Meya wa Ubungo kufungua kesi ya jinai dhidi ya Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Meya wa Ubungo Mh. Boniface Jacob anakusudia kufungua shauri mahakamani la kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuonesha vyeti vyake ili kuondoa utata uliojitokeza hivi karibuni dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa.

Kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa Jumatato ijayo ya tarehe 20/03/2017.

Stay tuned.

---------
Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki.

Jacob pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora. Amesema kesi hiyo ambayo itaongozwa na mawakili Tundu Lissu pamoja na Peter Kibatara.

“Tunachosubiri ni wanasheria wamalize mchakato wa uchaguzi Chama cha Wanasheria Tanganyika (TSL) na mara watakaporejea kutoka Arusha tutakwenda mahakamani” amesema Jacob.

Chanzo: Mwananchi
 
Ndugu Jacob kumbuka wahenga walinena "ukitaka kuanzia mbio sharti uagane na nyonga",

Je umetimiza sharti hilo kabla ya kuanza kupiga jalamba??

Kumbuka kuwa "usianzishe ugomvi wakati unaishi kwenye Nyumba ya vioo".

CC: Mwenyekiti wa ufipa....hivi alihitimu Yale masomo yake ya Q.T aliyotangaza kwenda kusomea ughaibuni..??
 
Mayor wa Ubungo Mh. Borniface Jacob anakusudia kufungua shauri mahakamani la kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuonesha vyeti vyake ili kuondoa utata uliojitokeza hivi karibuni dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa. Kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa jumatato ijayo ya tar 20/03/2017.

Stay tuned.
Amekosa kazi ya kufanya?? Namshauri ajikite kwenye kuwaongoza wapiga kura wake kujiletea maendeleo! Mwaka 2020 siyo mbali!!!
 
Mayor wa Ubungo Mh. Borniface Jacob anakusudia kufungua shauri mahakamani la kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuonesha vyeti vyake ili kuondoa utata uliojitokeza hivi karibuni dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa. Kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa jumatato ijayo ya tar 20/03/2017.

Stay tuned.
Lkn, nikidhani, kila mtumishi, ana wajibu wa kuwakilisha vyeti, na madodoso yake yote ya kitaaluma, kwa mamlaka zilizomuajiri, na si vinginevyo....
Kama Kuna uhakika kuwa "mtuhumiwa", kagushi, taratibu kisheria, si kumtaka mtuhumiwa atoe vyeti vyake, bali ni kwa mtuhumu kutoa ushahidi wa kuthibitisha tuhuma zake..
..."wanasiasa wetu, na wafuasi wenu, mbona hili jambo ni rahisi sana kulipatia ufumbuzi?"
 
Mayor wa Ubungo Mh. Borniface Jacob anakusudia kufungua shauri mahakamani la kumtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuonesha vyeti vyake ili kuondoa utata uliojitokeza hivi karibuni dhidi ya kiongozi huyo wa mkoa. Kesi hiyo inatarajiwa kufunguliwa jumatato ijayo ya tar 20/03/2017.

Stay tuned.

Ni jambo jema, pale Viongozi, wanapohitaji kujiridhisha ktk certificates za Elimu kwa wenzao.
 
Ndugu Jacob kumbuka wahenga walinena "ukitaka kuanzia mbio sharti uagane na nyonga",

Je umetimiza sharti hilo kabla ya kuanza kupiga jalamba??

Kumbuka kuwa "usianzishe ugomvi wakati unaishi kwenye Nyumba ya vioo".

CC: Mwenyekiti wa ufipa....hivi alihitimu Yale masomo yake ya Q.T aliyotangaza kwenda kusomea ughaibuni..??
M/kiti wetu vyeti vyake vipo & hajawahi kutumia jina bandia.

Acha justification za kipuuzi.
 
Hivi akili zenu huwa ni za kuvukia barabara ama!!???... MTU anapeleka shauri mahakamani kwa MTU alievunja sheria " Penal Codes" za Tanzania unamuona hafai... Kweli naanza kuamini mnyama pekee kumtawala kirahisi duniani ni mtanzania...

Hili suala la forgery lingekuwa Kenya ungeona na kushuhudia utofauti wa vichwa vya wakenya kama binaadamu na vichwa vya watanzania kama misukule isiyojielewa kama wewe
 
M/kiti wetu vyeti vyake vipo & hajawahi kutumia jina bandia.

Acha justification za kipuuzi.
Hivi form IV na VI Mwenyekiti matokeo yake yakoje?? Maana kama.kumbu kumbu zinaonesha kuwa Q.T inahusika .

Hivi Mwenyekiti wa ufipa alipokuwa anagombea nafasi ya urais mwaka uleeee alikuwa na elimu gani.?? Maana alitaka kupewa dhamana kubwa sana ya kuongoza Taifa zima na maliasili zake huku elimu yake ikiwa ni ya UPE tena akiwa kaunga unga na super glue.
 
Ndugu Jacob kumbuka wahenga walinena "ukitaka kuanzia mbio sharti uagane na nyonga",

Je umetimiza sharti hilo kabla ya kuanza kupiga jalamba??

Kumbuka kuwa "usianzishe ugomvi wakati unaishi kwenye Nyumba ya vioo".

CC: Mwenyekiti wa ufipa....hivi alihitimu Yale masomo yake ya Q.T aliyotangaza kwenda kusomea ughaibuni..??
Nani kakuzuia kushitaki Mbowe kama ana vyeti feki.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom