Meya wa Bukoba si raia wa Tanzania

..............

Inadaiwa kuwa Meya huyu ni raia wa Uganda aliyetoroka nchini kwake akiwa na umri wa mika sita na ukulia Tanzania na kwa muda wote huo hakuwahi kuomba uraia ambapo alikuja kufanya hivyo alipotafuta madaraka ya udiwani.
...........
Utasemaje si raia wakati tayari umesema ameishauomba na kukubaliwa ndio maana hata tume ikamruhusu kugombea baada ya kukosa pingamizi la kupinga sifa zake kama mgombea wa udiwani.
 
Kama anayosema Kagesheki ni ya kweli, basi, yeye Kagesheki anatakiwa ajiuzulu mara moja! Anatangaza kwa watanzania wote kwamba amekuwa akipindisha sheria za nchi kwa sababu binafsi, na kama si kutofutiana na huyo Meya mambo yangebakia chini ya carpet! Sasa tunaanza kupata mwanga kwanini wahamiaji haramu hawaishi nchini? Kumbe wanapata support toka kwa viongozi!

Ndugu yangu hilo lipo wazi biashara zote haramu zinasimamiwa na viongozi wa CCM.Hiki chama kikifa inabidi kushangilia badala ya kulia msiba..
 
Kumbe CCM haifanyagi screening ya wawakilishi wake?
Ilikuwaje mhamiaji haramu akapata post hiyo kubwa?

Mkuu mbona wako wengi tukisema waanze kupekua uraia wa makada wa hiki chama mbona watakimbia nchi....,ni kama mwamvuli wa kujificha ili usisumbuliwe, si unajue sera yao ya kulindana ukiwa ndani ya chama uko salama.
 
Tushishangae sana. Pengine ipo siku JK na Kinana wakikorofishana tukaambiwa kuwa mmoja wao sio raia! Eti niliweka sheria pembeni! Haka ka nchi bana!
 
Katika hali ya kushangaza na isiyotarajiwa, MEYA wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera si mtanzania.

Hili limewekwa wazi na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye kwa sasa ni waziri wa mali asili na Utalii na mbunge wa Bukoba Mjini, Bwana Hamisi Kagasheki kwenye uwanja wa mashujaa siku ya Jumamosi tarehe 24/11/2012.

Waziri Kagasheki aliweka bayana kuwa akiwa waziri anayehusika na uhamiaji alimnyima uraia na hatai ya kusafiria na hata watoto wake walipoomba hati za kusafiria na japo hawastahili kupewa kwa kuwa wao nao si raia kwa kuwa baba yao si raia aliamua kuziweka sheria pembeni na kuwapa hati hizo.

Inadaiwa kuwa Meya huyu ni raia wa Uganda aliyetoroka nchini kwake akiwa na umri wa mika sita na ukulia Tanzania na kwa muda wote huo hakuwahi kuomba uraia ambapo alikuja kufanya hivyo alipotafuta madaraka ya udiwani.

Kutofautiana kwa Meya wa Bukoba na Mbunge wa Jimbo hilo kunatokana na ukweli kuwa meya huyu anadaiwa kuuweka ubunge wa Kagasheki matatani kwa yeye kuutaka pia huku kagasheki akilewa madaraka anadai hakuna jambo lolote linaloewa kupitishwa na madiwani wa halmashauri bila yeye kukubali. Kagasheki anajisahau kuwa yeye kama mbunge ni diwani pia na hivyo kama kolamu ya vikao vya halmashauri imetimia, maamuzi ynaweza kupitishwa bila yeye kuwepo.

Kutofautiana huku ndio kulipelekea Waziri Hamisi kuanika ukweli kuwa yeye nafahamu fika kuwa meya huyu si raia wa Tanzaia.

Political expediency at its very best!!
Poor Hamis Kagasheki; when it served him right, Mayor Amani was OK! He could bend rules and play blind to issues about his nationality?! na huyo ni waziri wa mambo ya ndani anaueleza umma wa watanzania! mtu mwenye dhamana ya kuangalia usalama wa raia na mali zao!!?? I think Hamis has taken leave of his faculties. no wonder CCM na serikali yake are wallowing in a can of worms.

Balozi Kagasheki anakiri kwamba ni yeye aliyemfuata Amani agombee udiwani na kumtosa Luhangisa, sasa ni hadithi ya bedui na Ngamia.

Hii ndio kansa inayoitafuna CCM; no single leader in CCM is beyond reproach; Lets wait and see how this story unravels!!
 
masikini wanyamapori wetu,..jangili amepewa mamlaka ya kuzunguka mbugani na bunduki
 
Kagasheki amgwaya Dk. Slaa
• Akataa miradi ya meya akidai inanyanyasa wananchi


na Mwandishi wetu




WAZIRI wa Maliasili na Utalii, ambaye pia na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki (CCM), ameapa kuwa hayuko tayari kusutwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kutokana na mikataba mibovu aliyoingia Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory Amani.

Akihutubia mkutano wa hadhara mwishoni mwa wiki mjini Bukoba, Kagasheki alisema kuwa haungi mkono miradi ya kuvunja soko kuu la manispaa hiyo na wa upimaji wa viwanja 5,000.

Katika kile kinachoonekana kama msigano ndani ya CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Waziri Kaghasheki alisema wazi kuwa miradi anayoitekeleza Meya Amani inawanyanyasa wananchi.

Huu ndiyo umekuwa msimamo wa CHADEMA tangu ilipoibuliwa miradi hiyo, ambapo viongozi wake wamekuwa wakiipinga wakimlalamikia Meya Amani kwa usiri wake katika kuingia mikataba.

Tanzania Daima pia limewahi kuandika kuhusu utata wa miradi hiyo mapema Juni mwaka huu, lakini Meya Amani vile vile alifika hatua ya kudai gazeti hili linatumiwa kisiasa na CHADEMA kummaliza.

Hatua hiyo pia inakuja zikiwa ni siku chache tangu kuzuka mtafaruku ndani ya kikao cha Baraza la Madiwani wa manispaa hiyo, ambapo Meya Amani, aliwageuzia kibao baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kuwa, wamekuwa wakimhujumu ili asitekeleze miradi hiyo.Waziri Kagasheki ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Meya Amani, juzi aligeuka mbogo na kusimama upande wa wananchi, akisema kuwa kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo, alizungumza na meya huyo na kumtahadharisha kuwa mradi wa viwanja usiguse mashamba ya watu.

“Mnapokwenda kwenye mikataba ya namna hii na kusema mbunge ni kitu gani, siwezi kukubali nikae kimya, kesho Dk. Willibrod Slaa aje hapa aanze kuzungumzia ufisadi huu wakati mimi niko hapa,” alisema.

Alifafanua kuwa katika manispaa hakuna uongozi shirikishi, na kuwa yeye amechaguliwa na wananchi wengi wa jimbo zima wakati Amani amechaguliwa na watu wachache wa kata moja tu.

Wakati Kagasheki akirusha madongo hayo, Meya Amani alikuwa ameketi jukwaa kuu na kutulia kama hasikii kinachozungumzwa, na baada ya mkutano kumalizika aliondoka huku akicheza muziki wa chama hicho uliokuwa ukipigwa.

“Mchezo mnaoanza kuucheza ndani ya CCM utapoteza jimbo, mwaka 2000 jimbo lilipotea na kuchukuliwa na wapinzani kwa sababu ya wana-CCM wenyewe, kwa sababu ya vurugu na uchu wa kutaka madaraka, na sasa naona mmeanza mchezo huo huo,” alionya.

Waziri Kagasheki aliongeza kuwa, katika kutekeleza mradi wa upimaji viwanja, mwenye ardhi anapaswa kutendewa haki baada ya kupima kiwanja chake na kuwa lazima atetee haki hiyo ya mnyonge ila si kwamba anapinga maendeleo kama inavyodaiwa.

“Manispaa wamekwishasaini mkataba wa kuchukua mkopo wa sh bilioni 2.2 kutoka Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Nchini (UTT) kwa masuala ya viwanja. Mkataba unaoeleza hayo uko wapi, nani atalipa mkopo huo? Lazima ieleweke,”alisema.

Sakata hilo la Meya Amani kuwa msiri katika uingiaji mikataba ya baadhi ya miradi limekuwa likilalamikiwa sana na wananchi wa manispaa hiyo, ingawa yeye aliwahi kunukuliwa na gazeti hili akisema si lazima wajue.

Ni katika utata huo Waziri Kagasheki alisema kwa sasa kuna taarifa nyingine za kuwa wako katika mchakato wa kupata tena mkopo wa sh milioni 768, lakini akasisitiza kwamba mambo hayawezi kwenda kienyeji namna hiyo.

Alisema kuwa kuhusu kuvunjwa na kujengwa upya soko la kisasa la Bukoba kwa sasa pia haungi mkono, maana kuna watu ambao wanatakiwa kujua haki zao ni zipi, na kwamba yeye atakuwa kiongozi wa ajabu akikubali livunjwe katika mazingira kama hayo.

Kagasheki alisema kuwa kwanza katika eneo wanakotangaza kujenga jengo hilo la ghorofa hapajafanyiwa utafiti wa kitaalamu ili kuonesha kama upo uwezekano wa kujenga jengo la namna hiyo, akahoji watasemaje endapo itabainika kuna tatizo wakati wamekwishasaini mikataba.

Msimamo huo wa Kagasheki ulionekana kuwashangaza wananchi wengi kwani ni siku chache zimepita alifanya mkutano akiwa na meya huyo na kuwaomba wananchi wamuunge mkono katika mradi wa kuvunja soko, akidai ni utekelezaji wa moja ya ahadi zake.

“Nawashukuru wazazi wangu kwa kunipeleka shule, wanaotaka kubomoa na kujenga soko jipya hawajui watalijenga kwa muda gani, kuna pia suala la mahakama imesema italiltolea suala hilo maamuzi Machi mwakani,” alisema.

