Meya wa Kinondoni, akabidhiwa Ilani ya CHADEMA, Vipaumbele na Muongozo wa CHAMA

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,486
CHADEMA WAMKABIDHI RASMI ILANI, VIPAUMBELE NA MUONGOZO WA CHAMA MEYA WA HALMASHAURI YA KINONDONI
11215710_437031689822768_2124188459744883227_n.jpg

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob (Katikati) akikabidhiwa Ilani ya chama

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Jumatano 3 Februari 2016 katika ofisi za Mstahiki Meya wa Kinondoni zilizopo Magomeni Kinondoni, Dar es salaam imemkabidhi rasmi muongozo, ILANI na vipaumbele vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kuwahudumia wananchi wote wa Manispaa ya KinondonI.

Akiongea mbele ya waandishi habari Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Boniface Jacob amesema, kwa sababu anatokana na CHADEMA, viongozi wake wameeona watembelee Manispaa ya Kinondoni ili waweze kumkabidhi ILANI hiyo, Muongozo na Vipaombele vya Chama.

Wao kama Chama wameona kama kulikuwa na tatizo la maji katika Manispaa ya Kinondoni, sasa jukumu lake wanamtaka akasimamie kuhakikisha kwamba wananchi wa Manispaa ya Kinondoni wanapata huduma za uhakika tofauti na ilivyokuwa awali wakati Manispaa hiyo ikiwa chini ya CCM.

Akiongea katika makabidhiano hayo Bw. Kasmir Mabina akiwa ni Mratibu wa Kanda ambaye ndiye aliyemkabidhi ILANI, Muongozo na Vipaumbele vya Chama kwa niaba ya Chama Makao Makuu ya CHADEMA Kinondoni, Dar es salaam amesema “tumekuja hapa tukiwa sisi ndiyo Chama tawala katika Halmashauri ya Kinondoni, kwa hiyo basi inabidi tuwaelekeze WANAUKAWA kupitia Meya wa Halmsahauri ya Kinondoni, ambaye wamemchagua wenyewe, Bw. Boniface Jacob, ILANI tuliadhimia kupitia ILANI yetu, amabyo ipo wazi kabisa, ILANI ya CHADEMA/UKAWA ni kitu gani wanaweza kutekeleza, na mambo gani yapo ndani ya ILANI, hasa ukizinagatia tumeona mambo mbalimbali yakiendelea kabla hata wajaingia madarakani au hata Meya hajaingia madarakani, tumeona bomoa bomoa na vitu vingi vikifanyika NEMC imefanya mambo mengi, matamko mengi yakiwemo ya elimu na mambo mbalimbali tukaona kwamba tusikae kimya tumuache Meya wetu aende tu inatakiwa tumkumbushe yale ambayo inawezakana anayajua tukimkumbusha kwamba tutayafuatialia na tunataka tuone kwamba anayatolea taarifa pamoja na Madiwani wetu”.

Akiongelea suala la bomoa bomoa na vitu mbalimbali vinafanyika, akiikagua ILANI ya CHADEMA/UKAWA ukurasa wa 29 Bw. Mabina amesema ILANI imeeleza wazi kabisa, wakazi wengi hasa wa mijini wamepoteza mali zao na vitu mbalimbali bila kulipwa fidia na hivyo kuwafanya wananchi hao kuwa katika lindi la umasikini, katika mabonde ambayo yapo katika Manispaa ya Mstahiki Meya wa Kinondoni Bw. Boniface Jacob, wananchi wake wamebomolewa na wanaendelea kubomolewa bila kulipwa fidia.

Kama Chama hawakatai kubomolewa, kwa sababu kila unapotaka kufanya maendeleo hulazimika miundo fulani iliyokuwepo iondolewe, lazima kuna watu watahamishwa kwenda sehemu nyingine, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo hakipingi maendeleo hayo lakini ni jinsi gani mchakato huo au operesheni ya kuwaondoa watu kwenye maeneo hayo.

