Meya wa Kinondoni awataka Wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia huduma za DCB Pesa

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
203
83

Mstahiki Meya wa manispaa ya kinondoni Benjamin Sita Azindua huduma ya kipesa ya "DCB JIRANI" na "DCB PESA" sambamba na Makumu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Pro. Lucian Msambichaka(kulia) na mkurugenzi mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa

Katika kuboresha huduma za kibenki, Benki ya DCB sasa imeanzisha huduma za kibenki kwa njia ya Mawakala (DCB Jirani ) ambapo itarahisisha upatikanaji wa huduma ya DCB PESA, kupata huduma za kibenki kwa wepesi kwa njia ya simu za mkononi.Ofisa wa DCB Pesa bwana Boniphace Asenga amesema Benki hiyo sasa imewasogezea wateja wake waliopo mikoani huduma hii huku zaidi ya mikoa 20 itanufaika na huduma hii,
Mikoa ambayo itafikiwa na huduma hii ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Arusha, Mwanza, Iringa, Mbeya, Njombe, Makambako, Tanga Mjini, Korogwe, Mombo, Morogoro Mjini, Kilosa, Kilombero, Mikumi, Ifakara, Mtwara, Babati, Manyara, Dodoma Mjini, Kibaigwa, Kondoa, Mpwapwa, Bahi, Chamwino na Kongwa.Bwana Asenga amesema kuwa benki yao sasa inafikisha jumla ya mawakala 700 ambao watatoa huduma hizo za kifedha katika kila mkoa

Aidha ameongeza kuwa Benki ya DBC pia inatoa nafai za kibiashara kwa wafanyabiashara wanaotaka kuwa mawakala katika mikoa tajwa hapo kujitokeza ili waweze kupatiwa uwakala kwa lengo na kufikisha huduma kwa karibu zaidi kwa wateja wao kote nchini.

DCB Pesa inamrahisishia mteja kupata huduma za kibenki kupitia simu yake ya mkononi popote alipo ikiwa ni pamoja na Kulipia bili kama vile Luku, Maji, DSTV, Startimes, AzamTV, Zuku, TTCL na Smile, Kuhamisha pesa kwenda kwenye mitandao ya simu kama M-Pesa, Tigo pesa, Airtel Money na Halo Pesa, Kuongeza salio na kununua vifurushi vya muda wa maongezi, Kutuma pesa kutoka akaunti moja kwenda akaunti nyingine pamoja na Kuweka fedha kwenye mtandao wako wa Simu
 
Back
Top Bottom