Scolari Ndenga
JF-Expert Member
- Aug 4, 2008
- 271
- 43
Katika hali ya kushangaza na isiyotarajiwa, MEYA wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera si mtanzania.
Hili limewekwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye kwa sasa ni waziri wa mali asili na Utalii na mbunge wa Bukoba Mjini, Bwana Hamisi Kagasheki kwenye uwanja wa mashujaa siku ya Jumamosi tarehe 24/11/2012.
Waziri Kagasheki aliweka bayana kuwa akiwa waziri anayehusika na uhamiaji alimnyima uraia na hatai ya kusafiria na hata watoto wake walipoomba hati za kusafiria na japo hawastahili kupewa kwa kuwa wao nao si raia kwa kuwa baba yao si raia aliamua kuziweka sheria pembeni na kuwapa hati hizo.
Inadaiwa kuwa Meya huyu ni raia wa Uganda aliyetoroka nchini kwake akiwa na umri wa mika sita na ukulia Tanzania na kwa muda wote huo hakuwahi kuomba uraia ambapo alikuja kufanya hivyo alipotafuta madaraka ya udiwani.
Kutofautiana kwa Meya wa Bukoba na Mbunge wa Jimbo hilo kunatokana na ukweli kuwa meya huyu anadaiwa kuuweka ubunge wa Kagasheki matatani kwa yeye kuutaka pia huku kagasheki akilewa madaraka anadai hakuna jambo lolote linaloewa kupitishwa na madiwani wa halmashauri bila yeye kukubali. Kagasheki anajisahau kuwa yeye kama mbunge ni diwani pia na hivyo kama kolamu ya vikao vya halmashauri imetimia, maamuzi ynaweza kupitishwa bila yeye kuwepo.
Kutofautiana huku ndio kulipelekea Waziri Hamisi kuanika ukweli kuwa yeye nafahamu fika kuwa meya huyu si raia wa Tanzaia.