Katika ILANI ya CHADEMA/UKAWA ilieleza kwamba watu walipwe, utu uzingatiwe kwamba wale ni binadamu wana watoto, wazee, wakinamama kuna wajawazito, Bw. Mabina alihoji utu uko wapi? Wale sio kuku, sio mbuzi, kwa katika Manispaa ya Kinondoni iliyopo chini ya CHADEMA/UKAWA wametakiwa kulitazama hili, katika nchi zilizoendelea na katika nchi nyingi, kuna Master Plan za miji na majiji.

Bw. Kasmir Mabina aliendelea kuhoji kwamba Master Plan za jiji la Dar es salaam, NEMC pamoja na Wizara ya Ardhi pamoja na vyombo vyote, vinatakiwa kuonyesha Master Plan, watu hutangulia kufanya maendeleo kabla ya kuona Master Plan, Master Plan ikifika ndipo suala la bomoa bomoa linapokuja, Mstahiki Meya na Madiwani wametakiwa kwenda kwenye maeneo husika, kuanza kujua athari zilizotokea na wale wanaostahili kulipwa walipwe.

Kususiana na elimu Bwa. Kasmiri Mabina amsema amesikia madiwani waliochini ya Meya Boniface, wameshaana kuzunguka, wamekuta watoto wakikaa chini, akimkumbusha Mstahiki Meya kwamba kitakachopimwa katika Manispaa iliyopo chini ya CHADEMA/UKAWA ni jinsi gani wamesimamia mchakato wa elimu, toka mwaka 2010 ilipoundwa ILANI ya kwanza ya CHADEMA, ILANi ilieleza kwamba CHADEMA watatoa elimu bure, 2015 ikaeleza hivyo hivyo, huu ni wakati kulizingatia hilo kwa kutazama vyanzo vya fedha na kuhakikisha inatimizwa katika maeneo hayo.

Ingawa serikali iliyopo madarakani imesema kwamba itatoa elimu bure mpaka fomu four, Manispaa ya Kinondoni inatakiwa kuangalia ili kuona ni jinsi gani wataweza kuziba mapengo hayo, kwa sababu Manispaa ya Kinondoni imekuwa ikikusanya fedha nyingi sana zaidi ya bilioni 50, kwa kushikwa na CHADEMA kuna uhakika hayo yatatekelezwa.

Akimkabidhi pamoja na KATIBA ya Chama, Bw. Mabina amesema KATIBA ya Chama inamtaka Mstahiki Meya pamoja na Madiwani katika ibara ya 3 ya kanuni za kuendesha Manispaa , ibara ya 2 kifungu kidogo cha 2 (D) inasema “ Kila Mwenyekiti wa Halmashauri, akiwa Mwenyekiti ni Meya wa CHADEMA, anatakiwa kuwasilisha mipango ya mikakati ya maendeleo na huduma waliojiwekea kwa mwaka husika katika kikao cha Kamati Kuu ya kwanza ya mwaka huo wa fedha.

Kifungu cha (D) kinasema kila Mwenyekiti wa Halmshauri ya CHADEMA, atatakiwa kutoa taarifa za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Halmashauri yake kwa mujibu wa ILANI ya Chama, kwenye kila kikao cha Kamati Kuu, kwa maana hiyo Kikao cha kwanza cha Kamati Kuu ambacho kitafanyika mwezi wa Februari mwishoni, atatakiwa kuwasilisha programu ya mwaka mzima, katika kuona ILANi inatekelezwa, lakini kila Kamati Kuu inapokutana, Meya atatakiwa kueleza utekelezaji unavyofanywa na Mstahiki Meya, hatua kwa hatua, itasaidia kujua ni kwa jinsi gani CHADEMA na UKAWA wanaweza kusimamia utekelezaji, pamoja na kuwaharifu wawakilishi wao waliopo bungeni kwa wale wanaotunga sheria, namna gani Halmashauri zinaendeshwa na namna gani wanaweza kuisimamia serikali, kwa maana ya chombo ya utungaji wa sheria.

Baada ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amesema amepokea maagizo ya Chama ya kusimamia haki, usawa kutenda vile ambavyo Chama kimekuwa kikijinadi, isije ikawa CHADEMA inapinga uonevu alafu wanafika Manispaa wanaendeleza uonevu, kwa hiyo atakuwa akikihaibisha Chama na kukiweka katika hali mbaya. Mstahiki Meya amewahakikishia wananchi kwamba kupokea maelekezo ya Chama sasa ndio iwe kuvionea vyama vingine, amesema atakuwa Meya wa watu wote, Meya wa CCM, TLP na vyama vingine vyote.

Akiendelea kuongea na waandishi wa habari, Mstahiki Meya ameeleza kwamba, kila Chama kinaposhinda kinakuwa na jambo lake la kutekeleza katika ILANI yake, kwa sababu CHADEMA imepewa dhamana ya kuongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, hivyo ni lazima apewe miongozo inayoendana na Manispaa ya Kinondoni, akiongea Mstahiki Meya amesema “Naona huku kwenye ILANI Chama wamehainisha mambo muhimu ya kuanza nayo, vikiwemo unyanyasaji, ukandamizaji kupitia bomoa bomoa, lakini humu vile vile naona wameainisha mambo ya ardhi, wameainisha maji, wameainisha uchafu, wameainisha makusanya ya Halmashauri, ambayo mimi kama Meya kutokana na Chama hicho na UKAWA, kuhakikisha yale tuliyokuwa tukijinadi nayo kuyatenda sawa na kama tulivyowahi kuyaongea”.

Mstahiki Meya wa Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amekihakikishia Chama kwamba atakuwa na Chama sambamba katika kuyatekekeleza yale yote yaliyokusudiwa, pia ameanisha mipango ambayo wameshaanza nayo kama Manispaa ya Kinondoni, wameanza kuweka nguvu nyingi kwenye kumaliza uchafu kwa sababu Manispaa imeonekana ni chafu, Manispaa ina mikakati kamambe ya kununua trucks kwa ajili ya uzoaji wa taka, kwenye bajeti ya mwaka huu, trucks 35 hadi 40, kununua compactor kwa ajili ya kushindilia taka taka.

UKiacha hayo pia kuna mpango wa kujenga dampo la kisasa la kuchomea taka katika eneo la Mwabepande, katika kuhakikisha taka zinaondoka, tumekuta Manispaa inakusanya taka tani 700 wakati kuna taka tani 2026, Mstahiki Meya amesema ndani ya Mwaka mmoja itawezekana Manispaa ikawa inakusanya taka zote 2026 kwa siku moja.

Uwezo wa ukusanyaji taka taka unaenda kuwa mkubwa zaidi lakini hapo awali uwezo ulikuwa mdogo sana, Meya amemuhakikishia Meya kwamba wamekuta kwamba katika bajeti yao wamekuta wana bilioni 48 mpaka 51, walipitisha 51 kwenye Barza, zikiwa ndiyo malengo yao, bungeni TAMISEMI waliwaambia kwamba wakusanye bilioni 48, Mstahiki Meya ameahidi kwamba uongozi wake kwa mwaka mmoja wataweza kukusanya mara tatu ya hiyo.

Mstahiki Meya amesema atatoa listi ya makampuni yalikwepa kodi ambapo kodi bilioni 5 mpaka 10, ameahidi kuwaita waandishi wa habari kuwaeleza ni wakina nani wanakwepa kodi hizo na watalazimika kuzilipa, Pia amasema kwa wale waharibifu wa barabara, wakikamatwa wataandikiwa barua hawatakiwi kuonekana Kinondoni tena, watapeleka kwa mamla zote za uandisi ikiwemo bodi ya usajili wa Waandisi, ikiwemo bodi ya Makandarasi, CRB, ERB pamoja na bodi ya manunuzi ya UMMA BBRA.

Akiongelea sakata linaloendelea la Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Fredirick Sumaye, Mstahiki Meya amesema anaona kwamba kuna siasa inachezwa, siasa yenyewe ni ya kitoto, inapaswa kupuuziwa, Bw. Boniface Jacob Meya Manispaa ya Kinondoni amekuwa diwani kwa miaka 5 iliyopita katika Halmashauri hii, wavamizi walishamalizwa wote katika Manispaa ya Kinondoni, hakuna sababu ya kuongea na mvamizi kwa Manispaa ya Kinondoni, haiwezekanai kiongozi wa serikali unaenda kuelewana na wavamizi katika Manispaa ya Kinondoni haitatokea.

Manispaa ya Kinondoni ilikuwa chini ya CCM, 2013 iliendeshwa operesheni ya kubomoa nyumba 360 chini ya Mkuu wa Wilaya aliyekuwa Bwa. Jordan Ligumbala, na operesheni hiyo ilisimamiwa na Manispaa ya Kinondoni, nyumba 360 zilizobomolewa walikuwa ni wavamizi walioingia kwenye mashamba ya watu, siku hizi viongozi wanatengeneza wavamizi kwa kuwaruhusu alafu baadae wanakuja kutafuta attention ya kwenda kuongea na wavamizi, Mstahiki Meya ameiita huo kama ni utaratibu wa ajabu na mbaya sana na amemuahidi Mratibu wa Kanda kuwa hilo halitotokea kwa Manispaa ya Kinondoni.

Amesema hivyo kwa sababu jukumu la kugawa ardhi ni baraza la Madiwani, kupitia kamati yake ya mipango miji na kamati yake ya fedha ndiyo unaweza kupewa ardhi, kwa hiyo asijitokeze mtu yeyote akasema anaweza kutoa ardhi, viongozi wengine wa serikali kama polisi wanaruhusiwa kuingia sehemu tu kama kuna waandishi wahabari hapo ndipo wanaruhusiwa hawana mamlaka ya hata kujadili watampa nani kwenye sheria na katiba ipo wazi, kwa hiyo zimeonekana siasa za kitoto ambapo kada wa CHADEMA Waziri Mkuu Mstaafu Fredirick Sumaye, pia yalisikika maneno kwenye kampeni, walisema kwamba watamnyang’anya mashamba, kwa hiyo ilikuwa ni kutaka kuanza kutekeleza mkakati mchafu, kwa kuanza kunyanyasa, kwa hiyo wakifanya hivyo kwa kada yule kwa sababu ni CHADEMA, Mstahiki Meya ameeleza kwamba wanajua mashamba mengi ya viongozi wa CCM, watawaruhusu wananchi wa Kinondoni wakayavamie, wanajulikana wengi na ni viongozi wakubwa serikalini.
 
Yaani kuziba na kujaza kabisa! . Ndani ya mwaka kusiwe na mtoto anakaa chini shule za Kinondoni !. Pili taka mitaani inatakiwa isionekana kama shilingi inavyokuwa kungumu kupata! etc
 
Hivi Meya anatakiwa kutekeleza ilani ya Serikali iliyopo madarakani au ya kwake ya mfukoni??

Je vipaumbele vinavyotekelezwa ni vya Serikali iliyopo madarakani au ya Kwake ya mfukoni?

Je rasilimali watu, fedha nk zinatoka kwa Serikali iliyopo madarakani au iliyopo mfukoni???

Kuna mambo siyaelewi hapa naomba ufafanuzi!!!

Queen Esther

Tangu lini CHADEMA wakawa na Ilani!?
 
Mbona cover ni ya Chadema na wewe UNASEMA ni ilani ya UKAWA?? Unawachokoza CUF na NCCR ambayo imekosa hata Mbunge mmoja Wa Viti maalum. Hata wale Wa kuhamishwa kama walivyo wahamisha wale Wa CCM na wakapewa Ubunge Viti Maalum Chadema.

Nimesikia ACT baada ya Mhe. Zitto kuwasilisha madai ya wabunge Wa Viti maalum baada ya kupata 5% karibu atapata wabunge. Vipi vyama vya NCCR na Vingine vilivyounda UKAWA nje ya CUF na CDM????????????? Au ni Muungano haramu???????

