Meya wa Kigoma Ujiji: Nachukulia tishio la Waziri Mkuchika kama tangazo la vita dhidi ya watu wa Manispaa yetu

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
605
1,536
Kauli ya Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kufuatia tishio la Serikali kuvunja Manispaa yetu

Nimeshtushwa, kushangazwa na kuchukizwa na tishio la kuivunja Halmashauri ya Manispaa ambalo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa leo bungeni. Waziri wa Utawala Bora alikuwa anajibu swali la mbunge wetu wa Kigoma Mjini kuhusu uamuzi wa Serikali kujitoa katika Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa uwazi ( OGP ). Waziri George Mkuchika ameionya Manispaa yetu kuwa isipojitoa OGP itavunjwa na badala yake kuundwe Tume ya Manispaa.

Nikiwa Meya wa Manispaa hii nachukulia tishio hili la Waziri kwa uzito mkubwa na ni tangazo la vita dhidi ya watu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji. Mnamo mwezi Februari mwaka 2016 Manispaa yetu ilishindana na Miji mingine 45 duniani kuchaguliwa kuwa waanzilishi wa program ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa kwa uwazi. Miji 15 ilichaguliwa ikiwamo Manispaa yetu. Shindano hili halikuwa na mahusiano yeyote na uanachama wa Tanzania kwenye OGP. Hivyo Manispaa yetu ilijiunga na OGP kwa kujitegemea na wala hatukuhitaji hata barua ya Serikali Kuu kutuidhinisha.

Serikali kutulazimisha kujitoa kwa sababu tu wenyewe wamejitoa ni kinyume cha demokrasia, kutuingilia mambo yetu na ni njama za kutukwamisha kwa sababu za kisiasa. Manispaa yetu inapata faida kubwa kuwa mwanachama wa OGP SubNational. Watendaji wetu wamejengewa uwezo, idara yetu ya ardhi inawezeshwa vifaa vya kisasa vya kuhifadhi kumbukumbu za wamiliki wa ardhi na kuondoa kabisa migogoro ya ardhi kwenye manispaa, wananchi wanapata taarifa za mapato na matumizi ya manispaa yao kwa kuweka wazi kila fedha inayoingia na taarifa ya robo mwaka ya ukaguzi wa ndani ( www.kigomaujijimc.go.tz ). Vile vile tumeweza kujenga mtandao wa mahusiano na Miji kama Bojonegoro wa Indonesia, Madrid ya Hispania, Paris ya Ufaransa, Ontario ya Canada na Sekondi Tokoradi ya Ghana. Kuwa kwenye OGP SubNational kumewezesha watu wenye mitaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia kutaka kuwekeza kwenye Manispaa yetu.

Mfano kesho Manispaa inaingia makubaliano na kampuni ya LingHang Group ya kuwekeza Kituo cha Biashara cha Maziwa Makuu ( The Ujiji City ) na Kiwanda cha Samaki cha Katonga. Vile vile kampuni ya HITACHI ya Japan inawekeza kuzalisha umeme wa jua kuendesha mitambo ya Maji kwenye manispaa, uwekezaji wa Utalii wa matibabu ( medical tourism) nk.

Kwa hakika kutulazimisha kujitoa OGP ni kupunguza nafasi yetu ya ushawishi duniani. Nikiwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, nimefanya juhudi za kuwasiliana na Serikali Kuu ili kupata ufafanuzi na kuitaka Serikali ituache tuendelee kutekeleza Mpango Mkakati wetu wa OGP. Hata hivyo Serikali haikunipa majibu yeyote mpaka leo tuliposikia Bungeni tukionywa kuacha kuwasiliana na watu wa OGP.

Tunashangazwa na hatua hii ya Serikali inayojitanabaisha kwa kupambana na ufisadi. Uwazi ni dawa endelevu dhidi ya ufisadi. Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji litakaa na kujadili suala hili na kufanya maamuzi yenye kujali maslahi mapana ya Mji wetu.

Hussein Ruhava
Meya Manispaa Kigoma Ujiji
13/11/2017
 
Uwekezaji toka nje ya nchi unafanywa na manispaa bila kushirikisha serikali kuu? Hao wawekezaji waweza ingia kinyemela mikataba na Manispaa bila kupitia kituo cha uwekezaji wala bila wizara ya biashara na viwanda kuhusika?
 
tatizo Zitto kuendesha manispaa anafikiri ameshakuwa rais wa sehemu ile nchi imeshajitoa walichokuwa wanatakiwa kufanya ni kujenga ushawishi ili nchi ibadili maamuzi na sio kushindana na serikali kuu
 
Mi Naomba kujua tu kama Serikali kuu au Manispaa isipofuata Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa uwazi (OGP) itakua inafuata Mpango Gani mwengine??

Yaani nini maudhui ya hii Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa uwazi (OGP) na nini yasisyo maudhui yake pia?? Ina maana serikali inataka kua inaendesha mambo yake kwa kuficha ficha zaidi kuliko kuweka wazi?? Naomba alieelewa anieleweshe please
 
Uwekezaji toka nje ya nchi unafanywa na manispaa bila kushirikisha serikali kuu? Hao wawekezaji waweza ingia kinyemela mikataba na Manispaa bila kupitia kituo cha uwekezaji wala bila wizara ya biashara na viwanda kuhusika?
Swali fikirishi. Serikali iangalie hili swala kwa mapana yake sio kupanic na kutoa matamko yatayoikosesha fursa Kigoma kwa sababu zisizo na msingi
 
Kauli ya Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kufuatia tishio la Serikali kuvunja Manispaa yetu

Nimeshtushwa, kushangazwa na kuchukizwa na tishio la kuivunja Halmashauri ya Manispaa ambalo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa leo bungeni. Waziri wa Utawala Bora alikuwa anajibu swali la mbunge wetu wa Kigoma Mjini kuhusu uamuzi wa Serikali kujitoa katika Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa uwazi ( OGP ). Waziri George Mkuchika ameionya Manispaa yetu kuwa isipojitoa OGP itavunjwa na badala yake kuundwe Tume ya Manispaa.

Nikiwa Meya wa Manispaa hii nachukulia tishio hili la Waziri kwa uzito mkubwa na ni tangazo la vita dhidi ya watu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji. Mnamo mwezi Februari mwaka 2016 Manispaa yetu ilishindana na Miji mingine 45 duniani kuchaguliwa kuwa waanzilishi wa program ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa kwa uwazi. Miji 15 ilichaguliwa ikiwamo Manispaa yetu. Shindano hili halikuwa na mahusiano yeyote na uanachama wa Tanzania kwenye OGP. Hivyo Manispaa yetu ilijiunga na OGP kwa kujitegemea na wala hatukuhitaji hata barua ya Serikali Kuu kutuidhinisha.

Serikali kutulazimisha kujitoa kwa sababu tu wenyewe wamejitoa ni kinyume cha demokrasia, kutuingilia mambo yetu na ni njama za kutukwamisha kwa sababu za kisiasa. Manispaa yetu inapata faida kubwa kuwa mwanachama wa OGP SubNational. Watendaji wetu wamejengewa uwezo, idara yetu ya ardhi inawezeshwa vifaa vya kisasa vya kuhifadhi kumbukumbu za wamiliki wa ardhi na kuondoa kabisa migogoro ya ardhi kwenye manispaa, wananchi wanapata taarifa za mapato na matumizi ya manispaa yao kwa kuweka wazi kila fedha inayoingia na taarifa ya robo mwaka ya ukaguzi wa ndani ( www.kigomaujijimc.go.tz ). Vile vile tumeweza kujenga mtandao wa mahusiano na Miji kama Bojonegoro wa Indonesia, Madrid ya Hispania, Paris ya Ufaransa, Ontario ya Canada na Sekondi Tokoradi ya Ghana. Kuwa kwenye OGP SubNational kumewezesha watu wenye mitaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia kutaka kuwekeza kwenye Manispaa yetu.

