Akizungumza na waandishi wa habari jana Meya huyo Bwana Boniface Jacob alisema, kuna baadhi ya viongozi wilaya ya Kinondoni wanatengeneza matukio na kujifanya kwenda kusuluhisha.
Hivi karibuni, mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alitembelea shamba la waziri Mkuu Mstaafu mh. Sumaye ili kusuluhisha mgogoro uliojitokeza kwenye shamba hilo.
Alisema, "Hakuna mahali kokote unaweza kuendesha kesi baina ya wavamizi na mmiliki halali, mwenye mamlaka na ardhi ni Baraza la Madiwani, vyombo vingine ni kulinda amani".
"Tunachokiona sasa ni kutengeneza matukio na kutafuta 'kiki' ya kisiasa". alisema.
Source: Magazeti na TV.