi na watu ambao wamedhulumiwa wakiwa wazima, hata nao watawadhulumu wengine. Wanawake wanaovumilia dhuluma kwa muda mrefu mara nyingi huuawa na wapenzi (waume) wao kwa hivyo ni muhimu wapate usaidizi na wajiondoe katika mazingira haya.

  Kuna msaada wakukusaidia kukabiliana na uhusiano wa kidhuluma unaotolewa bure.
   
 4. princess ariana

  princess ariana JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2016
  Joined: Aug 19, 2016
  Messages: 4,446
  Likes Received: 5,908
  Trophy Points: 280
  Je kama inakupata kutokana na sababu tofauti?
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Inategemea kama huna hizo sababu utakuwa una mapepo wachafu Mashetani wabaya ndio wanao kusumbuwa mwilini mwako.
   
 6. princess ariana

  princess ariana JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2016
  Joined: Aug 19, 2016
  Messages: 4,446
  Likes Received: 5,908
  Trophy Points: 280
  kwahiyo nikaombewe?
   
Loading...