Meya wa Bukoba si raia wa Tanzania

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, hata Benjamin William Mkapa siyo raia wa Tanzania, yeye ni M'meto kutoka Msumbiji.
 
Ni hv MH. Rais anatakiwa kumfuta kazi mara moja kagasheki kwa kuidhalilisha serikali..pu...fu kabisa huyu waziri!natamani awe mbele yangu nimchape kofi
 
Wote wapuuzi!

Tena wapuuzi kweli kweli na CCM yao. Leo Kagasheki amenukuliwa na magazeti akisema hivi:-

"Wanasema mengi eti sitaki maendeleo, mara namchukia Amani. Siwezi kumchukia mtu ambaye katika uchaguzi uliopita mimi ndiye nilimtafuta na kumwomba agombee udiwani na baadae nikaweka jitihada zangu na kuhakikisha anakuwa meya, kwa nia nzuri na kusababisha niingie katika uhasama na Samwel Ruangisa aliyekuwa meya," aliongeza (Tanzania Daima; 26 Nov. 2012; Pg. 04).

Hiyo ndiyo kauli ya Kagasheki ambaye huyo aliyetafutwa naye anadaiwa na hao hao (CCM) waliomtafuta, kumptisha kwenye vikao hadi kuwa meya eti leo sio raia! Muda wote huo walikuwa wapi? Hizi siasa za maji taka za CCM hazina mustakabali mwema kwa taifa letu. Ndio maana nadiriki kuunga mkono hoja ya WOTE WAPUUZI.
 
Nimenukuu baadhi ya maneno aliyoyasema waziri Kagasheki juu ya Meya Amani.

“Kama namchukia mbona watoto wake walikwenda kuomba hati za kusafiria Uhamiaji wakanyimwa kwa kuwa wao si raia, kwamba wakati baba yao anawazaa alikuwa hajawa raia wa Tanzania, lakini nilimsaidia na watoto wake wakapata uraia,” alisema.
 
Nimekumbuka mizengwe ya Masha kwa mhe.Wenje.Hawa watu nadhani huwa hawatumii akili
 
Wanabodi, kitendo cha waziri Kagasheki kukiri mbele ya umma kwamba alipindisha sheria na kuwapa hati za kusafiria wahamiaji haramu, ni either ajiuzuru au Rais amfukuze kazi mara moja na asipomfukuza kazi naomba nguvu ya umma imsaidie rais kumwondoa huyu waziri
 
Wanabodi, kitendo cha waziri Kagasheki kukiri mbele ya umma kwamba alipindisha sheria na kuwapa hati za kusafiria wahamiaji haramu, ni either ajiuzuru au Rais amfukuze kazi mara moja na asipomfukuza kazi naomba nguvu ya umma imsaidie rais kumwondoa huyu waziri

tuone sasa nguvu ya umma nanguvu ya dola nani zaidi
 
Hii nchi inaendeshwa kwa pombe kama fuel.

Didas Masaburi aliwahi kusema kuwa endapo wabunge wa DAR wakiendelea kumfuatafuata na yeye atasema mambo yao. Kauli hiyo inaonesha kuwa kuna mambo mabaya anayajua lkn hayasemi mpaka achokozwe. Mamlaka zilimsikia na hazikuamua kitu.

Leo Kagasheki anasema fulani si raia na anasema alipindisha sheria kwa manufaa yake lkn hutasikia hilo likihojiwa.
 
Mwaka 2001 nakumbuka huyu bwana pamoja na mtu mmoja aliyeitwa Kabendera Shinani(mwandishi wa Bbc) waliambiwa warundi makwao, Kabendera alipewa tuhuma za mauaji ya halaiki nchini Rwanda hakua na jinsi akaamua kujiua kwa kujirusha majini.
Morinyo UPO JUU MKUU, HIYO HADITHI YA kABENDERA Shinani nimeipata kwa uhakika kwa mdau mzuri wa siasa za tANZANIA , uGANDA NA rWANDA
 
Last edited by a moderator:
Ameenda mbali kwa kusema kuwa yeye AMEMCHONGA Meya mwenyewe ikiwa ni pamoja na kumpa uraia, hata na watoto wake kawapatia uraia yeye, akasema amemfanya awe meya na kusababisha agombane na Mzee Luangisa. Wadau wanasema wamezidiana kwenye maslahi
 
Utawala wa sheria huwa haupindishi sheria, sasa kama waziri alipindisha sheria, hana budi kuwajibika sasa, ili kuepusha zengwe siku za usoni.:rofl:
 
Back
Top Bottom