Meya wa Bukoba si raia wa Tanzania

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
Katika hali ya kushangaza na isiyotarajiwa, MEYA wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera si mtanzania.

Hili limewekwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye kwa sasa ni waziri wa mali asili na Utalii na mbunge wa Bukoba Mjini, Bwana Hamisi Kagasheki kwenye uwanja wa mashujaa siku ya Jumamosi tarehe 24/11/2012.

Waziri Kagasheki aliweka bayana kuwa akiwa waziri anayehusika na uhamiaji alimnyima uraia na hatai ya kusafiria na hata watoto wake walipoomba hati za kusafiria na japo hawastahili kupewa kwa kuwa wao nao si raia kwa kuwa baba yao si raia aliamua kuziweka sheria pembeni na kuwapa hati hizo.

Inadaiwa kuwa Meya huyu ni raia wa Uganda aliyetoroka nchini kwake akiwa na umri wa mika sita na ukulia Tanzania na kwa muda wote huo hakuwahi kuomba uraia ambapo alikuja kufanya hivyo alipotafuta madaraka ya udiwani.

Kutofautiana kwa Meya wa Bukoba na Mbunge wa Jimbo hilo kunatokana na ukweli kuwa meya huyu anadaiwa kuuweka ubunge wa Kagasheki matatani kwa yeye kuutaka pia huku kagasheki akilewa madaraka anadai hakuna jambo lolote linaloewa kupitishwa na madiwani wa halmashauri bila yeye kukubali. Kagasheki anajisahau kuwa yeye kama mbunge ni diwani pia na hivyo kama kolamu ya vikao vya halmashauri imetimia, maamuzi ynaweza kupitishwa bila yeye kuwepo.

Kutofautiana huku ndio kulipelekea Waziri Hamisi kuanika ukweli kuwa yeye nafahamu fika kuwa meya huyu si raia wa Tanzaia.
 
Inakuawaje CCM ni chama cha ma-genius halafu wanashindwa kilijua hilo? Labda bwana William Malecela atatujuza
 
Hilo sipingi hata alikuja kugombea huku kwetu KYERWA mwaka 2005 akawa anazunguka na masufuria ya pilau watu wakamuita bwana misosi(kura za maoni ccm) baadaye ikasemekana kuwa ni MHIMA(Mnyarwanda: wengine wanasema ) na cheo cha udaktari alijipa maana alifukuzwa akiwa form two.
 
Kagasheki alikua wapi siku zote kumuanika Diwali/MEYA. Adi alipokua tishio kimaslai.. Waache danganya toto tushawazoea hata bashe nae walisemaga sio raia!...
 
Kagasheki alikua wapi siku zote kumuanika Diwali/MEYA. Adi alipokua tishio kimaslai.. Waache danganya toto tushawazoea hata bashe nae walisemaga sio raia!...

Mwaka 2001 nakumbuka huyu bwana pamoja na mtu mmoja aliyeitwa Kabendera Shinani(mwandishi wa Bbc) waliambiwa warundi makwao, Kabendera alipewa tuhuma za mauaji ya halaiki nchini Rwanda hakua na jinsi akaamua kujiua kwa kujirusha majini.
 
.Waziri Kagasheki aliweka bayana kuwa akiwa waziri anayehusika na uhamiaji alimnyima uraia na hatai ya kusafiria na hata watoto wake walipoomba hati za kusafiria na japo hawastahili kupewa kwa kuwa wao nao si raia kwa kuwa baba yao si raia aliamua kuziweka sheria pembeni na kuwapa hati hizo..

Sitaki kuamini kabisa kwamba maneno haya ameyasema Mheshimiwa Waziri Kagasheki! Kwamba akiwa Naibu waziri wa mambo ya ndani aliamua kuweka Sheria pembeni na kumpatia DR. Anthony Amani hati ya Kusafiria ya Tanzania wakati akijua fika kwamba SIO RAIA wa Tanzania!!!

Mambo haya yanawezakana Tanzania tu. Zingekuwa nchi za wenzetu MAKINI Mh. Kagasheki anapaswa KUJIUZULU in the first place, kwa kuvunja sheria za nchi tena makusudi huku akijua. Hii ni kashifa kubwa sio kwa Dr. Amani bali kwa Waziri Kagasheki.

Nchii hii kweli hakuna utawala wa SHERIA, kila mtu anafanya apendavyo.
 
kama hangekuwa upande wa hk kumbe angekuwa raia mzuri,tanzania bwana ukubwa ni fimbo,safari tunayo kuifikia ukombozi wa kweli
 
Waziri Kagasheki aliweka bayana kuwa akiwa waziri anayehusika na uhamiaji alimnyima uraia na hatai ya kusafiria na hata watoto wake walipoomba hati za kusafiria na japo hawastahili kupewa kwa kuwa wao nao si raia kwa kuwa baba yao si raia aliamua kuziweka sheria pembeni na kuwapa hati hizo.

.

Kama anayosema Kagesheki ni ya kweli, basi, yeye Kagesheki anatakiwa ajiuzulu mara moja! Anatangaza kwa watanzania wote kwamba amekuwa akipindisha sheria za nchi kwa sababu binafsi, na kama si kutofutiana na huyo Meya mambo yangebakia chini ya carpet! Sasa tunaanza kupata mwanga kwanini wahamiaji haramu hawaishi nchini? Kumbe wanapata support toka kwa viongozi!
 
kama hangekuwa upande wa hk kumbe angekuwa raia mzuri,tanzania bwana ukubwa ni fimbo,safari tunayo kuifikia ukombozi wa kweli

Kinachoonekana hapa ni kwamba kuna mahali wametofautiana kwenye percentage na bwana meya (MGANDA) akamzidi bwana Hamisi na Hamisi akaamua kumtundika msalabani kwa kufichua swala hili ambalo kwa namna moja linakula kwa Hamisi kwa kupindisha sheria kama waziri na bwana meya kuongoza manispaa huku akiwa si raia
 
namsubili diwani naye afunguke ndo tutajua ukweli ni upi. hata bashe walisema sio raia lakini baadae ikaja gundulika ni raia. mawaziri walio pitia mambo ya ndani huwa wana ubabe sana. Nakumbuka masha alivyo mfanyia wenje nakosa amani kabisa na siwaamin watu wote walio pitia mambo ya ndani. mia
 
Back
Top Bottom