Meya wa Kinondoni, awasimamisha kazi Mwanasheria mkuu wa Kinondoni na Mthamini wa Manispaa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
BARAZA la Madiwani Manispaa ya Kinondoni imewasimamisha kazi watumishi wawili akiwemo mwanasheria mkuu wa manispaa hiyo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali ya Shilingi Bilioni 7.

Hayo yametokea leo, katika waliosimamishwa yupo mwanasheria wa Halmashauri na mfanyakazi mwingine. Kuna upotevu wa pesa nyingi sana na wamesababisha serikali hasara zaidi ya billioni saba.

=====================

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016 ametangaza kuwasimamisha kazi kwa watumishi wawili wa Manispaa ya Kinondoni, akiweo Mwanasheria Mkuu BW. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga baada ya Madiwani kuamua kwa kauli moja kuwachukulia hatua hiyo.

Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/04/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bwana Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.Kufuatia makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, baraza la Madiwani la terehe 04/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga.

Makosa yaliyogundulika katika Mashauri hayo ni kama yafuatayo:-

1. Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa.
Mkataba huo, ulifanyiwa marekebisho mbalimbali bila idhini ya Halmashauri na hali hiyo kumpatia sauti zaidi Mwekezaji na kuamua analotaka. Manispaa ilipaswa kupata shilingi milioni 900 kwa mwaka katika uwekezaji huo,lakini kutokana na Mgogoro wa kimkataba mapato hayo hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi billion 4.5 mpaka sasa. Mradi ulikamilika tangu 2011 katika viwanja vyote viwili kiwanja Na.277 na 322 ambapo uwekezaji katika kiwanja namba 277 una nyumba (Apartments) 44 na katika kiwanja Na.322 nyumba 68 (Mwekezaji nyumba 29 KMC Nyumba 17)

2 .Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota.
Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota , hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo kongwe. Wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika nyumba, na kutoa madai ya kujengewa nyumba,ama kulipwa fedha za fidia kutokana na usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaana kumalizana na wapangaji nje ya mahakama.

Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya Mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja.Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo,kwa mchanganuo wa Tshs.695,520,000/= pango la mwaka na Tsh2,576,000,000/=fidia ya viwanja 644.

3.Uwekezaji Eneo la Coco Beach Oysterbay.
Manispaa iliingia Mkataba wa Q-Consult Limited. Kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo.

Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini hakukuwa na hatua zozote zilizochukuliwa, na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na serikali mwanasheria mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.

4.Mradi wa ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital LTD)
Katika shauri hili mabadiliko ya mradi yalifanyika bila idhini ya Halmashauri kwa kubadili michoro na kuongeza maeneo mengine katika mradi kama vile kituo cha Mabasi , Matangazo na choo. viwango vya mgawanyo wa mapato ya Manispaa katika maeneo yaalioongezewa ni kidogo ukilinganisha na uhalisia.

Halmashauri haina mkataba na mwekezaji kwa baadhi ya uendeshaji wa majengo 'above two storey'hazipo kwenye kumbukumbu za Halmashauri.
Mkataba juu ya ujenzi na uendeshaji wa stendi hauna manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1%ya makusanyo kwa mwaka sawa na mil.4 tu kwa mwezi wakati kabla ya uwekezaji ,local standy Halmashauri ilikuwa ikipata 12mil. kwa mwezi.

5.Kubomolewa Kwa Ofisi ya Kata ya Msasani.
Mwanachi aliyejulikana kwa jina la Chacha aliingilia eneo la Ofisi ya Kata Msasani na baadae kuishitaki Manispaa.Usimamizi dhaifu wa shauri hilo ulisababisha mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaoendelea.

Hata hivyo bwana Chacha kwa makusudi aliamua kuuza kiwanja hiki, kwa Lake Oil Co. Limited wakati shauri halijaisha. Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo.Tangu upandewa pili ulikataa jaji.Tuna zaidi ya mwaka hatuja pangiwa jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.

