Meya wa Ilala aikataa sheria mbovu ya ada za machinjio

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,507
55,021
13873222_1135131436566115_4703400256908667277_n.jpg
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mhe Charles Kuyeko amezikataa Sheria mdogo (Biashara ya Zao LA ngozi na Ada za machinjio) za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za mwaka 2015. Sheria hizo zilipitishwa na Baraza la Madiwani LA Ilala lililokuwa chini ya Jerry Silaa ambaye ni Meya mstaafu wa Ilala. Sheria hizo zilianzishwa chini ya kifungu cha 6(1) na 16(1) cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa (Sura ya 290) na kufuatiwa na Tangazo la Serikali Na.592 la 25/12/2015.

Meya Kuyeko ameikataa sheria hiyo kutokana na mchakato wake kukiuka taratibu na kanuni za uanzishwaji wa sheria ndogo za Manispaa husika. Moja ya taratibu alizozitaja Mhe. Kuyeko kuwa hazikufuatwa ni pamoja na wadau wa biashara ya Mifugo (Ng'ombe, mbuzi, kondoo na mazao yake ambayo ni nyama, Ngozi,Damu, pembe, mifupa, kwato na mbole) kutoshirikishwa ambao ndiyo wahusika wakuu. "Hii sheria ni mbovu sana, inaumiza wananchi wetu na hii ni sheria dhulumati kwa hiyo lazima irudi upya kwa wadau" amesema Kuyeko.
 
Back
Top Bottom