Mfano kesho Manispaa inaingia makubaliano na kampuni ya LingHang Group ya kuwekeza Kituo cha Biashara cha Maziwa Makuu ( The Ujiji City ) na Kiwanda cha Samaki cha Katonga. Vile vile kampuni ya HITACHI ya Japan inawekeza kuzalisha umeme wa jua kuendesha mitambo ya Maji kwenye manispaa, uwekezaji wa Utalii wa matibabu ( medical tourism) nk.

Kwa hakika kutulazimisha kujitoa OGP ni kupunguza nafasi yetu ya ushawishi duniani. Nikiwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, nimefanya juhudi za kuwasiliana na Serikali Kuu ili kupata ufafanuzi na kuitaka Serikali ituache tuendelee kutekeleza Mpango Mkakati wetu wa OGP. Hata hivyo Serikali haikunipa majibu yeyote mpaka leo tuliposikia Bungeni tukionywa kuacha kuwasiliana na watu wa OGP.

Tunashangazwa na hatua hii ya Serikali inayojitanabaisha kwa kupambana na ufisadi. Uwazi ni dawa endelevu dhidi ya ufisadi. Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji litakaa na kujadili suala hili na kufanya maamuzi yenye kujali maslahi mapana ya Mji wetu.

Hussein Ruhava
Meya Manispaa Kigoma Ujiji
13/11/2017
Hii habari imenifanya nimkumbuke mchora katuni wa Kenya, Gado, alimchora Magufuli anakimbia, ila ukimtazama huwezi kujua anakimbia kwenda mbele au kurudi nyuma...
 
Swali fikirishi. Serikali iangalie hili swala kwa mapana yake sio kupanic na kutoa matamko yatayoikosesha fursa Kigoma kwa sababu zisizo na msingi
Hili sio tamko, Serikali imeulizwa swali na wana Kigoma na hill ndio jibu la serikali. Mlitaka jibu LA keremba? Ukweli ndio huo, Serikali ilijitoa na watoto mpaka vitukuu wanatakiwa kujitoa, ndio kanuni ya mkataba. Wana Kigoma wanahaki ya kumshawishi baba madhara ya kujitoa lakini sio kutunisha musuri kama majibu ya Meya.
 
tatizo Zitto kuendesha manispaa anafikiri ameshakuwa rais wa sehemu ile nchi imeshajitoa walichokuwa wanatakiwa kufanya ni kujenga ushawishi ili nchi ibadili maamuzi na sio kushindana na serikali kuu

Tatizo la upinzani Tanzania hawajui kitu kinaitwa how to manage your boss to be in your favor.Management skills and tactics wako zero.They are very poor in negotiations and persuasion skills.angalia akina lema,,

Msigwa walivyo hujiita maraisi walipo kwenye majimbo yao!!! Kutwa confrontation na their bosses wakuu wa wilaya,mikoa na raisi hivi kuna kitu kitaenda bila collaboration na serikali?

Zitto anajitambulisha kuwa anasoma vitabu vingi sana lakini naona anasoma vitabu vya kibwege ambavyo havimsaidii
 
Hili sio tamko, Serikali imeulizwa swali na wana Kigoma na hill ndio jibu la serikali. Mlitaka jibu LA keremba? Ukweli ndio huo, Serikali ilijitoa na watoto mpaka vitukuu wanatakiwa kujitoa, ndio kanuni ya mkataba. Wana Kigoma wanahaki ya kumshawishi baba madhara ya kujitoa lakini sio kutunisha musuri kama majibu ya Meya.
unawezq kutuelezea sababu za kujitoa?
kwanini kila kitu wanataka kifanyike gizani? bunge gizani, magazeti gizani, mitandao isieleze wananchi kinqchojiri, kivuko cha bagamoyo gizani, uwanja wa chitto gizani na ukihoji unapata pyu pyu pyu! why????
 
Mkuchika ametoa sababu ya kujitoa, Canada ni mdau wa maendeleo, Tanzania ofisi za Ubalozi Canada, na wote ni wanachama wa Comonweath, shughuli zote za OGP zinaweza kufanyika chini ya "umbrella" ya mahusiano hayo
 
Back
Top Bottom