Meya wa Ubungo akabidhi mashtaka yake dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kwenye tume ya Maadili

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob akiongea na wandishi wa Habari baada ya kukabidhi mashtaka yake dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye tume ya Madili asubui ya leo

IMG-20170322-WA0018[1].jpg

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amemfungulia mashitaka matano Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo ameyawasilisha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Makonda ni pamoja na kughushi vyeti, kupokea zawadi bila kutangaza, jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma, kujipatia mali kutoka kwa watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, kuwadhalilisha watu kwa kuwataja kwenye tuhuma za madawa ya kulevya bila kuwa na vielelezo na kutumia madaraka vibaya.

Hatua hiyo ya meya Jacob, imekuja siku chache baada ya mkuu huyo wa mkoa, kudaiwa kuvamia kwenye ofisi za Clouds Media, kushinikiza kipindi kilichorekodiwa kikiwa na habari ya Mchungaji Josephat Gwajima, kirushwe hewani wakati kipindi cha Shilawadu kikiendelea.

Kitendo hicho kilimlazimu Waziri Nape Nnauye, mwenye dhamana ya kuwalinda waandishi wa habari, aunde tume maalum kuchunguza sakata hilo, ambayo ilipewa muda wa saa 24 kukamilisha kazi yake, lakini mpaka sasa bado ripoti yake haijatoka.
 
Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob akiongea na wandishi wa Habari baada ya kukabidhi mashtaka yake dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye tume ya Madili asubui ya leo
Naomba elimu, hivi tume ya maadili ina coercive powers? or to put it the other way round, to what extent are the decisions of tume ya maadili binding, of what legal effect?
 
Naomba elimu, hivi tume ya maadili ina coercive powers? or to put it the other way round, to what extent are the decisions of tume ya maadili binding, of what legal effect?

hakuna kitu hapo, niamini mimi!
 
Watu wanatafuta sifa za kijinga Makonda anawatengenezea majina wanasiasa uchwala
 
Back
Top Bottom