Meya Wa Jiji la Dar es Salaam Kuyeko amjulia Hali Dkt. Massaburi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko Jana alimtembelea na kumjulia hali Mstahiki Meya mstaafu wa Jiji la Dar es salaam, Dkt. Didas Massaburi ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kuyeko alikutana na Mhe. Diwani wa Chanika (CCM), ndugu Ojambi Massaburi ambaye ndiye anamuuguza Babake.

Mbali na kumjulia hali Dkt. Massaburi, Mhe. Kuyeko pia alimtembelea Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) MKoa wa Geita, Kamanda Mwita Mhere aliyepata ajali wiki Jana Mkoani Dodoma. Mhere amelazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kitengo cha MOI akitibiwa majeraha yaliyokana na ajali alisema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri. Mhere pia alimshukru Mhe. Kuyeko kwa kuweza kutenga muda wake na kwenda kumuona hospitalini.

Aidha, Mhe. Kuyeko aliwapa pole wagonjwa hao aliowatembelea kwa kuwaombea kwa Mungu ili awaponye haraka na walejee kwenye majukumu yao ya kawaida ili tuendelee kulijenga taifa.
 

Attachments

  • IMG-20161011-WA0014.jpg
    IMG-20161011-WA0014.jpg
    71.1 KB · Views: 66
  • IMG-20161011-WA0015.jpg
    IMG-20161011-WA0015.jpg
    37.8 KB · Views: 64
Kuyeko ni wa Jiji au ni wa Ilala?
Upone haraka Didas Masaburi
 
Back
Top Bottom