Meya wa Moshi afunguliwa mashtaka kortini kwa kumzaba kibao mlinzi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,949
22,117
Meya wa Moshi afunguliwa mashtaka kortini kwa kumzaba kibao mlinziNa Daniel Mjema, Moshi

HATIMAYE Serikali imemfungulia mashitaka, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Lameck Kaaya kwa tuhuma za kumpiga makofi na kumjeruhi mlinzi wa manispaa, Christina Joseph.

Kesi hiyo ya jinai namba 258/2009 ilifunguliwa juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi.
Hata hivyo mshitakiwa hakuwepo mahakamani wakati kesi inafunguliwa.


Kwa utaratibu uliozoeleka, watuhumiwa wa makosa ya jinai hufikishwa mahakamani wakiwa chini ya ulinzi isipokuwa pale mtuhumiwa anapokuwa ametoroka.

Ikiwa Meya huyo atatiwa hatiani kwa shitaka hilo lililofunguliwa chini ya kifungu namba 241 cha kanuni ya adhabu namba 16 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Wakili wa Serikali kanda ya Moshi, Scolla Lugongo, aliiomba mahakama iliyokuwa imeketi chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Geni Dudu kutoa hati ya kumuita mshitakiwa mahakamani na mahakama ilikubali ombi hilo.

Kwa mujibu wa hati za kuitwa shaurini, meya huyo ametakiwa kwenda mahakamani Mei 13 mwaka huu, siku ambayo atasomewa rasmi mashitaka yanayomkabili.

Kufunguliwa kwa kesi hiyo kumekuja wiki moja tu baada ya Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kwenda kumuona Waziri wa Mambo ya Ndani kulalamikia upelelezi wa tukio hilo kuchukua zaidi ya siku 40.

Tayari Taasisi ya Haki za binadamu mkoa Kilimanjaro(KWIECO) imemkodisha wakili, Ralph Njau, ili kumtetea mlinzi huyo.

Inadaiwa kuwa kushambuliwa kwa mlinzi huyo kulifanyika Machi 16 mwaka huu katika eneo la maegesho ya magari ya viongoziwa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Inadaiwa kuwa meya alimshambulia mlinzi huyo baada ya kuzuiliwa asiegeshe gari lake binafsi katika eneo la maegesho ya magari ya halmashauri.
 
Back
Top Bottom