Meya wa Bukoba si raia wa Tanzania

Katika hali ya kushangaza na isiyotarajiwa, MEYA wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera si mtanzania.

Hili limewekwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye kwa sasa ni waziri wa mali asili na Utalii na mbunge wa Bukoba Mjini, Bwana Hamisi Kagasheki kwenye uwanja wa mashujaa siku ya Jumamosi tarehe 24/11/2012.

Waziri Kagasheki aliweka bayana kuwa akiwa waziri anayehusika na uhamiaji alimnyima uraia na hatai ya kusafiria na hata watoto wake walipoomba hati za kusafiria na japo hawastahili kupewa kwa kuwa wao nao si raia kwa kuwa baba yao si raia aliamua kuziweka sheria pembeni na kuwapa hati hizo.

Inadaiwa kuwa Meya huyu ni raia wa Uganda aliyetoroka nchini kwake akiwa na umri wa mika sita na ukulia Tanzania na kwa muda wote huo hakuwahi kuomba uraia ambapo alikuja kufanya hivyo alipotafuta madaraka ya udiwani.

Kutofautiana kwa Meya wa Bukoba na Mbunge wa Jimbo hilo kunatokana na ukweli kuwa meya huyu anadaiwa kuuweka ubunge wa Kagasheki matatani kwa yeye kuutaka pia huku kagasheki akilewa madaraka anadai hakuna jambo lolote linaloewa kupitishwa na madiwani wa halmashauri bila yeye kukubali. Kagasheki anajisahau kuwa yeye kama mbunge ni diwani pia na hivyo kama kolamu ya vikao vya halmashauri imetimia, maamuzi ynaweza kupitishwa bila yeye kuwepo.

Kutofautiana huku ndio kulipelekea Waziri Hamisi kuanika ukweli kuwa yeye nafahamu fika kuwa meya huyu si raia wa Tanzaia.

Witch hunting will take us nowhere. Jali umaskini wako!
 
sasa alipataje hiyo hati ya kusafiria?kagasheki na wewe ni mtuhumiwa namba 1 katika hili sakata la kuwakaribisha wahamiaji haramu,maana umeyasema hayo mara baada ya meya kuutaka ubunge?ccm wote ni wezi baba JK mwizi mama Salama mwizi mtoto RITZ1 muuza sembe wajukuu ndio usiseme
 
Hamis KAGASHEKI kwa ushahidi wa maneno ya kinywa chake na kwa kukusudia kupindisha sheria za jamhuri ya muungano

(1) Ajiuzulu/ asimamishwe kazi
(2) Awajibishwe kwa kutumia madaraka vibaya
(3)Kuwa mbinafsi n.k.
 
labda walishindwana kuchukua chao mapema, kama kagasheki alionga mali yaani soda na pilau mkoa mzima hapo kuna nini si alitegemea chochote maana fedha zake alizozikomba ulaya ziliishia kwenye ubunge .
 
Na people za maeneo hayo kwa kupenda kuhongwa ni balaa! hahaha lazima Kagasheki imuume, na bado 2015 ubunge uko hatarini wakati pesa ikiwa haijarudi. Bora tembo waishe ilimradi pesa irudi, hahaha majangaa!
 
Katika hali ya kushangaza na isiyotarajiwa, MEYA wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera si mtanzania.

Hili limewekwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye kwa sasa ni waziri wa mali asili na Utalii na mbunge wa Bukoba Mjini, Bwana Hamisi Kagasheki kwenye uwanja wa mashujaa siku ya Jumamosi tarehe 24/11/2012.

Waziri Kagasheki aliweka bayana kuwa akiwa waziri anayehusika na uhamiaji alimnyima uraia na hatai ya kusafiria na hata watoto wake walipoomba hati za kusafiria na japo hawastahili kupewa kwa kuwa wao nao si raia kwa kuwa baba yao si raia aliamua kuziweka sheria pembeni na kuwapa hati hizo.

Inadaiwa kuwa Meya huyu ni raia wa Uganda aliyetoroka nchini kwake akiwa na umri wa mika sita na ukulia Tanzania na kwa muda wote huo hakuwahi kuomba uraia ambapo alikuja kufanya hivyo alipotafuta madaraka ya udiwani.

Kutofautiana kwa Meya wa Bukoba na Mbunge wa Jimbo hilo kunatokana na ukweli kuwa meya huyu anadaiwa kuuweka ubunge wa Kagasheki matatani kwa yeye kuutaka pia huku kagasheki akilewa madaraka anadai hakuna jambo lolote linaloewa kupitishwa na madiwani wa halmashauri bila yeye kukubali. Kagasheki anajisahau kuwa yeye kama mbunge ni diwani pia na hivyo kama kolamu ya vikao vya halmashauri imetimia, maamuzi ynaweza kupitishwa bila yeye kuwepo.

Kutofautiana huku ndio kulipelekea Waziri Hamisi kuanika ukweli kuwa yeye nafahamu fika kuwa meya huyu si raia wa Tanzaia.

Mbona hajarejea kwao
 
Back
Top Bottom