Meya wa Iringa ang’olewa madarakani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Iringa. Wajumbe wa Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa nchini Tanzania wamemuondoa madarakani meya wa manispaa hiyo, Alex Kimbe.

Kimbe ambaye anatokana na chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema ameng’olewa madarakani leo Jumamosi Machi 28, 2020 katika kikao maalum cha madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa, mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Ryata amesema wajumbe waliohudhuria kikao ni 26 na kura 14 zimeridhia kumuondoa meya huyo.

“Ndugu zangu wajumbe, kura zilizopigwa ni 26, kura zilizoharibika ni 12, kura halali ni 14 na kura za ndio ni 14 na hapana ni kura zero (sifuri), hivyo Baraza la leo limepiga kura kihalali na taratibu zote zimezingatiwa,” alisema Ryata.

“Kuanzia leo Machi 28, 2020 Alex Kimbe hatakuwa meya hadi taratibu zitakavyofuata na baada ya kusema hayo naomba mkurugenzi uahirishe kikao” amesema.

Kabla ya kupiga kura mkurugenzi wa manispaa hiyo, Hamid Njovu alitoa utaratibu wa kupiga kura ya kumuondoa meya huyo.

Njovu alisema kura zinazopigwa ni za kumuondoa mustahiki meya madarakani baada ya tuhuma zake kuthibitishwa na tume ya uchunguzi.

“Kura zinapigwa kumuondoa mustahiki meya madarakani baada ya tuhuma zake kuthibitishwa na kamati ya uchunguzi” alisema Njovu akitoa maelekezo kabla ya upigaji kura.

Akiahirisha kikao hicho, Njovu amesema kama Kimbe hajaridhika na uamuzi huo, anaweza kukata rufaa kwa waziri wa Tamisemi.

Miongoni mwa tuhuma ambazo alikuwa anakabiliwa nazo Kimbe ni matumizi mabaya ya madaraka ikiwamo kufanya uamuzi bila kuzingatia kanuni za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri hiyo ikiwamo kutumia gari la halmashauri kwa matumizi yake binafsi.

Kimbe ameondolewa ikiwa ni miezi kama miwili imepita tangu Januari 9, 2020 Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kumng’oa Meya Isaya Mwita anayetokana na Chadema kwa tuhuma kama hizo za matumizi mabaya ya madaraka.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma > Iringa, baraza la madiwani laitishwa kumng'oa Meya, baada ya mahakama kutupa madai yake kwa kukosea vifungu vya pingamizi lake - JamiiForums
 
Huu ni ushauri ninaoupeleka kwa ccm Makao Makuu , kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Kwa DED wa Iringa Mjini .

Kwa kura halali za kumng'oa Kimbe kwenye umeya ccm Iringa Mjini haina uwezo wa kuzipata , njia pekee ya halali ni kuhakikisha Meya huyo anakufa kwa Uchawi au kwa Corona ama kwa njia nyingine yoyote mtakayoona inafaa
 
Mbon kila meya anaeondolewa niwa chadema!? Sjawahi kuskia meya wa ccm akiondolewa wakat wapo wengi nchini kuzidi hawa wa vyama pinzani ccm hawataki wapinzani washike nyazifa!?
 
Kuna mambo ambayo watu wanayafanya unajiulizaaaaa hadi hupati majibu, sasa unatumiaje madaraka yako ya umma kuwaondoa watu waliochaguliwa na umma?

Hivi huyo mtu mmoja tu akiwa hapo utakufaaaaa? Na Kwa nini unataka uchukue asilimia Mia moja Kwa kutumia nguvu? Ili iweje?

Daaaaah sijui tumefikaje hapa yani watu wanasikitika Sana na hiii hali Lakini ipo Siku tu hawa yatawakuta Kama yaliyomkuta logemarila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo matunda ya maridhiano ya CCM Kirumba!

Yule wa Dar hata chama chake hakikujishughulisha naye,kakubali matokeo na maisha yanaendelea.
 
Erythrocyte, Sasa aliekuambia juuu ya uhalali kwa nchi hiii katika kipindi hiki ni Nani? Hayo wanayohangaika nayo tu sio halal sembuse kwenye kura wanaweza kupiga za kumuondoa zikawa tano na za kukataa zikawa 20 Lakini wakabadilisha wakasema 20 ndio za kumuondoa na wasione aibu Au unadhani kuwa wanaaibu hao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mambo ambayo watu wanayafanya unajiulizaaaaa hadi hupati majibu, sasa unatumiaje madaraka yako ya umma kuwaondoa watu waliochaguliwa na umma? Hivi huyo mtu mmoja tu akiwa hapo utakufaaaaa? Na Kwa nini unataka uchukue asilimia Mia moja Kwa kutumia nguvu? Ili iweje? Daaaaah sijui tumefikaje hapa yani watu wanasikitika Sana na hiii hali Lakini ipo Siku tu hawa yatawakuta Kama yaliyomkuta logemarila

Sent using Jamii Forums mobile app
Dua la kuku...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa eti viongozi wakubwa nao wanaharibu kura.. Kumbe elimu ya kupiga kura inatakiwa itolewe kwa nguvu

-all is well-
 
Back
Top Bottom