Meya wa Moshi aagiza Sh3.2 milioni za kununua bastola ya mkurugenzi kurejeshwa

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,613
Chanzo:- Mwananchi (Friday May 28 2021)

Moshi. Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza Sh3.2 milioni zilizotengwa na halmashauri ya manispaa hiyo kwa ajili ya kununua bastola ya mkurugenzi kurejeshwa.

Raibu ametoa tamko hilo leo Ijumaa Mei 28, 2021 katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Stephen Kagaigai ambaye pia alishiriki kikao hicho.

Amesema fedha hizo zilipitishwa na halmashauri hiyo mwaka 2015 na kubainisha kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

"Kuna fedha zilipitishwa mwaka 2015 kiasi cha Sh3.2 milioni kwenye akaunti ya halmashauri kununua bastola ya mkurugenzi, haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma, nimeagiza fedha hizi zirudishwe mara moja," amesema Raibu.
 
Back
Top Bottom