Meya wa Jiji Mwanza, Wabunge wa Nyamagana, Ilemela wanyimwa taarifa ya kwenda kuwahamisha Machinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meya wa Jiji Mwanza, Wabunge wa Nyamagana, Ilemela wanyimwa taarifa ya kwenda kuwahamisha Machinga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Jul 7, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mwanza, Francis Mkambenga, alisema hali ilikuwa tete na kwamba operesheni hiyo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya kuwaondoa machinga katika eneo hilo la msikiti na shule eneo la Makoroboi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Mkambenga, alisema operesheni hiyo ilikuwa na baraka zote za jiji huku Meya wa jiji hilo, Josephat Manyerere, alisema hana taarifa kutoka ofisi ya mkurugenzi.
  “Mkurugenzi ana dharau fulani, pengine ana nia ya kunikomoa mimi na chama changu cha CHADEMA,” alisema Manyerere.
  Manyerere alisema wakati yeye akifichwa taarifa za kuwapo kwa operesheni hiyo, taarifa hizo zilipelekwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa.
  Aliongeza kuwa ofisi za wabunge wa Jiji la Mwanza, Ilemela na Nyamagana nazo zilinyimwa taarifa hizo kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
  “Ninalaani operesheni hii haramu, maana imefanywa bila kujulishwa ofisi yangu ya meya. Hapa inaonekana mkurugenzi anataka kunikomoa mimi kama meya na chama changu cha CHADEMA tunaoongoza jiji hili. Hii ni dharau inayofanywa na ofisi ya mkurugenzi kuninyima taarifa muhimu kama hizi,” alisema Meya Manyerere. Meya huyo aliwataja watu waliojeruhiwa na kulazwa katika hospitali za Sekou Toure na Bugando kuwa ni Omari Abdallah, Juma Machumu, Calvin Jeremiah, Brayen Pastori, Kulwa John (amepigwa risasi kichwani), Medard Benard na Dotto Thomas, na kwamba majeruhi wawili kati ya hao wamelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU), katika Hospitali ya Bugando (BMC).

  Source. Tanzania Daima
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Haya sasa!
  Thanksgod hawakupewa taarifa, maana unyama uliofanyika si wa aina ya cdm!
  Acha waendelee kunywa damu, wamezowea hawa!
   
 3. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nadhani huyo mkurugenzi amevuna alichopanda
   
 4. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii inasikitisha sana, kwa nini CCM wanaona wao ndio watanzania zaidi ya wengine? Hizi siasa za kimangimeza ndio zinaliharibu bara la Afrika. Vyama vya siasa sio vita ni itikadi na falsafa tofauti za uongozi. Ni maono tafauti tu. CCM wakubali hawawezi kuwa na vision sawa na CDM, wawaachie CDM jiji lao waongoze watu wake.
   
 5. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi police si wameelekezwa kupiga risasi miguuni?(KAMA IMEBIDI) Sasa aliyepigwa kichwani Police walikuwa wanataka nini?! Hata hvyo cjaunga mkono kuchoma gari la yule jamaa aliyeonekana analia kwenye Tv jana.
   
 6. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Where is FaizaFoxy?? Maana jana wakati watu wanapigwa risasi amewakejeli eti Mwanza inaongozwa na CHADEMA. Aseme sasa ni CHADEMA waliowapiga watu risasi. CCM ni Jehanam ya Tanzania, chama cha majini hiki. Ndo maana wanataka damu zetu kila kuchwapo.
   
 7. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  huyu mkurugenzi ndiye aliyempiga chini Wenja ili MASHA apite bila kupigwa kama hasipoondolewa hapo mwanza hali itakuwa ya uhasama
   
 8. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Busara ingetumika yote hayo yasinge tokea. Tanzania inatatizo kubwa la kuajiri wafanyakazi bila ujuzi. Madhara yake ni nguvu nyingi bila tija. Nchi yenyewe bima kitim tim, unasababisha uharibifu wa mali, na kujeruhi watu kwa mambo yanayozungumzika. Utasikia sasa tukae chini tuzungumze na wamachinga.
   
 9. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magamba watumie busara wawaache cdm wafanye kazi tuliyowapa cc wapigakura ili tuwapime vizuri after 5yrs
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nafikiri madiwani wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Mkurugenzi na kisha kumng'oa. Naweza sahishwa kama siko sahihi.
   
 11. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,

  CCeM Lazima waondoke madarakani, Kanda ya ziwa hatuwataki kabisa.