Queen Esther

uko sahihi , ni ilani ya UKAWA .
 
sikia dadaangu , ilani ya Chadema , ndiyo ilani ya UKAWA , hii ni kwa mujibu wa makubaliano .
 
Hivi Meya anatakiwa kutekeleza ilani ya Serikali iliyopo madarakani au ya kwake ya mfukoni??

Je vipaumbele vinavyotekelezwa ni vya Serikali iliyopo madarakani au ya Kwake ya mfukoni?

Je rasilimali watu, fedha nk zinatoka kwa Serikali iliyopo madarakani au iliyopo mfukoni???

Kuna mambo siyaelewi hapa naomba ufafanuzi!!!

Queen Esther
kuna mapato yanayokusanywa na halmashauri na yanatumika kwa halmashaur husika.

it's just a percentage sent to central government

Mayor Ana mamlaka katika eneo lake
 
Najua wengi tunashambikia zaidi, ila Ilani ya CDM haiwezekani kutekelezwa kwa sababu bajeti inakuja kutegemea na mpango kazi wa utekelezaji wa Ilani ya chama Tawala.

Zaidi usimamizi ndo watafanya na kujitofautisha na CCM. Ingawa, pia kunaweza tokea shida ya bajeti ambayo ni hujama kwa kawaida.
 
CHADEMA WAMKABIDHI RASMI ILANI, VIPAUMBELE NA MUONGOZO WA CHAMA MEYA WA HALMASHAURI YA KINONDONI
11215710_437031689822768_2124188459744883227_n.jpg

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob (Katikati) akikabidhiwa Ilani ya chama

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Jumatano 3 Februari 2016 katika ofisi za Mstahiki Meya wa Kinondoni zilizopo Magomeni Kinondoni, Dar es salaam imemkabidhi rasmi muongozo, ILANI na vipaumbele vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kuwahudumia wananchi wote wa Manispaa ya KinondonI.

Akiongea mbele ya waandishi habari Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Boniface Jacob amesema, kwa sababu anatokana na CHADEMA, viongozi wake wameeona watembelee Manispaa ya Kinondoni ili waweze kumkabidhi ILANI hiyo, Muongozo na Vipaombele vya Chama.

Wao kama Chama wameona kama kulikuwa na tatizo la maji katika Manispaa ya Kinondoni, sasa jukumu lake wanamtaka akasimamie kuhakikisha kwamba wananchi wa Manispaa ya Kinondoni wanapata huduma za uhakika tofauti na ilivyokuwa awali wakati Manispaa hiyo ikiwa chini ya CCM.

Akiongea katika makabidhiano hayo Bw. Kasmir Mabina akiwa ni Mratibu wa Kanda ambaye ndiye aliyemkabidhi ILANI, Muongozo na Vipaumbele vya Chama kwa niaba ya Chama Makao Makuu ya CHADEMA Kinondoni, Dar es salaam amesema “tumekuja hapa tukiwa sisi ndiyo Chama tawala katika Halmashauri ya Kinondoni, kwa hiyo basi inabidi tuwaelekeze WANAUKAWA kupitia Meya wa Halmsahauri ya Kinondoni, ambaye wamemchagua wenyewe, Bw. Boniface Jacob, ILANI tuliadhimia kupitia ILANI yetu, amabyo ipo wazi kabisa, ILANI ya CHADEMA/UKAWA ni kitu gani wanaweza kutekeleza, na mambo gani yapo ndani ya ILANI, hasa ukizinagatia tumeona mambo mbalimbali yakiendelea kabla hata wajaingia madarakani au hata Meya hajaingia madarakani, tumeona bomoa bomoa na vitu vingi vikifanyika NEMC imefanya mambo mengi, matamko mengi yakiwemo ya elimu na mambo mbalimbali tukaona kwamba tusikae kimya tumuache Meya wetu aende tu inatakiwa tumkumbushe yale ambayo inawezakana anayajua tukimkumbusha kwamba tutayafuatialia na tunataka tuone kwamba anayatolea taarifa pamoja na Madiwani wetu”.

Akiongelea suala la bomoa bomoa na vitu mbalimbali vinafanyika, akiikagua ILANI ya CHADEMA/UKAWA ukurasa wa 29 Bw. Mabina amesema ILANI imeeleza wazi kabisa, wakazi wengi hasa wa mijini wamepoteza mali zao na vitu mbalimbali bila kulipwa fidia na hivyo kuwafanya wananchi hao kuwa katika lindi la umasikini, katika mabonde ambayo yapo katika Manispaa ya Mstahiki Meya wa Kinondoni Bw. Boniface Jacob, wananchi wake wamebomolewa na wanaendelea kubomolewa bila kulipwa fidia.

Kama Chama hawakatai kubomolewa, kwa sababu kila unapotaka kufanya maendeleo hulazimika miundo fulani iliyokuwepo iondolewe, lazima kuna watu watahamishwa kwenda sehemu nyingine, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo hakipingi maendeleo hayo lakini ni jinsi gani mchakato huo au operesheni ya kuwaondoa watu kwenye maeneo hayo.

Katika ILANI ya CHADEMA/UKAWA ilieleza kwamba watu walipwe, utu uzingatiwe kwamba wale ni binadamu wana watoto, wazee, wakinamama kuna wajawazito, Bw. Mabina alihoji utu uko wapi? Wale sio kuku, sio mbuzi, kwa katika Manispaa ya Kinondoni iliyopo chini ya CHADEMA/UKAWA wametakiwa kulitazama hili, katika nchi zilizoendelea na katika nchi nyingi, kuna Master Plan za miji na majiji.

Bw. Kasmir Mabina aliendelea kuhoji kwamba Master Plan za jiji la Dar es salaam, NEMC pamoja na Wizara ya Ardhi pamoja na vyombo vyote, vinatakiwa kuonyesha Master Plan, watu hutangulia kufanya maendeleo kabla ya kuona Master Plan, Master Plan ikifika ndipo suala la bomoa bomoa linapokuja, Mstahiki Meya na Madiwani wametakiwa kwenda kwenye maeneo husika, kuanza kujua athari zilizotokea na wale wanaostahili kulipwa walipwe.

Kususiana na elimu Bwa. Kasmiri Mabina amsema amesikia madiwani waliochini ya Meya Boniface, wameshaana kuzunguka, wamekuta watoto wakikaa chini, akimkumbusha Mstahiki Meya kwamba kitakachopimwa katika Manispaa iliyopo chini ya CHADEMA/UKAWA ni jinsi gani wamesimamia mchakato wa elimu, toka mwaka 2010 ilipoundwa ILANI ya kwanza ya CHADEMA, ILANi ilieleza kwamba CHADEMA watatoa elimu bure, 2015 ikaeleza hivyo hivyo, huu ni wakati kulizingatia hilo kwa kutazama vyanzo vya fedha na kuhakikisha inatimizwa katika maeneo hayo.

Ingawa serikali iliyopo madarakani imesema kwamba itatoa elimu bure mpaka fomu four, Manispaa ya Kinondoni inatakiwa kuangalia ili kuona ni jinsi gani wataweza kuziba mapengo hayo, kwa sababu Manispaa ya Kinondoni imekuwa ikikusanya fedha nyingi sana zaidi ya bilioni 50, kwa kushikwa na CHADEMA kuna uhakika hayo yatatekelezwa.

Akimkabidhi pamoja na KATIBA ya Chama, Bw. Mabina amesema KATIBA ya Chama inamtaka Mstahiki Meya pamoja na Madiwani katika ibara ya 3 ya kanuni za kuendesha Manispaa , ibara ya 2 kifungu kidogo cha 2 (D) inasema “ Kila Mwenyekiti wa Halmashauri, akiwa Mwenyekiti ni Meya wa CHADEMA, anatakiwa kuwasilisha mipango ya mikakati ya maendeleo na huduma waliojiwekea kwa mwaka husika katika kikao cha Kamati Kuu ya kwanza ya mwaka huo wa fedha.