6.Ujenzi wa Nyumba za Makazi. (Apartments ) Hill Road Oysterbay
Mradi unafanyika kwa ubia na Mwekezaji Texas Enterprise company LTD, Mkataba uliingiwa mwaka 2009, na Mradi umesimama kwa Muda Mrefu sasa.
Pamefanyika mabadiliko katika Mkataba na Mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya Mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa Mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.

7. Ujenzi wa nyumba za Makazi(Apartments).Kiwanja Na. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited. Mkataba uliingiwa 2019. Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila Idhini ya Halmashauri na kusababisha Mradi kuchelewa kukamilika. Manispaa inakosa Manufaa ya Mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi huu.

Imetolewa na:-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,
Mh. Boniface Jacob
IMG-20160505-WA0041.jpg
 
MWANASHERIA MKUU NA MDHAMINI WA MANISPAA YA KINONDONI WASIMAMISHWA KAZI.

Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/4/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza Mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.

Kufuatia makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, Baraza la Madiwani la tarehe 4/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Richard Chidaga.

Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni:

1. Miradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa, Manispaa vilipaswa kupata shilingi Milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo. Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba Mapato hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi Bilioni 4.5 mpaka sasa.

2. Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota, Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa Nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika Nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba ama kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja. Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa shilingi 695,520,000/= pango la mwaka na 2,576,000,000/= fidia ya viwanja 644.

3.Uwekezaji eneo la Coco Beach Oysterbay Manispaa iliingia mkataba na Q - Consult Limited, Kampuni hiyo ilishindwa kutekelezwa mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-Consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini haikuwa na hatua zozote zilizochukuliwa na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na Serikali Mwanasheria Mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa Mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.

4.Mradi wa Ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital Ltd) Mkataba juu ya uendeshaji wa stendi haina manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1% ya makusanyo kwa mwaka sawa na Shilingi Milioni 4 tu kwa mwaka, wakati kabla ya uwekezaji, local standy Halmashauri ilikuwa ikipata Milioni 12 kwa mwezi.

5. Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani, mwananchi ajulikanaye kwa jina la Chacha aliingilia eneo la ofisi ya kata ya Msasani na baadae kuishtaki Manispaa. Usimamizi dhaifu wa shauri hilo kuisababishia mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaendeleaje. Hata hivyo kwa makusudi Bw. Chacha aliamua kuuza Kiwanda hili kwa Lake Oil CO. Limited wakati shauri halijaisha.Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo, yangu upande wa pili ulikataa Jaji, tuna zaidi ya mwaka hatujapangiwa Jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.

6. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment) Hill Road Oysterbay, mradi inafanyika kwa ubia na mwekezaji Texas Enterprise Company Ltd, mkataba uliingiwa mwaka 2009, na mradi umesimama kwa muda mrefu sasa.Pamefanyika mabadiliko katika mkataba na mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.

7. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment s) Kiwanda no. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited mkataba uliingiwa 2009.

Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila idhini ya Halmashauri na kuisababishia mradi kuchelewa kukamilika, Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi.

Halmashauri bado inaendelea kufuatilia miradi mwingine ambayo umeingia na haina manufaa kwa Halmashauri.

Wakati mwingine JPM akisema kuna watu walifanya Tanzania shamba la bibi yupo sahihi kabisa. Haiwezekani projects zote hizi ambazo Manispaa imeingia ubia wao wawe loosers tu. Ni lazima kuna interest za wafanyakazi wa manispaa kwenye mikataba hiyo
 
Amerudi kwenye soko ati kaomba radhi................Unapokuwa una dable standadi ndivyo inavyokuwa.Wlishindwa kumchukulia hatua Damond na Khadija Kopa ambayo video yao haina tofauti na na ya CHURA.Unafanyeje???
Tena hiyo radhi yenyewe imebidi aende na nguo za ccm
 
Wakati mwingine JPM akisema kuna watu walifanya Tanzania shamba la bibi yupo sahihi kabisa. Haiwezekani projects zote hizi ambazo Manispaa imeingia ubia wao wawe loosers tu. Ni lazima kuna interest za wafanyakazi wa manispaa kwenye mikataba hiyo


Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom