Meya wa Jiji Mwanza, Wabunge wa Nyamagana, Ilemela wanyimwa taarifa ya kwenda kuwahamisha Machinga

Hivi police si wameelekezwa kupiga risasi miguuni?(KAMA IMEBIDI) Sasa aliyepigwa kichwani Police walikuwa wanataka nini?! Hata hvyo cjaunga mkono kuchoma gari la yule jamaa aliyeonekana analia kwenye Tv jana.

Nimeona kazi kweli kweli.
 
inawezekana huu ni mpango-mkakati wa ccm kuiletea chadema picha mbaya kwa jamii. Inakuwaje wafikie uamuzi huo bila kushirikisha ofisi ya meya na wabunge. Halafu jana namsikia naibu waziri wa mambo ya ndani anasema halmashauri ya mwanza inaongozwa na chadema, sielewi alikua anamaanisha nini hapo.
 
Ukweli ni mpango mkakati wa kuwachonganisha viongozi wa chadema na wananchi hili chadema lazima walikemee na waishitaki CCM na serikali yake kwa wananchi bila kumung,unya maneno,hizi ni dharau kubwa kwamba Meya anaweza kufichwa operesheni inayofanyika kwenye himaya yake ,nadhani pia CCM ishitakiwe katika jumuiya za kimataifa

Wakati huo huo wananchi wanapigwa risasi,wao walikuwa wakiburudika mnazi mmoja na kupiga mafataki,thanks God hata magazeti hayakujali hata hizo mbwembwe zao za kujimwaga mwaga kwa kutumia kodi za wananchi watu wanajistareheshe wakati wilaya 20 hazina chakula watu wanalala kwa kula mizizi
 
Where is FaizaFoxy?? Maana jana wakati watu wanapigwa risasi amewakejeli eti Mwanza inaongozwa na CHADEMA. Aseme sasa ni CHADEMA waliowapiga watu risasi. CCM ni Jehanam ya Tanzania, chama cha majini hiki. Ndo maana wanataka damu zetu kila kuchwapo.
anataka umaarufu tu huyo
 
Hivi police si wameelekezwa kupiga risasi miguuni?(KAMA IMEBIDI) Sasa aliyepigwa kichwani Police walikuwa wanataka nini?! Hata hvyo cjaunga mkono kuchoma gari la yule jamaa aliyeonekana analia kwenye Tv jana.
Jamani mbona wanasema hakuna wa2 waliuwawa? Ama wanaficha kwa sababu gani?
 
Taarifa nilizonazo mimi ni kwamba wamefariki watu si chini ya wanne
miili iliyoonekana ni minne ikitambulika namna hii, muhindi mmoja, askari mmoja na raia wawili.

Poleni sana Mwanza, na ninawaombea busara na hekima zitawale katika harakati
za kupata ukweli wa nini kilisababisha haya na majibu yake.
 
Nimepita nimeona vioo vya maduka viko chini,hongereni CCM na polisi wenu lakini............................
 
Jamani tupeni full story maana naona virakaraka tu humu JF hamna full story.

1.Je nini has kimetokea?
2.Nini chanzo cha ke?
3. Je police wameua na kuawa tena?
4. Nini kinaendelea sasa?
 
Jamani wahurumieni hawa maskini, mbona hawana wa kuwasemea? serikali sasa tunataka kuwambia kuwa unyama unatosha...vinginevyo jiandaeni kunyolewa na umma wa watanzania
 
Polis jijin mwanza jana walipambana na wamachinga,wamachinga walikuwa wakiwarushia mawe polis wakat walipotakiwa kuhama maeneo yao ya awali waliyokuwa wakifania biashara zao,baada ya polisi kuanza kuwapiga nao wakaanza kurusha mawe,hivyo vurugu kubwa zikazuka,polisi wametumia risas za moto kutuliza ghasia hizo.......kwa maelezo zaidi angalia mitandao ya magazeti ya leo au blogs kama vle www.gsengo.blogspot.com.......
Jamani tupeni full story maana naona virakaraka tu humu JF hamna full story.1.Je nini has kimetokea? 2.Nini chanzo cha ke?3. Je police wameua na kuawa tena?4. Nini kinaendelea sasa?
 
nimetoka kusikiliza taarifa ya habari ya saa 2 usiku huu tbc, SIRRO anasema watakaa chini na wamachinga kutafuta muafaka na ktk fujo hizo hakuna aliyeuwawa, na polisi hawakumpiga mtu hata mmoja na hivyo basi sasa wanachunguza chanzo cha hayo majeraha

my take: i cant believe it.. may be all those injuries were caused by natural force
 
Hivi viongoz wanaohubiri amani kila siku huwa wanamaanisha wanachokisema au? Na tena imekuja tabia nyingine ya kuhusisha kila jambo na siasa,utasikia 'wanasiasa waache kuingilia mambo,' mara ooh utasikia,'kiongozi mmoja wa chama cha siasa anatumika kuchochea vurugu'! Hivi kiongoz wa serikali (waziri,mkuu wa mkoa/wilaya) au chombo cha dola wanaposema maneno haya huwa wanamlenga nani? Je wanakua specif kwa vyama fulan vya upinzan huku wao wakijiweka kando kana kwamba wao si wanasiasa,wanamwonyesha nani unafiki wao! Sasa hao waheshimiwa waliofanya maamuzi kwa kubagua upande mmoja,wanamkomoa nani? Hivi wanataka wananchi waamini kwamba wao ndio pekee wanaostahili kuongoza! Imefikia wakat wanasiasa waheshimu utu wa watu kwani kuishi ni haki ya kila mtu. Kwa tukio hilo wanataka tuone kwamba wapinzani hawana uwezo wa kuongoza,kwa faida ipi? Mbona uzalendo unapewa kisogo kwa ajili ya ulevi wa siasa za kipumbavu? Najiuliza Hivi kweli kwa style hii hata siku wananchi wakiamua kukipumzisha chama tawala cha sasa na kuamua kwa kura kukipa dhamana hio chama kingine,watakua tayari kukabidhi ofisi kwel? 'TUNAJENGA BOMA MOJA, YANINI BASI FITO TUZIGOMBANIE.' tena kwa kuwafanyia wenzenu fitina ili mpendwe?! Tunatia aibu kama nchi inayoaminika kimataifa kwa kuwa kisiwa cha amani kwa sababu za kipumbavu eti fulan afanyiwe fitina akomolewe aonekane hafai! Kumbuken mko kwenye hizo ofisi na vyeo vyenu kwa sababu wananchi wananchi wamewaamini! CCM+CDM Upinzani wenu upelekeni majukwaaani na si kuleta majanga kwa watu tusiohusika na migogoro yenu! Tunachotaka ni maendeleo wether kiongozi ni ccm,chadema au wote wawili kwa pamoja. Tofaut zenu zisipoteze malengo yetu ya kuishi tanzania yenye kutiririsha maziwa+asali!..! WANASIASA MNAKERAAA!!
 
Huo ni uvunjaji wa haki za kibidamu.Kwanini watumie risasi za moto kwa watu wasio na silaha moto?kwanini wasitumie risasi za pulastiki?Tunaomba jumuiya ya kimataifa iuangalie huu unyama unaoendelea Tanzania.Ikiwezana serikali ya CCM ishitakiwe kwenye mahakama ya kimataifa.kwani unyama huu ni swawa ule unaofanywa na Gadaff kule Libiya. CCM wanauwa watu wasikuwa hatia,hii nikuwaogopesha watu wasiendelee kudai haki zao.Jk ukae ukijuwa damu ya mnyonge haimwagiki bure,punde utatafuta pa kukimbilia.Tumechokaaa.
 
Meya wa jiji la Mwanza kwa tiketi ya CDM aruhusu machinga kuendelea kufanya biashara kwenye eneo ambalo polisi waliwatimua kwa mabomu na risasi. Asema yeye hana taarifa ya kutimuliwa kwa wapiga kura wake na yeye ndiye mkuu wa jiji.
Polisi wakana kupiga watu Risasi wasema risasi zilizopiga raia wasio na hatia ni za askari wa jiji.
 
Kwa maoni yangu, CCM inaleta kwa makusudi kabisa vurugu ktka maeneo yote yaliyoko chini ya uongozi wa chadema. Miaka ya nyuma walivunja mabomba karatu wakaleta vurugu, Ubungo walileta vurugu baada ya Mnyika kushinda pale karibu na national house, Arusha majuzi na sasa wamehamia mwanza. Hizi vurugu zinalengo la kuwaaminisha watanzania kwamba kila mahali panapoongozwa na chadema ni vurugu tu. Hivyo, kuwaaminisha watz kuwa, chadema ni chama cha vurugu. We must think outside the box as Chadema.
 
Back
Top Bottom