Meya wa Kinondoni Boniface Jacob ameachiwa kwa dhamana muda huu baadaye kushikiliwa kwa amri ya Dc

Huyo DC labda sio mfuatiliaji wa mambo, aliye karibu naye amweleze kuwa kuna mtu aliwahi kujenga ofisi ya spika nyumbani kwake!
 
NAUTAFAKARI UBONGO ULIOTOA AMRI MEYA AWEKWE MAHABUSU SAA 48

Katika mamlaka za Serikali za Mitaa (Municipal/Local Government), hapo yakizungumzwa majiji, manispaa na miji, kiongozi wa juu kabisa ni Meya.

Kwenye nchi ambazo mamlaka za Serikali Kuu na Serikali za Manispaa zimetenganishwa vizuri, Meya ni cheo ambacho hakichezewi. Meya ni Ofisa Mtendaji Mkuu kwenye jiji, mji au manispaa yake. Meya ni kiongozi mwenye mamlaka kamili ambayo hayaingiliwi na Serikali Kuu.

Hivi karibuni Meya wa New York, Bill de Blasio, alitangaza kuwa New York itaendelea na Mkataba wa Mazingira wa Paris ambao Rais wa Marekani, Donald Trump anaupinga.

Uamuzi wa Blasio uliungwa mkono na mameya wa majiji mengine ya Marekani kwa sababu waliona kuwa Mkataba wa Paris una manufaa makubwa kwenye maeneo yao, hivyo wameahidi kuendelea nao hata kama Rais wao anaukataa.

Hali hiyo inatokea Marekani kwa sababu Serikali za Manispaa haziingiliwi na Serikali Kuu.

Novemba 21, mwaka Jana, baada ya Trump kushinda Urais wa Marekani, Blasio aliwahutubia wakazi wa New York na kuwaeleza kuwa ataiongoza mamlaka ya Jiji la New York kupambana dhidi ya amri za Trump ambazo aliziita za kibaguzi.

Blasio alisema kuwa hakuna Muislam wa New York atakayesajiliwa na hakuna mhamiaji wa Marekani atakayetenganishwa na familia yake. Kauli hiyo ilikuwa kuonesha kuwa Meya anasimamia mamlaka yake.

Umeya ni cheo chenye nguvu. Kipindi cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kumfukuza kazi Mkuu wa Mkoa lakini alishindwa kumfukuza Meya wa Jiji la Dar, Kitwana Kondo ingawa kosa lao lilikuwa moja. Sababu ni kuwa Meya ni mamlaka nyingine. Meya haguswi kienyeji.

Tanzania na sheria zake, Serikali za Manispaa zipo kama matawi ya Serikali Kuu, ndiyo maana Mameya hawana nguvu dhidi ya viongozi wa Serikali Kuu.

Tulishashuhudia vyanzo vingi vya mapato ya Serikali za Manispaa vikihamishiwa Serikali Kuu. Mfano kodi za majengo na mabango ya matangazo barabarani. Serikali za Manispaa zimebaki kuungaunga vyanzo vingine.

Wakati hayo yakiendelea, natafakari kuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob, yupo mahabusu kwa siku ya pili sasa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwamba kiongozi huyo awekwe mahabusu saa 48.

Kosa la Meya inaelezwa ni kuwaalika wana Chadema wenzake kukagua shughuli za halmashauri ambayo inaongozwa na chama hicho. Wana Chadema kutembelea ofisi za halmashauri inayoongozwa na chama chao imeonekana ni kosa.

Wakati huo mwaka huu, Rais Magufuli akiwa ndiye Mwenyekiti wa CCM, aliongoza kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (Nec) ya chama hicho, kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam. Ikulu ikapambwa kijani na njano, rangi za chama.

Ikawa sahihi kwa ofisi kuu ya umma (Ikulu) kufanya shughuli za chama, ila imekuwa dhambi kubwa kwa Manispaa ya Ubungo kupokea wana Chadema kukagua kama jukumu waliloomba kwa wananchi linatekelezwa ipasavyo.

Wana Chadema wameitwa wavamizi na mwenyeji wao, yaani Meya, amewekwa korokoroni kwa saa 48. Uamuzi ni wa Mkuu wa Wilaya. CCM wao walionekana wenyeji wa Ikulu kwa sababu Rais ni wa chama chao.

Tukio la Meya Jacob kuwekwa mahabusu halitoshi kulaaniwa, kwani ni kichekesho kikubwa cha siasa za Tanzania.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Ufisadi wa ndege,na nyumba za serekali
Nilisahau hizi: Duh hasa kwenye Nyumba za Serikali...lakini hii mzee naona atairuka kwanza maana inaweza ikamrudia yeye..tuendelee na haya mengine kwanza maana yapo mengi..
 
Du,kazi ipo je ameachiwa kwa dhamana mahakamani? au kwenye kituo cha polisi?,je ni mashitaka gani yapo kwenye docket?mie nimeachwa na maswali mengi kuliko majibu.
 
Mara nyingi sana vijana wadogo wasiokuwa na busara na hekima wakipewa madaraka hulewa m
apema sana kama huyu Dc na wengine
Ila Mh Makori ni mtu wa makamo na amekuwa serikalini muda mrefu tu. So kuna tatizo jingine na labda wametakiwa kutenda hivyo, either uamue kuachia madaraka au utii maagizo hata kama ni ya kitoto na kijuha.
 
Wabaki naye tu, sisi siasa tumeacha tunaendelea kulinda resilimali zetu. Mpaka December yeyote anayejijua ni fisadi atakuwa ndani...Deep Green, Escrow, IPTL, Stanbic pesa na magunia, EPA etc. Just wait and see the power of JPM..
INAHUSIANAVP NA KUWEKWA NDANI KWA MEYA????
 
Nilisahau hizi: Duh hasa kwenye Nyumba za Serikali...lakini hii mzee naona atairuka kwanza maana inaweza ikamrudia yeye..tuendelee na haya mengine kwanza maana yapo mengi..
Hahahahahaha, nyumba za serikali
 
jackob.jpg


=======

UPDATES

Hatimaye Meya wa Ubungo Jacob, Katibu wa CHADEMA Ubungo Justine, Katibu wa Kata ya Makurumula na makamanda wengine waliokamatwa.

Kwa ya amri ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo wameachiwa huru baada ya saa 48 za kuwekwa ndani bila makosa yoyote.

Chama kitachukua hatua dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwa ukiukaji wa sheria za nchi na matumizi mabaya ya Sheria ya Tawala za Mikoa.

Chanzo: Chadema Media Twitter
 
Back
Top Bottom