Meza huru: Wanasheria tujadili kuhusu sehemu ya "V" ya sheria ya huduma za habari Na. 12/2016

sagaciR

JF-Expert Member
Jun 17, 2017
644
875
Habari za mchana wana JF

UTANGULIZI:
Wakati tukijiandaa na uchaguzi wa Rais wa TLS siku za usomi, naomba kujadili kuhusu sehemu ya "V" (i.e kifungu cha 35-41) ya sheria ya huduma za habari Na. 12/2016.

Jana, Februari, 29, 2019 nimemsikia wakili msomi L. Manyama kuputia ukurusa wa Millarday ayo kuwa kosa la kudhalilisha kwa mujibu wa sheria tajwa hapa, faini yake ni shilingi kati ya 5mil - 10mil au jela miaka 3-5 au vyote kwa pamoja hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 51 cha sheria husika. Na kwamba, kifungu cha 35 (3) kinaweka wazi kuwa mashtaka juu ya sehemu hii ni hadi yapate kibali kutoka kwa DPP.

HOJA:
(i) Je, kisheria udhalilishaji chini ya sehemu ya 5 ("V") ya sheria hiyo ni kosa la jinai ama madai?

(ii) Je, ni halali Kisheria DPP kutoa idhini kwa mujibu wa kifungu cha 35(3) cha sheria hiyo?

(iii) Je, wakili Manyama amejielekeza sahihi (properly directed) kuwa kifungu cha 51 kinatumika pia kwny sehemu ya V ya sheria hii?

MAONI YANGU:

1. Je, kisheria udhalilishaji chini ya sehemu ya 5 ("V") ya sheria hiyo ni kosa la jinai ama madai?.

Udhalilishaji (Defamation) ni dhana ambayo hasa tumeiiga kutoka nchi za nje (Uingereza) ambako huko kwao sio kosa la jinai bali ni madai na mtu aliyedhalilishwa hulipwa fidia ya kifuta jasho (yaan kisheria GENERAL DAMAGES). Kwenye kesi ya "Sim v Stretch [1936] 2 All ER 1237, 1240," Jaji ATKIN alitoa maana ya udhalilishaji (defamation) kwa maneno yafuatayo:-

"A defamatory statement is one which injures the reputation of another by exposing him to hatred, contempt, or ridicule, or which tends to lower him in the esteem of right-thinking members of society"

Kwamba, Nchini Uingereza na India wao marehemu huwa hadhalilishwi, yaani huwezi kumshushia heshima kwny jamii wakti yeye sio sehemu ya jamii na pia haathiriki (no injury) kisheria kuna kanuni (Latin maxim) inaitwa "actio personalis moritur cum persona"

Kwa mujibu wa kanuni za jaji mkuu wa Tanzania G.N 108/2019 (nampongeza sana Mhe. CJ kwa kutunga kanuni haraka ndani ya miaka 3 tu tangu sheria hii itungwe HONGERA SANA Mhe. Jaji mkuu kwa uchapa kazi wako mzuri) zinaelekeza kuwa mwenendo unaotumika kushitaki chini ya sehem ya V ya sheria mama ni mwenendo wa madai (CIVIL PROCEDURE CODE CAP 33 R.E 2002) na sio mwenendo wa jina. Na uwasilishaji wa mashtaka ni kwa njia ya PETITION, (kama ilivyoelekezwa Kwenye jedali, FOMU DP) na sio CHARGE SHEET/INFORMATION, kama ilivyo kwenye kesi za jinai.

Mashitaka katika sehemu hii yataangalia uwezo wa mahakama kusikiliza shauri lililoletwa mbele yake kwa kuangalia kiasi cha fedha kinachodaiwa (i.e Pecuniary jurisdiction). Yaan
1-30,000,000 Mahakama ya Mwanzo
30,000,001-300,000,000, mahakama ya wilaya na ya Hakimu mkazi na zaidi ya 300,000,000 Mahakama kuu. Wakati kwny jinai hatuna pecuniary jurisdiction. Lakini kwa kuwa Mahakama ya mwanzo haina mamlaka ya kusikiliza madai nje ya madai ya kimila na kiislamu basi mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri linalotoka sehemu ya V ya sheria Na. 12/2016 (rejea kanuni ya 2 ya kanuni za Mhe. Jaji mkuu GN 108/2019.

Hivyo basi kwa maoni yangu, kumbe kosa chini ya sehemi ya V ya sheria Na. 12/2016 sio kosa la jinai bali ni madai.

2. Je, ni halali Kisheria DPP kutoa idhini kwa mujibu wa kifungu cha 35(3) cha sheria hiyo?

Kwamba, DPP anatambulika kisheria na kikatiba chini ya Ibara ya 59B ya katiba ya JMT 1977. Ibara hiyo inatamka kuwa atahusika na masuala ya makosa ya jinai kesi za madai hazikutajwa. Hivyo ni wazi kabsa DPP anahusika na jinai pekee na si madai.

Ngoja ibara ya 59B iongee yenyewe

"59B.-(1) N/A
(2) The Director of Public Prosecutions shall have powers to institute, prosecute and supervise all criminal prosecutions in the country.
(3) N/A
(4) N/A
(5) The Director of Public Prosecutions shall exercise his powers as may be prescribed by any law enacted or to be enacted by the Parliament."

Kwa maoni yangu, DPP kutoa kibali cha kushitaki kosa la madai ni kinyume na ibara ya 59B ya katiba.


3. Je, wakili Manyama amejielekeza sahihi (properly directed) kuwa kifungu cha 51 kinatumika pia kwny sehemu ya V ya sheria hii?

Kwamba, wakili msomi manyama amenukuliwa akisema kosa hili adhabu yake ipo chini ya kifungu cha 51 cha sheria husika (KWA HESHIMA KUBWA NAPINGANA NAYE KWA HILO) kifungu cha 51 kinahusu mtu wa tatu ambaye atasambaza udhalilishaji huo (i.e A defames B to C,D,E, etc also F disseminates the same defamatory words to G,H,I,J etc) huyo (F) ndo atawajibishwa na kifungu cha 51 siyo A.

Sehemu ya V ya sheria hiyo iliwekewa utaratibu tofauti na sehemu nyingine na ndiyo maana utaratibu wa sehemu hyo akapewa madaraka Jaji mkuu kuweka utaratibu utakaoharakisha mashauri ya sehemu hiyo tu. Fidia italipwa kulingana na udhalilishaji ulivyofanyika na kuelea. Mahakama ya rufani ya Tanzania katika kesi ya Prof. Lipumba vs Zuberi J. Mzee (2004) TLR 381 iliweka mwongozo wa kukadiria fidia ya mtu aliyedhalilishwa. Kifungu cha 51 hakitumiki kwny sehemu hii ya sheria.

KWA KUHITIMISHA, NAHITIMISHA KUWA:-
Hoja Na. 1 naijibu kuwa ni kosa la madai.
Hoja Na. 2 naijibu kuwa siyo halali, na
Hoja Na. 3 naijibu kwa hakuwa sahihi.


===== Karibuni kwa maoni ======
MUCH OBLIGED YOUR HONS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom