Meya wa moscow atimuliwa na rais medvedev baada ya miaka 18.

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Meya wa jiji la moscow Yuri Luzhkov ametimuliwa leo baada ya kuwa meya wa moscow kwa miaka 18.Rais Medvedev alisaini barua ya kumfukuza meya huyo siku chache tu baada ya meya huyo kusema kuwa hatan'goka madarakani hata kwa mpini.Medvedev ambaye yuko safarini nchini china alinukuliwa akisema kuwa amemfukuza meya huyo kutokana na wananchi na ikulu kutokuwa na imani naye.Meya huyo ambaye mkewe ni billionea na anamiliki makampuni ya ujenzi anatuhumi kuwa chanzo cha mkewe kuwa bilionea,pia meya huyo ameonekana waziwazi kupingana na ikulu ya moscow(kremlin), na alionekana kupata upinzani kutoka kwa wananchi baada ya yeye kwenda mapumzikoni mwezi wa nane ilihali moscow ilikuwa imetandwa na wingu zito na kuungua kwa misitu inayoizunguka.
Baada ya meya huyo kufukuzwa aliandika barua ya kustaafu kwenye chama kikubwa chenye nguvu cha Putin(idinaya rasia) hali ambayo imeleta wasiwasi mkubwa kutokana na kwamba meya huyo ana wafuasi wengi.
Source:jamiiforums.com
 
Akapumzike kwa amani. Huyo ni mafia mkubwa huyo rais ajiandae kwa revenge maana jamaa ni nuksi huyo.:doh:
 
Akapumzike kwa amani. Huyo ni mafia mkubwa huyo rais ajiandae kwa revenge maana jamaa ni nuksi huyo.:doh:

Marais wote waRussia lazima wawe KGB (Mafia ya Russia). Medvedev hana wasiwasi na maisha yake, yeye mwenyewe kawekwa na hao hao KGB, Putin.
 
Back
Top Bottom