Meya wa Ilala, Charles Kuyeko akutana na Jerry Silaa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Ni takribani mwaka mmoja sasa tangu Mhe. Charles Kuyeko (CHADEMA) kukalia kiti cha Meya wa Manispaa ya Ilala jana kwa mara ya kwanza amekutana uso kwa uso na mtangulizi wake ndugu Jerry Silaa (CCM) Meya mstaafu wa Manispaa hiyo.

Wawili hao wamekutana jana Jijini Dar es salam maeneo ya chanika katika msiba wa Dkt. Didas Massaburi aliyefariki jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Aidha, wawili hao hawakuwahi kukutana popote tangu Kuyeko kushikiria kiti cha Meya wa Ilala kutokana na kwamba Silaa alikaidi kufika ofisini ili kumkabidhi ofisi Mhe. Kuyeko. Hata hivyo, kitendo hicho hakikuzuia chochote kwa Mhe Kuyeko kuendelea na majukumu yake ya Umeya.

Hata hivyo, Slaa alipoona hakuna dalili ya kupata tena kiti cha Umeya alijaribu bahati kwa kugombea ubunge Jimbo la Ukonga ambapo pia aliambulia patupu na kutupwa mbali na Mbunge wa sasa Mhe. Mwita Waitara.

Mhe. Kuyeko alifika Msibani maeneo ya chanika (Chuoni kwake) majira ya saa 09:30 alasiri akiongozana na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita. Marehemu Massaburi anatarajiwa kuzikwa tarehe 17/10/2016 maeneo ya Chanika Jijini Dar es salaam.

IMG-20161014-WA0008.jpg

IMG-20161014-WA0011.jpg

IMG-20161014-WA0010.jpg
 
Mleta habari kaleta kinazi
Slaa aliposhindwa umeya akaamua kugombea ubunge!aidha hajui taratibu za uchaguzi mkuu au ameamua kuwalisha watu matango pori
 
Masaburi. Bwana..lowasa akiwa rais hatakaa wiki moja ikulu atakufa ...

Mungu apendagi ujinga
 
kutokA kwenye umeya hadi kwenye kuisomA nambA.InaonekanA hii itakuwA ni CHEMICAL CHANGE
 
Back
Top Bottom