Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire ashikiliwa na Polisi kwa amri ya RC John Mongella

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,758
71,136
Meya Mwanza akamatwa asimwage mboga mbele ya Rais Magufuli

By Moses C. N

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire amekamatwa na jeshi la Polisi, baada ya kubainika kwamba katika salamu zake kwa Rais John Magufuli katika uzinduzi wa kiwanda cha Sayona kilichopo Nyakato Ilemela jijini Mwanza, atatoa siri za ufisadi uliofanyika katika kiwanda hicho.

Wanaotajwa kufanya ufisadi huo ni mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kibamba na viongozi wengine wa mkoa huo. Pia viwanda vya kampuni hiyo vimekuwa vikituhumiwa kuwanyanyasha wafanyakazi wake wengine wakitimliwa kazi bila kulipwa stahiki zao.

Baada ya kamati ya Ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza chini ya John Mongella kubaini kwamba Meya huyo anataka kumwaga ukweli mbele ya rais, inadaiwa aliliagiza jeshi la Polisi kumkamata kiongozi huyo ambaye kwa kipindi kifupi ameonekana akifichua uchafu unaofanyika katika jiji la Mwanza.

COPY AND PASTE...
Jee kuna ukweli wowote hapo? Na kama ni kweli CCM itakuwa salama Mwanza?
===========================================

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi ikidaiwa ni kutokana na agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella.

Hata hivyo, Mongella amekana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza.

Mariam Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na meya Bwire amesema kuwekwa kwake ndani kunatokana na agizo la mkuu wa mkoa.

“Nimepata taarifa za meya kuwekwa mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua kinachoendelea,” amesema Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017.

Taarifa zinasema meya Bwire amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais John Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo.

Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.”

Tangu Aprili, Bwire na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba wamekuwa katika mgogoro kila upande ukiutuhumu mwingine kuhujumu shughuli za maendeleo. (Imeandikwa na Jonathan Musa, Ngollo John na Saadam Sadick)

CHANZO: Mwananchi
 
Breaking news

Meya Mwanza akamatwa asimwage mboga mbele ya Rais Magufuli

By Moses C. N

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire amekamatwa na jeshi la Polisi, baada ya kubainika kwamba katika salamu zake kwa Rais John Magufuli katika uzinduzi wa kiwanda cha Sayona kilichopo Nyakato Ilemela jijini Mwanza, atatoa siri za ufisadi uliofanyika katika kiwanda hicho.

Wanaotajwa kufanya ufisadi huo ni mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kibamba na viongozi wengine wa mkoa huo. Pia viwanda vya kampuni hiyo vimekuwa vikituhumiwa kuwanyanyasha wafanyakazi wake wengine wakitimliwa kazi bila kulipwa stahiki zao.

Baada ya kamati ya Ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza chini ya John Mongella kubaini kwamba Meya huyo anataka kumwaga ukweli mbele ya rais, inadaiwa aliliagiza jeshi la Polisi kumkamata kiongozi huyo ambaye kwa kipindi kifupi ameonekana akifichua uchafu unaofanyika katika jiji la Mwanza.

COPY AND PASTE...
Jee kuna ukweli wowote hapo? Na kama ni kweli CCM itakuwa salama Mwanza?
Siasa inahusika vipi katika ukweli hapo... Na hayo ndiyo matatizo ya Kiafrika.

Yeye ni Meya wa Jiji unasubiri Rais ukashitaki. Wewe Meya ndiyo Mwenyekiti wa Council wa Jiji na una kamati zinakagua miradi yote ndani ya Jiji na kutoa ripoti.
 
Na bado! maCCM mtakaangana mpaka mkome
 
Siasa inahusika vipi katika ukweli hapo... Na hayo ndiyo matatizo ya Kiafrika.

Yeye ni Meya wa Jiji unasubiri Rais ukashitaki. Wewe Meya ndiyo Mwenyekiti wa Council wa Jiji na una kamati zinakagua miradi yote ndani ya Jiji na kutoa ripoti.
Kwa vile hujui historia ya mgogoro wa jiji ndio maana unaandika hivyo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom