Meya wa Jiji la Dar: Kupanda kwa tozo za maegesho si dhambi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari zenu wakuu,

Meya mwenye ushawishi mkubwa, Mstahiki Isaya Charles Mwita(CHADEMA) akihojiwa katika kipindi cha Joto la Asubuhi juu ya sintofahamu ya kuongezeka kwa tozo za maegesho katika viunga vya jiji la Dar amesema kuwa,

"Kupandisha shilingi 200 hadi kufikia shilingi 500 kwenye maegesho ya magari sio dhambi, tunataka kuijenga Dar es Salaam ambayo vyanzo vyake vikuu vya mapato ni sisi wana Dar es Salaam".
 
Makonda kwa hili la maegesho ingilia kati, shs 500 kwa saa ni kumkomoa mfanyakazi hiyo ni katibu na 5000 kwa Siku.. Kama lengo ni kupunguza magari mjini, Huyu Mkenya atafanya gazi gani?
 
Ni dhambi.....toka 300 hadi 500
Too much

Anyway

Ukiwa na kijigari nchi hii ni majanga kila mahali
 
Halafu kuna sehemu Kama sea clieff hao wa tiketi wanakaa mpk SAA nne usiku na hawana jumapili wala jumamosi
 
Gari ni starehe ndio watu tunaotakiwa kulipa kodi........

Sio kuumiza mama ntilie na machinga kila siku.........

Kama kodi inatumika vizuri tatizo liko wapi.......

Tusubiri mapato na matumizi kwenye CAG auditing kama zitakuwa zimetumika vibaya tutamburuza mahakamani meya........

Watanzania tunapenda kulia lia kila jambo.....
 
Nilimsikia jana akieleza juu ya 'Wakenya' waliopewa tenda, kwamba waliokuwepo walikuwa wanalipa kama 200m na hawa waeahidi 4billion!
Sijaelewa hii ni kipindi gani na kama ni kweli basi tutaumia lakini mwishoni huenda tukaona kitu. Maana kwa ratio hiyo wangesema ikipanfa hadi 500/- basi kampuni itoe million 600 labda kwa ongezeko hilo!
 
tulisema wapinzani wakipewa nafasi tutapata unafuu kumbe afadhali waliopita, kodi za majengo wamepandisha ili mradi ni balaa tupu
 
Hizo Kodi za maegesho.zimefanya nini cha maendeleo?ni sawa na ubungo wamepandisha mpaka 300.mule ndani cha maana hakunaaa.
 
mungu tunusuru na huyu meya maegesho ni jambo lakutazamwa sana mpaka hospitali unatozwa jamani tutaenda wapi?
 
Habari zenu wakuu,

Meya mwenye ushawishi mkubwa, Mstahiki Isaya Charles Mwita(CHADEMA) akihojiwa katika kipindi cha Joto la Asubuhi juu ya sintofahamu ya kuongezeka kwa tozo za maegesho katika viunga vya jiji la Dar amesema kuwa,

"Kupandisha shilingi 200 hadi kufikia shilingi 500 kwenye maegesho ya magari sio dhambi, tunataka kuijenga Dar es Salaam ambayo vyanzo vyake vikuu vya mapato ni sisi wana Dar es Salaam".
Huyu ni mkombozi Wa wanyonge kipenzi cha wote
 
Back
Top Bottom