  Sisi hatuwambui hao wakuu wa wilaya na mkoa maana ni watumishi wa CCeM
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli na huyu Mkurugenzi akaendelea kuachwa, then imani yangu iliyobaki chembe itapotea kabisa. Maana nitaamini zaidi ya jeuri yake, wapo wengine juu wanaomuongoza kwa remote. Kwanini amruke bosi wake wa karibu na akimbilie Wilayani na Mkoani ambao ni chama kimoja? Kwani yeye/ama Meya nk wanaongoza jiji kwa kufata wanachama tu. Kweli siasa yetu bado ni changa sana katika kuhudumia wananchi.
   
 13. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,276
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  atakuwa anaongozwa kwa remote,hivi kwa nini police wa kibongo ni matriger happy sana?kwani hawana anymeans ya kutuliza riot.
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,000
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  sasa nionavyo huu uonevu utafikia mahala wananchi hawatavumilia, polisi na CCM wajiandae kupokea tsunami au kimbunga cha mapinduzi, hata kondoo akichoka kuvumilia hutumia bichwa lake kuondoa hasira dhidi ya adui yake.
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM imesha lewa madaraka na kwa taarifa wanajiumiza maana hasira za wapiga zinakuwa juu zaidi .Sasa wategemee kuvuna wanachopanda sasa .Uchaguzi hauko mbali .
   
 16. i

  ichawinga Member

  #16
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sas huyo mkurugenzi tuone atafanywa nini, na asipoadabishwa tutamwadabisha sisi, hii nchi ni kama ya watu fulani tu na siyo ya watz wote jamani tuvumilie mwisho tuseme basi nakumbuka siku moja nilikuwa naangalia tv CNN mwandishi akamuuliza mwandamaji nchini LIBYA kuwa GADAFF asipo toka madalakani atafanya nini akasema yupo tayali kufa hadi ahakikishe huyo rais wao anatoka madarakani.. sasa watanzania kazi kwenu.
   
 17. M

  MPG JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu KABWE mkurugenzi wa wa mwanza ni kada wa CCM na hafai kuwa mkurugenzi,yeye ndiyo chanzo cha vurugu MWANZA,amekuwa chanzo cha furugu muda wote katika jiji la mwanza,eheee MUNGU tuepushe na dhuruma hii ya CCM.
   
 18. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Huyu mkurugenzi kwa nini hakutoa taarifa ktk ofisi husika Kama maelekezo yanavyotaka!?.Haya makusudi sio mazuri ona sasa maisha ya watu yameingia doa na hii ni chuki inazi kupandwa kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Poleni sana kwa tukio hilo ila kwanza nataka kuujurisha Umma
  Mkurugenzi wa jiji ni Mwajiliwa kwa madiwani wote wa eneo husika kwaiyo Mayor na madiwani ndio Maboss wa Mkurugenzi sasa sielewi hawa wakurugenzi sasa iwe ni ajira ianayo tangazwa na sio kuteuliwa na Rais.

  Matatizo kama haya sasa yanafanyika office ya usalama mkoa inakubaliana na hali hii jamani ivi hata hawa police hawawezi elewa kufanya hivyo ni kuleta vurugu ndania ya jiji na mnajenga taswila gani hawa wananchi siku hizi wanajua mambo mampya sio kama zamani wanaburuzwa na wanajua fika makosa yalifanyika wapi na nani alipaswa kuwajibika sasa viongozi wa juu wanajaribu kuwa fichia viongozi wenzao maovu si haki eneo la makoroboi tokea mimi niko nasoama Lake & Nyanza Primary School ilo eneo lilikuwepo na watu wakhamishiwa mlango mmoja na hapo makoroboi pakabaki eneo wazi na kukawa na mwananchi Hospital na majumba ya wahindi i mean msikiti wa baniani hapo, sasa hilo eneo serikali wanatakia nini nadhani ni bora liwe eneo la wazi tuuuu patengenezwe gardeni au eneo la watoto kucheza period tusitafute ubaya na wananchi jamani khaaa.

  Ni muda wa kuijenga mwanza yetu sasa na sio kuleta zile si ha sa kama za Arusha ambako vigogo wengi wa serikali wameamisha vikao vingi na kuvipeleka Dodoma kwa kisingizio ati twajiandaaa kuwa makao makuuu kumbe ni Political interest imewafanya kukimbia mji wa Arusha.

  Watu wa mwanza ni muda mwafaka wa kutopelekwa pelekwa na viongozi wenye interest zao katika maeneo ya jiji letu, twatakiwa kuijenga Rock City now iwe ndio jiji la kiuchumi tuna resorce nying za kumwaga sasa hawa viongozi wanaletwa kuja kutuharibia ndio wa kuwapinga na kuwakataaa.
   
 20. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  atakuja baadae kidogo, muda huu kaenda kuvunja jungu na naniii!!!
   
Loading...