Meya wa jiji la Dar: Zoezi la ukaguzi kila nyumba aliloagiza RC Makonda ni Batili

Status
Not open for further replies.

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Meya Wa Jiji:

Yafuatayo Ni muhimu Kwa wakaaz wa Jiji la Dar kufahamu kama haki yao ya msingi kabla ya utekelezwaji wa amri ya Mh Mkuu wa mkoa wa Dar wa kufanya msako kwenye makazi na nyumba zao.

Moja: Kwanza zoezi hili ni BATILI na haliwezi kutekelezeka kwenye Halmashauri zetu za Jiji la Dar es Salaam

Pili: Nawaomba sasa nielezee sababu ambazo nasema agizo hilo na zoezi hilo litakuwa BATILI :

A. Sheria ya makosa ya Jinai Inaelezea utaratibu wa kukaguliwa nyumbani kama search warrant ambayo inatolewa Na Mahakama au polisi, Na ambayo Inaelezea wanatafuta nini

B. Sheria hiyo pia inamtaka mwananchi kuwakagua maafisa wa Mahakama Na Polisi watakaofika Nyumbani kwake ili wasiweze kumpandikishia ushahidi wa uongo

C. Kamwe popote duniani Kibali cha wananchi kukaguliwa majumbani hakiwezi kutolewa Na Viongozi wa kisiasa.

D. Kwa maagizo hayo inasemekana wananchi watawekwa ndani Kwa kukataa kutii agizo hilo, hakuna sheria Tanzania inayoruhusu Mwananchi kuwekwa ndani kwa sababu za hovyo Kama hizo.

Naomba nimalizie Kwa kusema wananchi wote wa Jiji la Dar wawe na Amani kabisa na wajue haki zao na wajue kuzitetea, sisi viongozi wao tupo imara kusimamia haki zao na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Issaya Mwita Charles
Mstahiki Meya Jiji la Dar es Salaam
 
Asante Mungu kwa kutuletea Makonda katika jiji la Dar ambalo lina potential ya kura nyingi sana kwa upinzani iwapo RC huyu ataendelea hivi hivi.

Ni wazi hata zile kura chache walizopata katika uchagumzi mkuu uliopita,uchaguzi ujao wa 2020 kuzipata itakuwa ni ndoto

Naomba Makonda aendelee kubaki Dar mpaka 2020 na pia tupate tume huru ya uchaguzi.

Hata hivyo,kutokana na unyeti wa jiji hili katika uchaguzi,huyu bwana akiendelea hivi anaweza kuondolewa kabla ya 2020.Naamini wahusika bado wanasoma upepo kwa sasa kabla ya kufanya uamuzi.Hata wazee wa chama wanaweza kubeba jukumu la kumshauri mh.amuondoe.
 
Safi sana meya kwa kuweka ukweli wazi kama makonda alitaka kukamata wahalifu alitakiwa kwenda kwenye mitaa kuwaambia wenyeviti Wa mitaa wampe majina ya vijana wanaojiusisha na uhalifu Wa namna yoyote katika mtaa sio kusema wasiokuwa Na kazi haya matamko yazingatie Sheria
 
Meya Wa Jiji:

Yafuatayo NI muhimu Kwa wakaaz wa Jiji la Dar kufahamu kama haki yao ya msingi kabla ya utekelezwaji wa amri ya Mh Mkuu wa mkoa wa Dar wa kufanya msako kwenye makazi na nyumba zao.

Moja: Kwanza zoezi hili ni BATILI na haliwezi kutekelezeka kwenye Halmashauri zetu za Jiji la Dar es Salaam

jPili: Nawaomba sasa nielezee sababu ambazo nasema agizo hilo na zoezi hilo litakuwa BATILI :

A. Sheria ya makosa ya Jinai Inaelezea utaratibu wa kukaguliwa nyumbani kama search warrant ambayo inatolewa Na Mahakama au polisi, Na ambayo Inaelezea wanatafuta nini

B. Sheria hiyo pia inamtaka mwananchi kuwakagua maafisa wa Mahakama Na Polisi watakaofika Nyumbani kwake ili wasiweze kumpandikishia ushahidi wa uongo

C. Kamwe popote duniani Kibali cha wananchi kukaguliwa majumbani hakiwezi kutolewa Na Viongozi wa kisiasa.

D. Kwa maagizo hayo inasemekana wananchi watawekwa ndani Kwa kukataa kutii agizo hilo, hakuna sheria Tanzania inayoruhusu Mwananchi kuwekwa ndani kwasababu za hovyo Kama hizo.

Naomba nimalizie Kwa kusema wananchi wote wa Jiji la Dar wawe na Amani kabisa na wajue haki zao na wajue kuzitetea, sisi viongozi wao tupo imara kusimamia haki zao na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Issaya Mwita Charles
Mstahiki Meya Jiji la Dar es Salaam
Kibusara Mkuu wa Mkoa amekosea tuache ukada na hata the boss know this naninadhani ameshaonywa, kuwa wawazi Mkuu wa sasa wa mkoa uwenda atabadilishwa hilo halina shaka ni swala la muda tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom