Meya wa Ilala Aiongoza Kamati ya Fedha na Utawala Kutembelea Maeneo ya Uwekezaji

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mei 21,2016 siku ya jumamosi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala mhe. Charles Kuyeko aliiongoza kamati ya kudumu ya fedha na utawala ya baraza la Madiwani kutembelea maeneo ya uwekezaji yaliyoko Manispaa ya Ilala.

Katika ziara hiyo, mhe. Kuyeko aliongozana na Madiwani mbalimbali ambao ni wajumbe wa kamati ya fedha na utawala. Mbali na Madiwani, wataalamu wa idara mbalimbali pia waliongozana na kamati hiyo katika ziara ya kutembelea maeneo ya uwekezaji. Baadhi ya wataalamu hao ni mchumi wa Manispaa ya Ilala, mkuu wa Idara ya ardhi na mpango miji, mkuu wa Idara ya fedha na biashara, mkuu wa masoko na pia Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala.

Maeneo ya uwekezaji yaliyotembelewa na kamati hiyo ni eneo la kiwanja cha Mkunguni mkabara na soko la Kisutu, stendi ya zamani ya mabasi kisutu, eneo la wazi maeneo ya agha khan hospital, eneo la biashara ndogo ndogo kibasila, soko la karume/mchikichini, eneo la nyumba za Manispaa la mchikichini, soko la Ilala, soko la Buguruni,na eneo la nyumba chakavu za Halmashauri-ukonga.

Katika ziara hiyo, kamati ilikutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi wa maeneo husika. Changamoto/kero hizo zilielezwa na wadau na wafanyabiashara katika masoko ambayo kamati iliyatembelea. Baadhi ya changamoto/kero hizo ni miundombinu mibovu katika masoko, migogoro ya uongozi wa soko, ubadhirifu wa mapato, ada na ushuru kinyume cha sheria mdogo za uendeshaji masoko ya 2015.

Changamoto nyingine ni maeneo yanayomilkiwa na Manispaa ya Ilala kuendesha miradi isiyo rasmi na mapato yake kuingia kwenye mifuko binafsi.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo mhe. Kuyeko aliwaangiza wataalamu aliombatana nao kuwa wajiandae kuja na majibu ya kutosha juu ya kwa nini maeneo hayo hayajaendelezwa mpaka sasa licha ya kuwa kuna mikataba mbalimbali iliyosainiwa na wabia mbalimbali kwa ajili ya kuyaendeleza maeneo hayo.

Aidha, mhe. Kuyeko amewataka waje pia na majibu ya kutosha kuwa ni kwa kuna miradi hewa/isiyo rasmi katika maeneo ya Manispaa mpaka sasa? Je kwa nini kuna ubadhirifu katika masoko takribani yote ya Manispaa.

Wataalamu hao wanatakiwa kuwasilisha majibu hayo katika kikao cha kamati ya fedha na utawala kitakacho fanyika Leo jumatatu tarehe 24/05/2016.

Imetolewa Leo 23/05/2016
Na Alex Massaba,
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala.
 

Attachments

  • IMG-20160523-WA0028.jpg
    IMG-20160523-WA0028.jpg
    75.7 KB · Views: 22
Mimi sijaelewa umesema alikuwa anafanya ziara au matembezi au kitu gani yaani maana yangu ni kuwa nini faida ya ziara hiyo kwa wananchi
 
Back
Top Bottom