Meya wa Kinondoni Agawa Bure Maeneo ya Biashara Leo na Kufuta Umiliki wa Vibanda na Vizimba 100

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
IMG-20160429-WA0039.jpg

IMG-20160429-WA0038.jpg

IMG-20160429-WA0041.jpg


Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob amezua taharuki kwa wamachinga wa ubungo na kukimbia biashara zao wakiambatana naye mithili ya Maandamano mara baada ya kutangaza kufuta umiliki wa vizimba na mabanda takriban 100 yaliyokuwa yakimilikiwa na watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika soko la Mawasiliano Maarufu kama Simu 2000 akiagiza wapewe bure.

Mstahiki Jacob aliyefuatana na watendaji wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu akiongea na wamachinga mmoja mmoja na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi ubungo maji akiwaelimisha umuhimu wa oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia za juu na kuanza kwa usafiri wa mabasi ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale alipotaja Manispaa kuwa na masoko 26 yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia Mikataba ya kupangisha wakati wamejiagawia bure.

Aidha Mstahiki Meya Boniface Jacob amesema katika kuhakikisha wafanya biashara wadogo wanatengewa maneo yao watafanya uhakiki katika masoko yote kubaini viongozi na watendaji waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili masoko yatumiwe na walengwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku mtendaji wa kata ya ubungo Bw. Gilbati Mushi akieleza hatua hiyo kudhirisha utawala bora.


Chanzo:ITV
=================

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob leo Ijumaa 29/04/2016 amefanya ziara katika eneo la ubungo na kuongea na wafanyabiashara ikiwemo kuwaonyesha eneo la kufanya biashara zao.

Amewataka wafanyabiashara hao kesho wasiwepo maeneo hayo na kuhamishia biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano (Sinza), kwani wasipofanya hivyo Kamati ya usalama na ulinzi na usalama Manispaa ya Kinondoni imeshakaa na imepanga kuwaondoa.

Meya ameona isingekuwa busara kuwaondoa bila kujua watakwenda wapi, Meya amewakabidhi wafanyabiashara hao kadi ambazo watazionyesha ili wasisumbuliwe,pia amewataka wasilipe pesa yeyote endapo watatakiwa walipie maeneo ya biashara waliyopewa.

Pia amesema kuhusu ushuru hawatalipa kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo watalipia, amewahakikishia wafanyabiashara hao hakuna atakayekosa eneo la kufanya biashara.

Afisa biashara wa Manispaa ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara kutokaidi agizo hilo kwani Meya aliomba aje azungumze nao kwanza ili wasishtukizwe bila kupewa taarifa,hivyo kuanzia kesho wataondolewa kwa nguvu.

Meya amesema kuna maeneo wamepewa madiwani akiwemo yeye na hayafanyiwi biashara, hivyi sio sawa maeneo hayo wapewe wafanyabiashara.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, amewaahidi wafanyabiashara hao kwamba kesho atafika katika eneo hilo ili kuona jinsi wafanyabiashara hao wanavyoendelea na kuangalia changamoto zilizopo ili zitatuliwe kwa haraka ili wafanyabiashara hao wafanye biashara zao katika hali nzuri.
 
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg


Anaadika Boniface Jacob ( Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni kuhusiana na hatma ya wafanyabiashara ndogondogo maeneo ya Ubungo)

Leo nimefanya ziara na maandamano katika eneo la UBUNGO na wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga),

Mwanzo utaratibu ulihitaji watolewe ili kupisha barabara ya mwendo kasi ila nimeona isingekua vyema vijana wetu kutolewa pasipo kuwa na mahala pa kufanyia kazi hivyo nimefanya jitihada za kuomba muda hadi tupate eneo la kuwahamishia, nafurahi jitihada hizo zimeheshimika na mwisho leo tumepata eneo la bure kutoka katika Halmashauri kwa ajili ya wafanyabiashara kufanya shughuli zao bila bugudha.

Nawasihi wafanyabiashara wa eneo la Ubungo wafanye mchakato wa kuhama maeneo hayo na kuhamishia biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano (Sinza).

Pia nimewakabidhi kadi za utambulisho baadhi na wengine watafuata utaratibu kesho asubuhi eneo la soko ili kupata umiliki, itambulike kuwa maeneo hayo ni bure na ushuru tutaanza kuwatoza baada ya mwezi mmoja ili kuruhusu kupiga hatua za mtaji.

Zaidi nawasihi wananchi wote wa maeneo ya Ubungo tuhamie kufanya manunuzi soko jipya la Stand ya Mawasilino(Simu 2000).
 
Usitegemee kuna machinga ataenda huko kirahisi, huko wataenda kukaba nafasi tu ila biashara watafanyia Ubungo kama kawaida.

Machinga ni mtaji kwa wanasiasa pia ni jipu kwa wanasiasa.!
Nafikiri baada ya sasa kuondolewa kwa kubembelezwa na kupewa vibanda bureeeeee....Kitakachofuatia ni "Geshi la Polisi" kufanya yake....pale Ubungo sisi watu wa mikoani tukija tunaibiwa sana na ule msongamano
 
Hivi wale kariakoo walioua MTU wamerudi?
Tatizo la marching guys wasipoona Wateja watarudi tena.

Wateja mkitaka hapo wahame basi msinunue bidhaa hapo
 
Hongera sana Meya tunahitaji viongozi kama hawa wa kutuletea maendeleo siyo maigizo
 
Usitegemee kuna machinga ataenda huko kirahisi, huko wataenda kukaba nafasi tu ila biashara watafanyia Ubungo kama kawaida.

Machinga ni mtaji kwa wanasiasa pia ni jipu kwa wanasiasa.!
Kweli kabisa. Machinga anahitaji sehemu yenye soko kufanya biashara yake. Kule hawakai maana biashara hamna!
 
Hongera sana Meya ila pia inabidi serikali wasimamie kwa nguvu zote kuhakikisha hawarudi k'koo na pia waboreshe mazingira ya pale wanapoamia yawavutie wateja.
 
Back
Top Bottom