Kagasheki alisisitiza kuwa, hatakubali kuburuzwa mpaka ajue hatima ya mtu wa kawaida, kwamba suala la soko likienda vibaya hata viongozi wa CCM waliopo madarakani watakwenda na maji.

“Wanasema mengi eti sitaki maendeleo, mara namchukia Amani. Siwezi kumchukia mtu ambaye katika uchaguzi uliopita mimi ndiye nilimtafuta na kumwomba agombee udiwani na baadae nikaweka jitihada zangu na kuhakikisha anakuwa meya, kwa nia nzuri na kusababisha niingie katika uhasama na Samwel Ruangisa aliyekuwa meya,” aliongeza.Alisema kuna wakati zilitoka taarifa kuwa Amani si raia wa Tanzania, na kwamba naye alikiri na kuomba kupewa uraia na nyaraka zipo hadi wizarani zinazoonesha alivyosimamishwa katika nyadhifa alizokuwa nazo kwa madai kuwa si raia.

“Kama namchukia mbona watoto wake walikwenda kuomba hati za kusafiria Uhamiaji wakanyimwa kwa kuwa wao si raia, kwamba wakati baba yao anawazaa alikuwa hajawa raia wa Tanzania, lakini nilimsaidia na watoto wake wakapata uraia,” alisema.Mgororo huo mpya wa viongozi hao, umesababisha CCM kuwa na makundi makubwa matatu, kundi la kwanza likiwa la aliyekuwa meya wa manispaa hiyo, Ruangisa, la pili ni la Meya Amani na la tatu ni la Kagasheki.

Hata hivyo, wakati Kagasheki akiweka msimamo wake, juzi Meya Amani alisisitiza kuwa msimamo wa manispaa wa kubomoa soko na kulijenga upya uko pale pale na kuwa yeye hatekelezi maagizo ya mbunge bali vikao.

Katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi Jumatano wiki iliyopita, Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Hamis Kaputa alisema mipango ya utekelezaji wa mradi wa soko inakwenda vizuri na kuwa wanaendelea na kuandaa mazingira ya kuwahamisha wafanyabiashara walioko katika soko hilo.

Aidha katika kikao hicho, madiwani walikubaliana soko hilo linalotarajiwa kujengwa kwa muda wa miezi 18, kwa gharama ya sh bilioni 12 bilioni, lianze kuvunjwa Januari 15 mwakani.




Video link.
PART 1 HOTUBA YA MH KAGASHEKI UWANJA WA UHURU 24/11/2012 - YouTube!

Mtazamo wangu.
Being born in Bukoba,Buyekera and lived almost 70% of my life down there,I love this show.This is how the former CCM MP(Katalaiya) went down.So far so good, I will be the first to arrange funeral in case our hated party(CCM) dies(Kuanzia sasa naanza kutembea na ndizi mbivu kwenye kanzu).Amani is CORRUPT as his party, and Kagasheki is another guy suffering from Romnesia na bingwa wa kukurupuka kwa kuangalia upepo.Kagasheki was not a politician but a made guy from father in law,Mzee Ruksa.
 
meya wa ccm, waziri naye ccm, mmoja raia mwingine sio, ilikuwaje kwenye kupitisha majina ya kugombea, na inakuwa vipi leo ndo wanakurupuka kusema sio raia, danganya toto inaendelea, kama alimkatalia uraia wakati ule hivi ni hatua zipi alichukua na ilikuwaje akawakubalia watoto wa mhusika, conclussion ni kwamba hapo hatuna waziri
 
CCM inaeleweka, ina makada kutoka mataifa mbalimbali. Kuna waarabu, wahindi, wasomali na sasa mganda. Nafikiri hiki si kwamba ni chama kikongwe tu, bali pia ni chama cha siasa cha kimataifa. Mtu anaweza kutoka taifa lolote na akawa kada wa CCM. Hatari!!!!
 
Japo no one's perfect ila hawa jamaa wamezidi..! Na hii tabia ya kuanikana hadharani kwamba sio raia pindi tu mnapokosana ni tabia ya muda mrefu sana.. Mmeshazoea wananchi hawafuatilii wala kusema lolote kuhusu upuuzi wenu huu..! Well sio sasa tena.. Wananchi wameamka na wanaelewa haki zao na pale viongozi wao wanapokosa credibility..! Mlisahau ule usemi wa "unaweza kuwadanganya baadhi ya watu kwa muda fulani.. Bali huwezi kuwadanganya watu wote na ciku zote".. Mmefikia ukingoni sasa..
 
Kagasheki inabidi afikishwe mahakamani kwa kuvunja sheria ya uhamiaji,utampaje mtu uraia kwa njia za panya tena unakiri hadharani..!!
 
Mtanzania ni Nani? Julius Nyerere? Benjamin Mkapa? Ali Hassan Mwinyi? Jakaya Kikwete? au Kingunge Ngomable?

Nani anyefahamu kwa uhakika kuwa yeye ni Mtanzania "HALALI"? Stupid Thinking...!
 
Back
Top Bottom