MEYA WA JIJI............!!

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,527
865
kwanza nikupongeze kwa kushinda udiwani kata ya Vijibweni kupitia Chadema(ukawa), hatimaye kushinda kiti cha Umeya wa jiji kubwa. pamoja na pongezi zangu, nakukumbusha kwa nafasi yako hiyo unawajibu wa kusimamia ahadi alizokuwa akizinadi mgombea nafasi ya Urais kupitia UKAWA. moja ya ahadi hizo ni kuwaangalia vijana wa bodaboda na akina mama ntilie......manyanyaso yameanza hususani kupitia jeshi la polisi. vijana wanakamatwa , wanatozwa faini na wala hawapewi risiti. ni shida kwa kweli.
 
Suala la Bodaboda ni gumu sana, kuna majambazi, wanasababisha ajali wao halafu wanaleta vurugu n.k. yeye tunataka azisimamie sheria zilizopo kwa ukamilifu
 
usije kuamini maneno ya wanasiasa hasa hawa wa chama kile kinachoanzia na cha......
 
Yapo mambo ambayo kama Meya atayatekeleza atakuwa amekonga nyoyo za watu wengi saana na hii itamfanya awe mfano wa kuigwa. Zipo kero amabazo zimeota mizizi na zinatakiwa zipatiwe ufumbuzi bila kuangalia utashi wa kisiasa. Kero kwa mfano hii ya bodaboda, wamachinga, uchafu, madawati, nk. Hizi akikaa chini na kutoa majibu yake atakuwa amesaidia sana wana Dar. Mameya waliopita aidha walikuwa hawajitoi sawasawa katika kushughulikia hizo kero. Sasa ni wakati wa UKAWA kuonyesha yaliyoshindikana yanawezekana!
 
Back
Top Bottom