Kifungu cha (D) kinasema kila Mwenyekiti wa Halmshauri ya CHADEMA, atatakiwa kutoa taarifa za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Halmashauri yake kwa mujibu wa ILANI ya Chama, kwenye kila kikao cha Kamati Kuu, kwa maana hiyo Kikao cha kwanza cha Kamati Kuu ambacho kitafanyika mwezi wa Februari mwishoni, atatakiwa kuwasilisha programu ya mwaka mzima, katika kuona ILANi inatekelezwa, lakini kila Kamati Kuu inapokutana, Meya atatakiwa kueleza utekelezaji unavyofanywa na Mstahiki Meya, hatua kwa hatua, itasaidia kujua ni kwa jinsi gani CHADEMA na UKAWA wanaweza kusimamia utekelezaji, pamoja na kuwaharifu wawakilishi wao waliopo bungeni kwa wale wanaotunga sheria, namna gani Halmashauri zinaendeshwa na namna gani wanaweza kuisimamia serikali, kwa maana ya chombo ya utungaji wa sheria.

Baada ya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amesema amepokea maagizo ya Chama ya kusimamia haki, usawa kutenda vile ambavyo Chama kimekuwa kikijinadi, isije ikawa CHADEMA inapinga uonevu alafu wanafika Manispaa wanaendeleza uonevu, kwa hiyo atakuwa akikihaibisha Chama na kukiweka katika hali mbaya. Mstahiki Meya amewahakikishia wananchi kwamba kupokea maelekezo ya Chama sasa ndio iwe kuvionea vyama vingine, amesema atakuwa Meya wa watu wote, Meya wa CCM, TLP na vyama vingine vyote.

Akiendelea kuongea na waandishi wa habari, Mstahiki Meya ameeleza kwamba, kila Chama kinaposhinda kinakuwa na jambo lake la kutekeleza katika ILANI yake, kwa sababu CHADEMA imepewa dhamana ya kuongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, hivyo ni lazima apewe miongozo inayoendana na Manispaa ya Kinondoni, akiongea Mstahiki Meya amesema “Naona huku kwenye ILANI Chama wamehainisha mambo muhimu ya kuanza nayo, vikiwemo unyanyasaji, ukandamizaji kupitia bomoa bomoa, lakini humu vile vile naona wameainisha mambo ya ardhi, wameainisha maji, wameainisha uchafu, wameainisha makusanya ya Halmashauri, ambayo mimi kama Meya kutokana na Chama hicho na UKAWA, kuhakikisha yale tuliyokuwa tukijinadi nayo kuyatenda sawa na kama tulivyowahi kuyaongea”.

Mstahiki Meya wa Kinondoni Mhe. Boniface Jacob amekihakikishia Chama kwamba atakuwa na Chama sambamba katika kuyatekekeleza yale yote yaliyokusudiwa, pia ameanisha mipango ambayo wameshaanza nayo kama Manispaa ya Kinondoni, wameanza kuweka nguvu nyingi kwenye kumaliza uchafu kwa sababu Manispaa imeonekana ni chafu, Manispaa ina mikakati kamambe ya kununua trucks kwa ajili ya uzoaji wa taka, kwenye bajeti ya mwaka huu, trucks 35 hadi 40, kununua compactor kwa ajili ya kushindilia taka taka.

UKiacha hayo pia kuna mpango wa kujenga dampo la kisasa la kuchomea taka katika eneo la Mwabepande, katika kuhakikisha taka zinaondoka, tumekuta Manispaa inakusanya taka tani 700 wakati kuna taka tani 2026, Mstahiki Meya amesema ndani ya Mwaka mmoja itawezekana Manispaa ikawa inakusanya taka zote 2026 kwa siku moja.

Uwezo wa ukusanyaji taka taka unaenda kuwa mkubwa zaidi lakini hapo awali uwezo ulikuwa mdogo sana, Meya amemuhakikishia Meya kwamba wamekuta kwamba katika bajeti yao wamekuta wana bilioni 48 mpaka 51, walipitisha 51 kwenye Barza, zikiwa ndiyo malengo yao, bungeni TAMISEMI waliwaambia kwamba wakusanye bilioni 48, Mstahiki Meya ameahidi kwamba uongozi wake kwa mwaka mmoja wataweza kukusanya mara tatu ya hiyo.

Mstahiki Meya amesema atatoa listi ya makampuni yalikwepa kodi ambapo kodi bilioni 5 mpaka 10, ameahidi kuwaita waandishi wa habari kuwaeleza ni wakina nani wanakwepa kodi hizo na watalazimika kuzilipa, Pia amasema kwa wale waharibifu wa barabara, wakikamatwa wataandikiwa barua hawatakiwi kuonekana Kinondoni tena, watapeleka kwa mamla zote za uandisi ikiwemo bodi ya usajili wa Waandisi, ikiwemo bodi ya Makandarasi, CRB, ERB pamoja na bodi ya manunuzi ya UMMA BBRA.

Akiongelea sakata linaloendelea la Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Fredirick Sumaye, Mstahiki Meya amesema anaona kwamba kuna siasa inachezwa, siasa yenyewe ni ya kitoto, inapaswa kupuuziwa, Bw. Boniface Jacob Meya Manispaa ya Kinondoni amekuwa diwani kwa miaka 5 iliyopita katika Halmashauri hii, wavamizi walishamalizwa wote katika Manispaa ya Kinondoni, hakuna sababu ya kuongea na mvamizi kwa Manispaa ya Kinondoni, haiwezekanai kiongozi wa serikali unaenda kuelewana na wavamizi katika Manispaa ya Kinondoni haitatokea.

Manispaa ya Kinondoni ilikuwa chini ya CCM, 2013 iliendeshwa operesheni ya kubomoa nyumba 360 chini ya Mkuu wa Wilaya aliyekuwa Bwa. Jordan Ligumbala, na operesheni hiyo ilisimamiwa na Manispaa ya Kinondoni, nyumba 360 zilizobomolewa walikuwa ni wavamizi walioingia kwenye mashamba ya watu, siku hizi viongozi wanatengeneza wavamizi kwa kuwaruhusu alafu baadae wanakuja kutafuta attention ya kwenda kuongea na wavamizi, Mstahiki Meya ameiita huo kama ni utaratibu wa ajabu na mbaya sana na amemuahidi Mratibu wa Kanda kuwa hilo halitotokea kwa Manispaa ya Kinondoni.

Amesema hivyo kwa sababu jukumu la kugawa ardhi ni baraza la Madiwani, kupitia kamati yake ya mipango miji na kamati yake ya fedha ndiyo unaweza kupewa ardhi, kwa hiyo asijitokeze mtu yeyote akasema anaweza kutoa ardhi, viongozi wengine wa serikali kama polisi wanaruhusiwa kuingia sehemu tu kama kuna waandishi wahabari hapo ndipo wanaruhusiwa hawana mamlaka ya hata kujadili watampa nani kwenye sheria na katiba ipo wazi, kwa hiyo zimeonekana siasa za kitoto ambapo kada wa CHADEMA Waziri Mkuu Mstaafu Fredirick Sumaye, pia yalisikika maneno kwenye kampeni, walisema kwamba watamnyang’anya mashamba, kwa hiyo ilikuwa ni kutaka kuanza kutekeleza mkakati mchafu, kwa kuanza kunyanyasa, kwa hiyo wakifanya hivyo kwa kada yule kwa sababu ni CHADEMA, Mstahiki Meya ameeleza kwamba wanajua mashamba mengi ya viongozi wa CCM, watawaruhusu wananchi wa Kinondoni wakayavamie, wanajulikana wengi na ni viongozi wakubwa serikalini.
Bado meya wa jiji na hapo ndio tutasikia masaburi kajitia katani kwa shingo
 
.....Na kazi ikafanyike sasa!! kwa maana tumewapa dhamana kwa eneo dogo kwa tarajio lilo kubwa.
Ifanyike kwa kipindi gani mkuu maana tuliwaachia ccm miaka 54 lkn hadi sasa hakuna kitu,tunawaombea ukawa wawashinde mashetani ccm
 
Back
Top Bottom